TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO

May 01, 2025 Add Comment

 

Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali. 
Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mkoani Njombe linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura ambapo mikoa 15 imeanza zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mkoani Njombe linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura ambapo mikoa 15 imeanza zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025. 
Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali.
***************** 
Na. Mwandishi wetu, Iringa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wananchi kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara inayotekeleza mzunguko wa kwanza katika awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia na kutazama daftari la awali lilolowrekwa wazi na kutoa taarifa za wale waliokosa sifa kuwepo kwenye daftari hilo.
 
Akizungumza baada ya kutembelea vituo katika Halmashauri za Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Mji wa Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, Mwenyekiti wa TumeHuru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema wananchi wameonesha mwitikio katika siku ya kwanza ya zoezi hilo la siku saba na kuwataka kuhakiki taarifa zao.
 
Jaji Mwambegele amesema Tume imeweka wazi daftari la awali la wapiga kura katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha na kuboresha taarifa za Wapiga kura katika awamu ya kwanza, hivyo wananchi wajitokeze kuhakiki taarifa zao na kutoa taarifa za wale ambao hawastahili kuwepo katika Daftari hilo.
 
“Nawasihi wananchi endapo wataona katika Daftari ambalo tumeliweka katika kila kituo kuna mwananchi ambaye amekosa sifa kama vile kufariki basi wawe huru kwa kutumia fomu namba 5B kumuondoa huyo ambaye amekosa sifa za kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”alisema.
 
Aidha, amesema yeye pamoja na viongozi wengine wa Tume wakiwepo Wajumbe wa Tume wametembelea mikoa yote inayotekeleza zoezi hilo na kushuhudia mwitikio wa watu vituoni, huku vituo vikifunguliwa kwa wakati uliopangwa wa saa 2:00 asubuhi.
 
“Wananchi wamejitokeza vizuri kuja kuboresha taarifa zao wale ambao hawakuboresha taarifa zao katika awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,”alisema Jaji Mwambegele.
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili unafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia Mei 01, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.
 
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.
 
Mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.
 
Aidha, mzunguko wa pili utahusisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025.
 
Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 04, 2025.
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo 7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.
 
Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa  taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
 
Lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni kutoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
 
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25 Machi, 2025.







Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na baadhi ya vijana waliojitokeza kujiandikisha kwa mara ya kwanza katika moja ya vituo Mkoani Iringa.



Matukio mbalimbali ya ziara ya Mwenbyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakati akitembelea vituo mkoani Iringa 

GIZ YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 975 KATIKA HALMASHAURI ZA MKO WA TANGA

May 01, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI ya Ujerumani kupitia shirika la  ufadhili wa kimataifa nchini humo (GIZ) limetoa msaada wa  vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milion 975 vitakavyotumika katika hospitali 20 zilizopo kwenye hamashauri mbalimbali Mkoani Tanga hii ikiwa ni  utekelezaji wa programu yake ya  kusaidia na kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.

GIZ ambayo inashirikiana na  Wizara ya afya pamoja ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI)kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma  bora kwa mama na mtoto pamoja na afya ya uzazi  utekelezaji wake umeleta mabadiliko chanya  katika vituo vya afya vilivyoguswa na mpango huo ambao umeanzishwa muda mrefu.



Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameipongeza Serikali ya Ujerumani  kupitia shirika la GIZ  ambapo kupitia msaada huo unakwenda kuongeza juhudi za Serikali katika kupambana kupunguza na kuondoa kabisa vifo vya wajawazito, wakinamama pamoja na watoto wachanga waliopo chini ya miaka mitano.

Alisema lengo kubwa la Rais ni kupunguza vifo vya wakina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya miaka mitano na wameona mafanikio vifo vimepungua kwa kiasi kikubwa sana sasa wamewasaidia kupata vifaa hivyo ili kuongeza vifaa tulivyonavyo na kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaozaliwa njiti , wanaozaliwa  na manjano , wanaozaliwa na changamoto ya upumuaji , wanakuwa salama wanapongeza na kuwashukuru kwa msaada huo



Aliongeza kuwa licha ya vifaa hivyo vilivyotolewa bado kuna uhitaji kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji kupatiwa huduma mbalimbali ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba shirika la GIZ kuangalia uwezekano wa kuendelea kuwezesha upatikanaji wa wa vifaaa vingine.

