SUMVE WAOMBWA KUPIGA KURA NYINGI ZA HESHIMA KWA CCM-DKT.BITEKO

September 22, 2025 Add Comment


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Taifa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Jimbo la Sumve, wilaya ya Kwimba Mkoani  Mwanza kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kuwa Chama hicho kimefanya jitihada kubwa ya kuwaletea maendeleo.

Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 21, 2025 Mwanza wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve kwa tiketi ya CCM, Moses Bujaga ikiwa ni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Amesema Serikali ya CCM imeendelea na jitihada zake za  kujenga Kituo cha Reli ya Kisasa ya SGR kwa ajili ya kupokea mizigo itakayosafirishwa kwenda maeneo mbalimbali pamoja na kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Mwanza ili kufungua uchumi wa mkoa huo kwa ujumla.


Aidha, imehakikisha wananchi wa vijiji vyote katika Jimbo hilo wanapata umeme ikiwa ni pamoja na usambazaji umeme katika vitongoji.

Dkt. Biteko ameendelea kusema Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na mtu wa vitendo  zaidi, ambapo katika Jimbo la Sumve pamoja na miradi mingine amejenga shule za msingi 75, vituo vya afya vitano pamoja na barabara za lami ili kusafirisha mazao kwa urahisi kufika sokoni.


“ Maendeleo haya hayasemwi tu yanaonekana na sisi tunataka kuleta maendeleo na katika kipindi cha miaka mitano ijayo Dkt. Samia anataka kutekekeza miradi mingi zaidi ya maendeleo. Nawaomba Sumve pigeni kura nyingi kwa wagombea wa CCM ili kuheshimisha chama chetu na mkimaliza kupiga kura mtudai maendeleo,” amesisitiza Dkt. Biteko.


Ameongeza kuwa zoezi la kupiga kura ni la uwekezaji wa maendeleo na kuwa uchaguzi wa mwaka huu una uhusiano wa moja kwa moja na maisha na maendeleo ya watu. Hivyo amewataka wananchi hao kumpigia kura mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve kwa tiketi ya CCM, Moses Bujaga, Dkt. Biteko amemtaja kuwa ni mtu makini, mtulivu na msomi mwenye umahiri katika katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za wananchi hivyo ifikapo Oktoba 29, wajitokeze kumchagua kwa kura nyingi.


Naye, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve, Moses Bujaga  ameishukuru CCM  kwa kumteua kugombea nafasi hiyo na atakapochaguliwa atafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kitimiza jukumu la kuleta maendeleo.


Naye mgombea Ubunge  wa Jimbo la Kwimba, Cosmas Bulala amesema kuwa Kwimba ni kitovu cha maendeleo katika Mkoa wa Mwanza na kuwa ili kuendelea kupata maendeleo zaidi Oktoba 29 wananchi wawachague tena wagombea wa CCM.


Mwisho.

MAJIKO BANIFU TEKNOLOJIA YA KISASA INAYOTUMIA MKAA KIDOGO

September 22, 2025 Add Comment


*📌Yanapunguza sumu ya mkaa kwa watumiaji*


*📌 Ni rafiki kwenye utunzaji wa mazingira*


*📌Majiko banifu 1000 kuuzwa kwa bei ya ruzuku katika Maonesho ya Madini Geita*


📍Geita


Imeelezwa kuwa majiko banifu yanayotolewa kwa bei ya ruzuku na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni majiko yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kulinganisha na majiko mengine ya mkaa. 


Hayo yamebainishwa na Wataalam kutoka REA wanaoendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. 

Aidha, majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo inasaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa. 

Halikadhalika, majiko banifu yanasaidia utunzaji wa mazingira, ni rahisi kwa matumizi yanadumu kwa muda mrefu bila kupata changamoto ya kuharibika kwa watumiaji. 


Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.



Majiko banifu yanatolewa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 6,195 kwa kuwa Serikali imeweka ruzuku ya bei katika majiko hayo ili wananchi waweze kuyatumia na kuyapata kwa urahisi ambapo kabla ya ruzuku yalikuwa yanauzwa kwa shilingi 41,300.


