NCAA YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA UTALII KUHUSU MATUMIZI YA MFUMO MPYA WA SAFARI PORTAL V2
Na Kassim Nyaki, NCAA.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Mei, 2025 kwa wadau wa Utalii kuhusiana na matumizi ya mfumo mpya wa *Safari Portal V2* ulioboreshwa kutoka mfumo wa zamani wa Safari Portal.
Akifungua Mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Huduma za Utalii na masoko NCAA, Afisa Uhifadhi Mkuu Peter Makutian ameeleza kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wadau wote wa Utalii kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa makusanyo ya mapato yatokanayo na shughuli za Utalii ambao umeboreshwa ili kurahisisha utoaji huduma kwa wadau wote wanaofanya kazi na NCAA.
"Tumeboresha mfumo wetu wa makusanyo ya mapato ya Utalii na utaaanza kutumika kuanzia tarehe 31/05/2025, kwa hiyo ni muhimu wadau wetu wanaopata huduma kupitia mfumo huu wawe na uelewa ya maboresho yaliyofanyika na kuwasaidia namna ya kuhamisha taarifa zao kwenye mfumo mpya kabla ya tarehe ya kuanza mfumo huo" alilisitiza Makuatian.
Makutian ameongeza kuwa sababu zilizopelekea kuboresha mfumo huo ni kuendana na mabadiliko ya kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano sambamba na kuzingatia mapendekezo ya Wadau wa utalii ambao ndio watumiaji wakuu wa mfumo huo.
Mafunzo hayo yameshirikisha makundi mbalimbali katika mnyororo wa sekta ya utalii ikiwemo Waongoza watalii, wamiliki wa kampuni za utalii, madereva wa utalii, wamiliki wa hoteli na wadau wengine wanaohusika na sekta ya Utalii.
Wadau wa utalii walioshiriki mafunzo hayo wametoa pongezi kwa uongozi wa NCAA kwa maboresho ya mfumo huo ambao umerahisisha taratibu za malipo bila kutumia mda mrefu wanapokuwa na shughuli za utalii na wageni ndani ya hifadhi ya Ngorongoro
DKT.BITEKO ATAJA MAENEO SITA YA VIPAUMBELE UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2020/2025
📌 CCM yajivunia kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii
📌 Rais Samia asema CCM kuzindua Ilani yake kesho
📌 CCM yazalisha ajira 800,000 kwa vijana 2020/2025
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita aliyowasilisha ni ya mwisho katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020.
Amesema hayo Mei 29, 2025 wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa - 2025 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Ametaja maeneo sita muhimu ya vipaumbele katika utekelezaji wa Ilani hiyo ya CCM kuwa ni pamoja na kulinda na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa.
Dkt. Biteko ameendelea kwa kusema kuwa eneo lingine ni kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.
Aidha, kipaumbele kingine “ Kuleta mageuzi ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji, umeme na makazi vijijini na mijini na kutengeneza ajira zisizopongua milioni nane katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vijana,” ameongeza Dkt. Biteko.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwemo nchi kuendelea kuwa na amani, umoja na mshikamano pamoja na kuendelea kuenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kudumisha Muungano wa Tanzania.
“ Vilevile, Serikali imeendelea kuimarisha demokrasia, utawala bora na haki za binadamu kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na hivyo kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari ili kuwezesha wananchi kupata habari kwa wakati,” amesema Dkt. Biteko.
Ameendelea kusema kuwa mafanikio hayo yamechagizwa na falsafa aliyoianzisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya 4R ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga Upya.
Amesisitiza “ Falsafa hiyo imekuwa dira na nguzo muhimu ya kisera katika kuijenga upya Tanzania yenye mshikamano, haki na maendeleo endelevu kwa misingi ya demokrasia na ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya msingi ya Taifa.”
Kupitia mkutano huo Dkt. Biteko alielezea mafanikio ya Rais Samia kitaifa na kimataifa hususan katika sekta ya nishati kwa kuwa kinara wa nishati safi ya kupikia barani Afrika.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Mkutano Mkuu huo ni sehemu muhimu ya maandalizi ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
“ Kesho tutafanya uzinduzi wa Ilani tutakayoinadi kwa wananchi ili kutupa nafasi nyingine ya kuongoza kwa miaka mitano,” amesema Dkt. Samia.
Amebainisha kuwa Ilani hiyo imehusisha vipaumbele vya Chama na kuwa kabla ya kuiwasilisha kwa wajumbe wameona ni muhimu kupitia utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2020 hadi 2025.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema lengo la mkutano huo ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2020 hadi 2025, kuzindua Ilani mpya 2025 hadi 2030 na kupitia maboresho machache ya Katiba ya CCM.
Aidha, Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umehudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja wawakilishi wa vyama rafiki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, China na Korea ya Kaskazini na Urusi.
MWISHO
DCEA YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA KUPITIA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA MITAA SAME
Mradi wa Miaka 13 wa Amend Wazidi Kutoa Matunda Tanzania
habariWADAU wa usalama wa barabarani wametoa wito wa kuanzishwa kwa mjadala wa kitaifa kuhusu namna ya kudhibiti ajali za barabarani, wakisisitiza kuwa vifo na majeruhi vinavyotokana na ajali hizo hususani kwa Watoto, haviwezi kuvumilika tena katika jamii ya Watanzania.