TPAWU YATAKA MCHAKATO KIMA CHA CHINI SEKTA BINAFSI UHARAKISHWE

May 27, 2025 Add Comment

 

 Mwenyekiti TPAWU Taifa Daniel Bariyanka Joachim akizungumza kwenye kikao hicho

Na Godwin Myovela, Morogoro

CHAMA cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo nchini (TPAWU) kupitia kikao cha Baraza Kuu la chama hichoTaifa, kimeomba kuharakishwa kwa mchakato unaoendelea wa kupanga kima cha chini cha mshahara sekta binafsi, kuzingatia maoni ya wadau-sambamba na kuhakikisha kima hicho kutopungua Tsh. 350,000 kwa mwezi, ili kusaidia kumudu gharama za maisha.

Mwenyekiti TPAWU Taifa, Daniel Joachim, alitoa tamko hilo wakati wa kikao hicho kilichofanyika mkoani hapa mwishoni mwa wiki, ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza baraza hilo limezingatia hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi mwaka huu, kuhusu utaratibu wa kisheria unaoendelea kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.

“Kufuatia tamko la Rais mkoani Singida, tunamuomba waziri mwenye dhamana kuharakisha mchakato wa utafiti wa kima cha chini cha mshahara sekta binafsi na kitangazwe kwenye gazeti la serikali ili kianze kutumika sambamba na kile cha watumishi wa umma kitakachoanza Julai Mosi mwaka huu,” alisema Joachim  na kuongeza;

“Wakati wa mchakato huo baraza linamuomba waziri mwenye dhamana pamoja na bodi ya kima cha chini cha mshahara sekta binafsi ifanye maandalizi hayo kwa kuzingatia maoni ya wadau ambao ni waajiri na wafanyakazi.”

Aidha, baraza hilo limewaomba waajiri wote kuzingatia takwa la sheria la majadiliano mahali pa kazi ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi kupitia mikataba ya hali bora za kazi kwa mujibu wa kifungu cha 68 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini sura ya 366.

Katika hatua nyingine, Tpawu imekemea na kulaani vitendo vya baadhi ya waajiri ambao hutumia kima cha chini cha sekta husika kama sababu ya wao kutoongeza mishahara, jambo ambalo halikubaliki.

“Huu ni mtazamo potofu sababu unakwamisha lengo la kutungwa kwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, pamoja na Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani Na. 98 vinavyotoa haki ya majadiliano mahali pa kazi,” alisisitiza Joachim

Hata hivyo, alimsihi Rais Samia kusaidia wafanyakazi wa sekta binafsi hasa sekta ya kilimo kupata mshahara unaoweza kuwasaidia kumudu gharama za maisha ya kila siku-mathalani-ikiwa sekta ya umma watalipwa kima cha chini Tsh.500,000 basi sekta binafsi kima cha chini kabisa kisipungue Tsh.350,000 kwa mwezi.Katibu Mkuu TPAWU Taifa John Vahaye akizungumza kwenye kikao hicho.Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye kikao hicho

Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakifuatilia ajenda mbalimbali kwenye kikao hicho.Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye kikao hicho 

MITAA 58 HALMASHAURI YA MJI WA TARIME IMEFIKIWA NA UMEME-MHE KAPINGA

May 27, 2025 Add Comment


📌 *Ni kati ya mitaa 81 ya Halmashauri  ya Mji wa Tarime*


*📌  Asema kazi ya kupeleka umeme vitongojini ni endelevu*


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imefikisha  umeme kwenye mitaa 58 ya Mji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kati ya mitaa 81 ya Halmashauri hiyo.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Kembaki aliyeuliza Serikali itapeleka lini umeme katika mitaa 18 ya Halmashauri ya Mji wa Tarime. 