" Tumekuwa na mazungumzo na tumekubaliana kwamba waongeze vifaa hivi ni kweli tumepata vingi lakini bado uhitaji ni mkubwa  tunaomba hivi vifaa vilivyopo viongezeke zaidi kutokana na idadi kubwa ya wahitaji tulionao katika vituo na hospitali zetu za halmashauri tuna imani kuwa tutaongezewa ili kuhakikisha kwamba huduma za wakina mama na watoto zinakwenda karibu zaidi na wananchi ikiwemo huduma za kibobezi" aliongeza.



Awali alizungumza Meneja wa  mradi huo hapa nchini Kai Strahler-Pohl  alipongeza juhudi za Serikali katika kuendelea kukabiliana na kupunguza  vifo vya watoto wachanga , kuboresha matokeo ya afya wakina mama na watoto, sambamaba na kuimarisha miundombinu ya vituo vya afya.

Alisema mpango huo umelenga katika  kuwezeshwa uwepo wa  vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya kuanzisha vitengo vipya vya utoaji wa huduma  za utunzaji wa watoto wachanga (NCU) katika hospitali za wilaya zote zilizopo Mkoani Tanga .



" Tunafurahi sana kuimarisha  huduma katika halmashauri zote za mkoa wa Tanga hasa kuweza kuzipatia hospital vitengo  vya utunzaji wa watoto wachanga vinavyofanya kazi kikamilifu takribani wakazi 870,000 sasa wanaweza kuwa na uhakika  kwamba Kila mtoto mchanga mvulana na msichana atatunzwa  vizuri karibu na makazi yao"

" Tunathamini ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara ya afya  , TAMISEMI, mikoa halmashauri za wilaya zote  pamoja na Serikali ya Ujerumani kukamilisha hili" alisema Meneja huyo.


Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt. Frank Shega alilishukuru shirika la GIZ kwa msaada huo ambao pia umeenda sambamaba na utoaji wa mafunzo ya utendaji wa kazi kwa baadhi ya watumishi kwa lengo la kuwaongezea maarifa na ujuzi katika utoaji wa huduma.



"Tunawashukuru na kuwapongeza sana wenzetu wa GIZ kwa  kutupatia msaada wa vifaa  hivi ambavyo vinakwenda kutusaidia kuhakikisha kuwa tunakuwa na vizazi hai na vyenye afya bora wamekuwa pia wakitoa mafunzo kwa watumishi kwaajili ya kuongeza weledi tumekuwa nao kwa muda mrefu na wamekuwa wadau wetu ambao wamwtusaidia sana" alisema Dkt Shega

Mwisho.

MACK D BONANZA &FUN RUN KURINDIMA JUNE 07,2025

May 01, 2025 Add Comment


Na Mwandishi wetu



UONGOZI wa Mac D umetangaza tarehe  ya kufanyika bonanza lake katika awamu ya pili ambapo  litaanza  asubuhi  saa 12:00  kutakuwa na mbio za  kujifurahisha 'Fun Run'  zitakazojulikana kwa jina la  'Mac D  Fun  Run 2025' .

Akizungumza na Waandishi wa Hbari leo tarehe 01 Mei 2025  kwenye Ukumbiwa EB Twenty Five uliopo Mbezi Makonde  Jijini Dar es Salaam Mratibu wa bonanza hilo Denzel Deogratius Rweyunga amesema kuwa  bonanza hilo linalofanyika kwa msimu wa pili litafanyika tarehe 07 Juni 2025 ambapo pia  mbio hizo zitaanza  katika Viwanja vya  Chuo Cha  Taifa Cha Jeshi (National  Defence  CollageNDC) Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

"Washiriki wa  mbio za KM 10 na KM5 wataanza  mbio majira ya saa moja asubuhi  kutoka Chuo Cha NDC  wataelekea  uelekeo wa  kwenda  Ununio  na  watakapofika  katika Uwanja wa mpira  unaofahamika kama Ununio  Playground  karibu na Kanisa la Roman Catholic  watageuza  hapo na kurejea katika uwanmja wa NDC.

