Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

BALOZI NCHIMBI AFUNGA KAZI RUVUMA

April 07, 2025 Add Comment

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amehitimisha ziara yake ya siku tano mkoani Ruvuma, akisisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa chama cha wanachama, kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote na kuwa mtetezi wa wanyonge.

Balozi Nchimbi amesema kwamba katika kuendeleza nafasi yake kama taasisi imara inayohusika na uongozi wa nchi, CCM hakina budi kuendeleza misingi ya sera zake zinazolenga kubadilisha hali za maisha ya watu, kuendana na mahitaji ya nyakati, na kuzingatia maslahi ya taifa.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanaCCM na wananchi wa mji wa Songea, waliokusanyika kumpokea alipofika kufungua mradi wa kitega uchumi wa Tawi la CCM la Mshangano mjini Songea, Jumapili tarehe 6 Aprili 2025, ikiwa ni siku ya tano tangu alipoanza ziara hiyo tarehe 2 Aprili 2025.

Katika ziara hiyo aliyoanzia katika Wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Nyasa, na hatimaye Songea mjini, Balozi Nchimbi alitoa pongezi kwa Serikali ya CCM, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, kwa jinsi inavyotafsiri kwa vitendo na ufanisi, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kupitia miradi ya maendeleo na huduma kwa wananchi.

Balozi Nchimbi alitoa maelekezo kwa Serikali kuendelea kusimamia na kubuni mipango inayolenga kuongeza matokeo chanya kwenye shughuli za uzalishaji mali, ikiwemo kilimo na madini, ili wakulima na wachimbaji madini waendelee kuzalisha kwa tija itakayoongeza pato la taifa na kuboresha maisha ya wananchi.


Aidha, Balozi Nchimbi alitembelea na kutoa maelekezo mahsusi katika miradi kadhaa ya maendeleo na ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kupitia wizara na taasisi zake, ikiwemo mradi wa uzalishaji mbegu chini ya Mamlaka ya Mbegu Nchini (ASA) na ujenzi wa Bandari ya Nyasa, kwa lengo la kuendelea kutafsiri utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.


Katika mikutano ya hadhara katika wilaya mbalimbali, pamoja na kusalimia wananchi katika maeneo ya Songea Vijijini, Mbinga na Songea mjini, Balozi Nchimbi alipokea taarifa za utendaji wa kazi kutoka kwa viongozi wa Chama na Serikali, na pia alipokea maoni ya wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili, kupitia kwa wabunge na wananchi moja kwa moja, kisha kutoa maelekezo ya kutatuliwa kwa kero hizo.


Balozi Nchimbi, ambaye amehitimisha rasmi ziara yake kwa kuondoka mkoani humo Jumatatu tarehe 7 Aprili 2025, alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wanaCCM na Watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano wao na Serikali ya CCM katika kulinda tunu za taifa, ikiwemo amani na utulivu. Alitoa wito wa kuendeleza hali hiyo wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


#Ends

DKT.SAMIA AMETENDA MAAJABU SEKTA YA NISHATI MIAKA MINNE YA UONGOZI -DKT.BITEKO

March 24, 2025 Add Comment


📌 Mashine ya 9 yakabidhiwa, yakamilisha MW 2115 - JNHPP


📌 Aitaka Jumuiya ya Wazazi ieleze Watanzania mafanikio ya Serikali


📌 Asema kuongezeka kwa mahitaji ya umeme nchini kunachochea ukuaji wa viwanda


📌 Atoa wito kwa Watanzania kuzingatia matumizi bora ya umeme


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan sekta ya nishati imepiga hatua kubwa nchini sambamba na kuzalisha umeme wa ziada dhidi ya mahitaji ya Watanzania.

Dkt. Biteko amesema hayo Machi 23, 2025 jijini Arusha wakati akitoa takwimu kuhusu  ongezeko la mahitaji  ya umeme nchini katika Kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa.


“ Rais Samia amefanya kazi kubwa katika sekta ya nishati nchini na hivi karibuni, tulikuwa nchini Barbados kueleza  mafanikio yetu katika sekta hii kwa kuwa Rais Samia amefanya jitihada kubwa sana katika ya nishati,” amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza “Ili uchumi wa nchi yoyote duniani upatikane lazima kuwe na sekta ya nishati. Aidha, katika sekta ya nishati ili viwanda viweze kuendelea umeme unaohitajika ni asilimia 40 na katika sekta ya madini umeme unaohitajika ni asilimia 30,” 


Dkt. Biteko amesema mwaka 2017 hadi 2018 mahitaji ya juu ya umeme nchini yalikuwa megawati 1045, mwaka 2018 hadi 2019 mahitaji ya juu ya umeme yalikuwa megawati 1,116 mwaka 2021 hadi 2022 megawati 1,340.7.

“ Mwaka 2022 hadi 2023 mahitaji ya juu yaliyoongezeka na kufikia  megawati 1,470 na mwaka 2024 hadi kufikia sasa mwaka 2025 ni megawati 1,908 ikiwa ni sawa na megawati 262, ongezeko la mahitaji ya namna hii haliwezi kutokea kama hakuna uwekezaji katika sekta ya nishati,” amesema Dkt. Biteko.


Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Mashine ya tisa ya mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Julius Nyerere Machi 22, 2025 imekabidhiwa na kuunganishwa kwenye Grid ya Taifa. Amesisitiza kuwa kutokana na ongezeko hilo la megawati za umeme Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere pekee linaweza kutosheleza mahitaji ya nchi licha ya kumalizika kwa muda uzalishaji wa umeme kwa kutumia mitambo ya Songas.

