Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo, Demetrius Mapesi (kulia),akimtwisha
ndoo ya maji Radhia Said baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji
mwishoni mwa wiki kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL. Kushoto ni
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,
Joseph Nicholaus
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph
Nicholaus (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo,
Demetrius Mapesi wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisika
cha maji kiolichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 29 kwa msaada wa TBL
katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Wanaopiga
makofi ni wananchi wa eneo hilo wakionekana kufurahishwa na msaada huo
muhimu kwani wataondokana na tatizo la maji ambapo walikuwa wakitembea
zaidi ya KM 2 kununua maji ndoo moja sh. 700. Katika Kisima hicho
watakuwa wananunua ndoo moja ya maji kwa sh. 50.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,
Joseph Nicholaus, akifungua maji kwenye bomba lililounganishwa kwenye
kisima hicho. Kisima hicho kina uwezo wa kutoa zaidi ya lita 5000 za
maji kwa saa. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO
BLOG
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph
Nicholaus (kushoto), akimtwisha Cecilia Dominic ndoo ya maji baada ya
kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King’ongo, wilayani
Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa
msaada wa TBL.
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph
Nicholaus (kushoto), akimtwisha Rehema Mohamed ndoo ya maji baada ya
kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King’ongo, wilayani
Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa
msaada wa TBL.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto),
akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kata hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya MO Resources Ltd, Onesmo Sigalla 9kushoto)
akimkabidhi kufuli na funguo pamoja na nyaraka zinginezo za kisima
hicho, Meneja Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholas ambaye
pia alimkabidhi Mwenyekiti Mwenyekiti wa Serikali ya Mataa wa King’ongo,
Mapesi (kulia). Kampuni hiyo ndiyo iliyopewa tenda ya kujenga kisima
hicho.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (wa pili kushoto),
akipongezwa na mwananchi wa kata hiyo, Abdalah Mangosongo kwa msaada huo
wa TBL.
Ofisa
Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu (kushoto), akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo, ambapo alisema kuwa TBL, mwaka huu imetenga sh. mil.
700 kwa ajili ya kuisaidia jamii nchini kuboresha sekta ya maji.
Share this
EmoticonEmoticon