 

"Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina mitaa 81, kati ya hiyo mitaa 58 tayari  imefikiwa na umeme, na mitaa 23 bado haijafikiwa na umeme."  Amesema  Kapinga


Ameongeza kuwa, mitaa 13 inapelekewa umeme kupitia mradi wa Hamlets Electrification Project - IIA (HEP IIA) unaotekelezwa na Mkandarasi Dyname Construction Engineering,  na mitaa 10 iliyobaki itafikishiwa umeme katika miradi inayofuata.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake (UWT), Mhe. Zaytuni Swai aliyeuliza kuhusu jinsi  Serikali ilivyojipanga  kupeleka umeme maeneo ya pembezoni mwa mji wa Arusha hususan kwenye Kata ya Telat, Mhe. Kapinga ameeleza kuwa, Serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika maeneo ya pembezoni  (Peri Urban)  kupitia Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) ambayo lengo lake ni kusambaza  umeme maeneo ya pembezoni mwa mji.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Pareso alyeuliza kuhusu Vitongoji vya Wilaya ya Karatu kutokuwa na umeme na vichache vilivyo kwenye mradi kupelekewa nguzo 40 ambazo hazitoshelezi mahutaji na kuiomba Serikali  kuongeza idadi hiyo, Mhe. Kapinga amesema kuwa kwa kawaida miradi ya Vitongoji inawigo kulingana na kazi aliyopewa  Mkandarasi, hata hivyo amesema  kuwa Wilaya ya Karatu ipo katika mradi wa Vitongoji 9,000 ambao utaanza kutekelezwa hivi karibuni na kusisitiza kuwa, miradi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ni endelevu.

Nyongo Ashuhudia Utiaji Saini wa Makubaliano ya Ushirikiano kati ya TIC na Axcel Africa

May 26, 2025 Add Comment
Osaka- Japan 26 Mei, 2025

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, ameshuhudia tukio muhimu la utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kampuni ya Axcel Africa. 

MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO

May 26, 2025 Add Comment

Na Mwandishi Wetu, OR- TAMISEMI


Mkuu wa Kitengo Cha Mawasilino Serikali na Msemaji Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI, John Mapepele ametoa wito kwa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutanguliza uzalendo na weledi wakati wa utoaji wa taarifa ili habari hizo ziwe na tija kwa taifa.

DKT.BITEKO AWATAKA WAZAZI KUVUMILIANA KUTUNZA FAMILIA ZAO

May 24, 2025 Add Comment


📌 Asisitiza wazazi kutenga muda wa kuwa na watoto wao


📌 Asema familia imara ni msingi wa dunia imara


📌 Mashirika, Wadau wa Maendeleo waipongeza Serikali kuimarisha malezi ya watoto


📌 Zaidi ya kaya 15,000 zapata elimu ya malezi jumuishi na huduma za afya ngazi ya jamii

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa wazazi nchini kuvumiliana na kushirikiana katika malezi ya watoto wao ambao ndio msingi wa familia yeyote na Taifa kwa ujumla. 

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Mei 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia yenye Kaulimbiu inayosema “ Mtoto ni Malezi: Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara”


“ Mtoto ni zao la matokeo ya wazazi wawili, Naomba wazazi tuthamini kuwa mtoto ni mtu muhimu na anahitaji  kulelewa, jambo hili la kutolea watoto likiendelea tutakuwa na jamii isiyo na msingi imara wa familia,” amesema Dkt. Biteko.

Ameendelea kusema “ Na sisi tukumbuke kuwa tumefika hapa kwa kuwa wako wazazi walivumiliana na wakatulea katika familia, sisi tusiwe watu wa kutelekeza familia zetu, ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa familia ni msingi, tukijua kuwa kila mtu ana mapungufu hivyo tuvumiliane tulee familia zetu, ”

Dkt. Biteko amebainisha kuwa familia ikiimarika na dunia itaimarika hivyo wazazi watenge muda wa kuwa na familia zao ili kuwarithisha mila na tamaduni zao. Aidha, matokeo ya wazazi kushtakiana kwa watoto yanajenga chuki miongoni mwa watoto hata katika maisha yao ya baadaye.


Pia, ametoa rai kwa watoto kuwa watiifu kwa wazazi na walimu wao sambamba na kujifunza kwa bidii na kuishi kwa kufuata miongozo ya dini.

Katika kuadhimisha siku hiyo ya familia, Dkt. Biteko ametaja baadhi ya majukumu ya familia kuwa ni kutoa huduma ili kukidhi mahitaji ya watoto na familia, kusimamia malezi na makuzi mema ya watoto na kurithisha mila na tamaduni nzuri kwa watoto na familia kwa ujumla kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Fauka ya hayo, amesema katika kuimarisha malezi bora kwa watoto chini ya miaka 8, Serikali kwa kushirikiana na Wadau imeandaa na inatekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa kipindi cha mwaka 2021/22 – 2025/26.



