TAASISI ya Sekta Binafasi Tanzania (TPST)leo imeendesha semina ya mafunzo ya elimu ya wajasiliamali kwa vikundi
vya Tawsei kwa wanachama wake wapato 50 kutoka maeneo mbalimbali katika kata ya Maramba wilayani Mkinga.
Akizungumza ufunguzi wa mafunzo hayo,Mshauri Mwelekezi wa mafunzo ya Biashara(BD Provider)Jane Gonsalves amesema
mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiliama mali hao pamoja na kujengea uwezo katika uendelezaji wa shughuli
zao za ila siku.
Gonsalves amesema suala la ujasiria mali ni ajira kwa vijana kutokana na ajira kuwa ngumu hivyo kutokana na kuwepo
kwa hali hiyo katika jamii yetu taasisi hiyo imeona bora kuanzisha ajira wa vijana kwa kuwapatia elimu ya ujasiria
mali ili kuwewezesha kufanya shughuli zao na kuweza kupata mafanikio.
Amesema umuhimu wa sekta binafasi inajumuisha wafanyabiashara wa aina mbalimbali wakubwa,wakati na wadogo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa ajira zaidi ya asilimia 80 kwa watanzania wote katika kujipatia riziki za kila siku.
Aidha ameongeza kuwa sekta binafasi ni mwajiri wa hiari hususani kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wengi wao wakiwa wameingia katika sektta binafsi bila maandalizi ya kutosha ya elimu ya ujasiriamali na kushindwa kabisa kuendesha biashara bila kujua kwamba mafanikio katika biashara yanataka maandalizi ya muda mrefu na ambayo ni makini.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo,Afisa Tarafa wa kata ya Maramba wilayani Mkinga,Nisa Mwakibete
amesifu jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kuwajengea uwezo wajasiriamali na kuwataka washiriki kuyatumia vema
mafunzo hayo katika kuendesha shughuli zao kila siku pamoja na kuhakisha wanapata mafanikio kwa kujiwekea malengo
endelevu.
Kwa upande wake,Mratibu wa Asasi ya kiraia isiyokuwa ya kiserikali ya Tanzania Woman For Self Imlietive,Benadeta
Choma amesema asasi yao imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wajasiria mali ili waweza kujikomboa kutoka
katika hali duni na kwenda katika hali nzuri kimaisha.
Choma amesema asasi hiyo pia imeona bora ijikinge pembezoni ili kuweza kuwatumikia wananchi katika maeneo yao pamoja na kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye jamii.
Semina hiyo imeanza leo na itakuwa ni ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiria mali waliopo kwenye
kata hiyo.
Mwisho.
EmoticonEmoticon