Amesema kuwa lengo kuu la mbio hizi  kwa mwaka huu  ni kuunganisha  jamii katika  kuboresha afya na  na kuwa wakakamavu  katika kufanya mazoezi  na kulenga kutokomeza  magonjwa yasiyoambukiza  kufahamiana  na kutengeneza marafiki wapya.

"Tunawaalika watu wote  mtu mmoja mmoja, vikundi  vya wakimbiaji  na taasisi  mbalimbali  kushiriki  pamoja nasi  na baada ya kujisajili mshiriki atapata Tshirt bure na kwa yeyote anayependa kushiriki ajisajili kupitia www.macdbonanza .co.tz, vituo vingine vya usajili ni pamoja na EB Twenty Five Mbezi Makonde, Mac D Wines & Spirits Kunduchi, Zaks Bay Boko Magengeni na Leather Men Mabatini Kijitonyama Dar es Salaam.

"Msimu wa pili wa bonanza letu tutaanza na Fun Run  hizi ni mbio za kujifurahisha  na kuweka miili yetu  katika hali nzuri  ya kiafya  ambapo hakuna mshindi  wala zawadi  yeyote itakayoshindaniwa bali washiriki wote watapatiwa  fulana na namba ya kukimbia  bure  pia Kituo cha ITV kitarusha matangazo hayo mubashara" amesema Rweyunga.

Mratibu huyo ameongeza kwa kusema kuwa baada ya Fun Run  kumalizika jioni kuanzia saa 10  timu mbili ambazo ni Mac D  FC na IPP Media watashuka dimbani  na katika mchuano wa mwaka huu  mshindi ataondoka na Kombe na mechi hii itatangazwa mubashara na kituo cha Radio One.

Wakati huohuo Rweyunga ametoa shukrani kwa wadhamini wa bonanza hilo sambamba na kuwatambulisha katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

"Bonanza la mwaka huu limeandaliwa katika viwango vya juu , tunawashukuru  sana wadhamini wetu  ambao wamejitokeza kutuunga mkono ambao ni ITL, Bonite Bottlers (Kilimanjaro Drinking  Water),Bodi ya Utalii Tanzania  (TTB), Isumba Trans  Limited , Zaks Bay Liquar na Pwani Inland  Clearance and Depot (PICD).

Mwisho.

NMB Yadhamini Na Kushiriki Kilele Cha Maadhimisho Ya Mei Mosi Kitaifa Singida

May 01, 2025 Add Comment

 Na mwandishi wetu.


Benki ya NMB imedhihirisha tena nafasi yake kama Mwajiri Kinara nchini kwa kudhamini na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini, yakiwemo mashirika ya umma na binafsi, taasisi na vyama vya wafanyakazi, yakilenga kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiambatana na viongozi waandamizi wa Serikali na wageni mbalimbali waalikwa.

Ujumbe wa NMB katika maadhimisho hayo umeongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna, akiwa na baadhi ya viongozi wakuu na wafanyakazi wa benki hiyo walioungana na wenzao kuadhimisha siku hiyo muhimu.

Kupitia ushiriki wake, NMB imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika ustawi wa rasilimali watu, kuboresha mazingira ya kazi na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya ajira nchini.

Benki hiyo pia imewatakia wafanyakazi wote nchini maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.








UWEKAJI WAZI DAFTARI NA UBORESHAJI AWAMU YA PILI

May 01, 2025 Add Comment

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mkoani Njombe linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura ambapo mikoa 15 imeanza zoezi hilo litafanyika kwa siku saba kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025. (Picha na INEC).

Wananchi wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa. Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025 unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali. (Picha na INEC).