Programu ambayo inahakikisha kuwa watoto wanapata huduma stahiki na jumuishi za malezi kwa uwiano ulio sawa kuanzia mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake hadi anapofikisha umri wa miaka 8.  


Ametaja mafanikio ya programu hiyo kuwa ni kuwajengea uwezo walimu wa awali 12,000 kutoka Halmashauri 184 kwa kutoa elimu ya malezi chanya ya watoto, wakihudumia zaidi ya watoto 360,000, kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo mchana 4,178, kutoa huduma za malezi na elimu ya awali kwa zaidi ya watoto 400,000. Aidha, vituo vya kijamii 206 vinavyomilikiwa na jamii yenyewe vimeanzishwa vikitoa huduma kwa watoto 11,675.

“ Katika kuimarisha huduma za kundi la watoto wa miaka 5 hadi 8, Serikali imejenga madarasa mapya ya awali 1,316 na kupatiwa vifaa vya kujifunzia. Pia, zaidi ya kaya 15,000 zimefikiwa na elimu ya malezi jumuishi na huduma za afya ngazi ya jamii wakipata huduma muhimu za afya, lishe, malezi yenye kuitikia hisia za mtoto, elimu ya awali na uchangamshi wa mtoto na ulinzi na usalama na mtoto,  amesititiza Dkt. Biteko


Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imetoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ya 15,000 wakiwemo Walezi wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo mchana, Wahudumu wa Afya, Waandishi wa Habari, na Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.


Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema kuwa Maadhimisho hayo yanalenga  kutathmini nafasi ya familia katika malezi ya watoto ambao ndio msingi wa familia yeyote na Taifa kwa ujumla. Vilevile, malezi ya mtoto yanaanza mara tu mtoto anapozaliwa na Serikali inasisitiza baba na mama kuwa karibu na mtoto wakati huo.

“ Akina mama na akina baba washirikiane  kwa pamoja kulea watoto ili wawe na  malezi bora, wapate elimu na huduma zingine muhimu kwao,” amesema Mhe. Mwanaidi.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema kupitia maadhimisho hayo wameandaa maazimio matano yanaloyenga kukuza malezi na makuzi ya mtoto ili kuimarisha familia.

Ametaja maazimio hayo kuwa ni kueneza vituo vya malezi na makuzi ya mtoto nchi nzima ili kila mtoto apate huduma jumuishi, lishe na kuwa na usalama wao pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi.


Ameendelea kusema maazio hayo ni pamoja na kuimarisha huduma za  utambuzi ili watoto wapate huduma mapema na kukuza eneo la smart malezi kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili wazazi waweze kubadilishana  mawazo kwa kutumia TEHAMA na watoto kupata nafasi ya kukua vizuri.


“ Kukuza na kuimarisha ushirikiano na taasisi za dini na mila ili kuimarisha masuala ya malezi, makuzi na taasisi  ya familia na kuongeza idadi ya watoa huduma wenye uwezo ili waweze kuenea  nchi nzima,” amemalizia Dkt. Jingu.


Akitoa salamu za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Elizabeth Maganga amesema kuwa Mashirika hayo yameendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika malezi na makuzi ya mtoto nchini.


Amesema umri wa kisayansi wa kumlea mtoto ni mwaka 0 hadi 8 na kuwa ni kipindi kizuri cha kumsaidia mtoto kukua vizuri hivyo ni fursa kwa Taifa kuwekeza katika malezi ya mtoto.


Akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Laximi Bhawan amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuweka mikakati ya kusaidia malezi ya watoto.


Aidha, pamoja na Maadhimisho hayo, Dkt. Biteko amezindua Miongozo ya Afua za Utekelezaji wa Malezi na Matunzo ya Watoto na Familia, Kutambua Mchango wa Wadau kwenye Malezi na Ustawi wa Familia na Kuzindua Kampeni ya Malezi kwa Mtoto.


Mwisho