Mwisho

BALOZI MATINYI AKUTANA NA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI SWEDEN

September 22, 2025 Add Comment


 Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi (katikati aliyekunja mikono), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wapya wa Tanzania waliokuja kusoma shahada za uzamili katika fani mbalimbali nchini Sweden katika muhula wa mwaka 2025/26. Kushoto kabisa ni maafisa watano wa Ubalozi wa Tanzania. Balozi Matinyi aliwaandalia wanafunzi hao hafla fupi katika makazi yake jijini Stockholm leo Jumapili tarehe 21 Septemba, 2025, ili kuwaeleza umuhimu wa kutumia maarifa na fursa waliopata kwa faida ya taifa (Picha kwa hisani ya Ubalozi).

TUME YAKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU MAFINGA MJI, WASISITIZWA WELEDI

September 22, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 21, 2025 ametembelea  Halmashauri ya Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya Mji huo kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.  

Jaji Mwambegele yupo Mkoani Iringa kukagua maandalizi hayo na kutazama kampeni za wagombea katika majimbo ya Mkoa wa Iringa 

kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume,Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu. 

"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"

Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa Bi. Nuru Sovella akizungumza jambo wakati wa utoaji wa taarifa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele
Msimamizi Jimbo la Mafinga Mjini Mwalimu Doroth Kobelo akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (katikati) kulia ni Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Bi. Nuru Sovella. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mafinga Mjini ambapo aliwasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mafinga Mjini ambapo aliwasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi. 
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Bi. Nuru Sovella akisikiliza kwa umakini 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia sehemu ya vifaa vya uchagzi ambavyo vimeshapokelewa. 

MHE. MCHENGERWA AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI MSASANI, MWANANYAMALA. AMWOMBEA KURA RAIS SAMIA

September 21, 2025 Add Comment

Na Mwandishi Wetu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM kuipitia Mkoa wa Pwani, na Waziri wa TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amewaomba watanzania kumpigia kura zote za ndiyo Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amefanya kazi kubwa ya kuwaletea watanzania maendeleo.

Mhe. Mchengerwa ametoa rai hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za udiwani katika kata za Msasani na Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Akimtambulisha na kumnadi mgombea wa udiwani wa kata ya Msasani Yusufu Hamisi Yusufu amesema kata ya Msasani ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) toka enzi za Mwalimu Nyerere hivyo wananchi hawana budi kulinda heshima hiyo kwa kukipigia kura za ndiyo Chama hicho katika ngazi zote kuanzia urais, ubunge na udiwani.

"Ndugu zangu naomba tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu tusibabaishwe, tuungane kupiga kura zote za ndiyo kwa Rais Samia, wabunge na madiwani wa CCM ili tuendelee kuboresha maisha ya watanzania." Amesisitiza Mhe Mohamed Mchengerwa
Aidha, amewasihi wananchi kumchagua mgombea wa udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM ndugu Yusufu huku akisisitiza kuwa mtu hodari na mtendaji zaidi kuliko maneno.

Akiwa Mwananyamala Mhe. Mchengerwa amewaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua aliyekuwa diwani na Meya wa Kinondoni ndugu Songoro ili aendelee kuwaletea maendeleo pale alipoishia.

Amesema kutokana na uchapakazi wake ndiyo maana pia aliweza kuchaguliwa kuwa Meya wa Kinondoni hivyo hana shaka kuwa hata kipindi hiki atarejea katika kiti hicho.

Amewasihi wananchi kuachana na siasa zisizo za maendeleo na badala yake kukipigia kura CCM kwani tayari kimeshawafanyia mambo makubwa ya maendeleo wananchi kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ametaja baadhi ya maeneo makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki kuwa ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu, SGR, kukamilika kwa bwawa la Mwalimu Nyerere, Elimu pamoja na Afya.

Msanii chipukizi wa Singeli nchini, Dogo Paten ametumbuiza na kukonga nyoyo za wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kata ya Msasani.