 “Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sekta ya nishati imefanya kazi kubwa, Rais Samia ametenda maajabu katika sekta hii na ameweza kuvutia wawekezaji wengi sana kuja kuwekeza nchini,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, amesema kuwa Jumuiya ya Wazazi nchini ina wajibu wa malezi na mazingira na kuwa nishati safi ni eneo mojawapo hivyo Wizara ya Nishati ina wajibu wa kushirikiana  na wadau mbalimbali ikiwemo Jumuiya hiyo, sambamba na kushirikiana nayo katika kampeni zake za kupeleka ujumbe kwa jamii.

Pamoja na hayo, Dkt. Biteko amewaasa Watanzania kuzingatia matumizi bora ya umeme kwa kuacha mazoea yanayosababisha upotevu wa umeme ikiwemo kuwashaa taa bila kuwa na matumizi nazo.


Ametolea mfano kuhusu matumizi mabaya ya umeme kupitia utafiti uliofanywa na Wakala wa Nishati wa Kimataifa (International Energy Agency) ambapo asilimia 30 ya umeme unapotea kutokana na mazoea.


Katika hatua nyingine, taasisi mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) zimewasilisha mada mbalimbali katika semina hiyo.


Pia, Wizara ya Nishati kupitia taasisi zake za TPDC, REA na TANESCO zimetoa semina kwa wajumbe wa kikao hicho kuhusu Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 hadi 2034, Matumizi Sahihi ya Nishati Safi ya Umeme.


Ambapo, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia, kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Ngeleja Mugejwa ameeleza faida mbalimbali za matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan kwa watoto wa kike ambapo  kupitia matumizi ya nishati hiyo itawasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea kuliko kuandaa na kupika chakula.

SHAMIRA AKABIDHI SHILINGI MILIONI 1 UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU KASKAZINI UNGUJA

March 24, 2025 Add Comment

Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Viti vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama @shamiramshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana CCM na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.

Shamira alitembelea ofisi ya UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar kufanya kikao kifupi cha ndani, na kukabidhi shilingi milioni moja kwa kamati ya Utekelezaji na viongozi wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyopokelewa na Katibu wa UVCCM Mkoa huo Comrade Rished Khalfan pamoja na wajumbe wengine ngazi ya mkoa na Wilaya.


Shamira amewasisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.

“Ujenzi wa Chama ni jukumu letu sote”.




DOYO HASSAN DOYO AMETANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

March 15, 2025 Add Comment






Na Oscar Assenga,MOROGORO

Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao. Doyo alifanya tangazo hilo mbele ya waandishi wa habari jana mkoani Morogoro, na kusema kuwa kwa heshima kubwa anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia kuwa na afya njema.

Akizungumza kwa hisia, Doyo aliwashukuru Watanzania kwa mwitikio wao wa kuendelea kukuza demokrasia nchini, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kupata haki ya kuchagua au kuchaguliwa. “Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, ambapo kila Mtanzania mwenye sifa anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa,” alisema.



Doyo aliongeza kuwa, yeye mwenyewe ana sifa zote zinazohitajika kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza kuwa amevuka umri wa miaka 45, umri wa kikatiba wa kugombea urais, na kwamba ana afya ya kuhimili majukumu makubwa ya urais.

Akizungumzia umuhimu wa uchaguzi mkuu ujao, Doyo alisisitiza kuwa huu utakuwa uchaguzi wa sita tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, na kwamba ni muhimu kwa maendeleo ya taifa. “Kama Mtanzania mwenye haki ya kikatiba, nimemudu kujitathmini kifikra, kiuwezo, na kiuweledi, na kujiridhisha kuwa nina uwezo wa kumudu nafasi hii,” alisema Doyo.

Doyo alifafanua kuwa uamuzi wake wa kugombea urais haujaanza kwa mkupuo, bali ni baada ya kupata busara kutoka kwa wazee na familia yake, ambao walimshauri kuendelea mbele kwa faida ya taifa. “Si busara kuwataja hapa, lakini wanajua na wanasikia wakiwa pale walipo,” alieleza.

Doyo aligusia masuala muhimu ambayo bado hayajapata kipaumbele kikubwa katika taifa letu, na ambayo ataenda kuyashughulikia iwapo atachaguliwa kuwa Rais. Masuala hayo ni pamoja na: ajira, elimu, kilimo na ufugaji, rasilimali za maji, kupambana na ukwepaji wa kodi, na kupambana na rushwa. Aliongeza kuwa ataweka nguvu katika kuimarisha sekta ya madini, kuimarisha muungano, na kuendeleza jitihada za watoto wa kike katika elimu na teknolojia.

“Kwa hiyo, nimeona ni muhimu kutoa mchango wangu kwa taifa letu ili kuleta faraja kwa Watanzania. Hivyo, leo hapa mbele yenu, mimi Doyo Hassan Doyo, mwanachama wa Chama cha National League for Democracy (NLD), natangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu cha NLD. Dhamira yangu ni kubeba dhana ya Uzalendo, haki, na maendeleo kwa vitendo ili tuwakomboe Watanzania,” alisisitiza Doyo.

NLD: Ukombozi wa

NLD: Mtetezi wa Umma.

NLD: Moto Moto Motooo!