Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

CCM :TUTASHUGHULIKA NA MATATIZO YA WATU

December 04, 2024 Add Comment

 



Na Mwandishi Maalum , Zanzibar 


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitaacha kushughulika na changamoto  zinazowakabilii wananchi kwakuwa  hiyo ni moja ya shabaha  ya kuanzishwa CCM  mwaka 1977.


Kimesisitiza kazi ya kupigania haki  za wananchi, uhuru,kuenzi thamani ya utu na heshima ya kila binadamu, majukumu hayo yalianza kutekelezwa na vyama vya TANU na ASP. 


Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya Nec Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto  Khamis, wakati  akijibu swali la sababu ipi inayowafanya watanzania kuendelea kuichagua CCM .


Mbeto  akijibu swali hilo, alisema watanzania wataendelea kuiamini CCM  kutokana na kusimamia  malengo  ya kuanzishwa kwake,  sera na siasa yake pia  ni chama kinachoshughilika na matatizo ya wananchi



Alisema CCM haitaacha wala kupuuzia kutafuta majibu  yoyote ya matatizo   yanayowakabili wananchi katika kila Mtaa, Kkijiji, Kitongoji, Wadi/Kata,Wilaya  hadi Mkoa .


"Chama kinachopigania maslahi  ya umma hakiwezi kunyimwa kura au  kutoaminiwa. Kitaendelea kushinda kwakuwa watanzania  wanaiamini na kuitegemea CCM kwa  kutumikia  kwake wananchi "Alisema mbeto 


Aidha alisema chama kinachohangaikia  shida na  matatizo ya watu , kinachotafuta majibu ya  matatizo  na kuwafikia wananchi  ,kuwasikiliza na kutoa ufumbuzi, lazima kiaminiwe na kushinda .


'Nadhani upinzani  ubadilishe  mtindo  wa siasa zake ili ukubalike katika jamii. Kubeza au kupondoka  kila jema la CCM  si mtaji utakaoufanya upinzami uungwe mkono. Kwa mtindo huo itawachukua miaka mia moja  ijayo hadi uaminike" Alieleza 


Pia alivishauri vyama hivyo  kuungana na kuunda chama kimoja kitakachokuwa na nguvu  za ushindani kwa CCM, kwani kadri unavyooendelea kubaki na utitiri wa vyama, hautakishanda chama tawala.


"kazi ya kushughulika na mataizo ya wananchi  hicho ni kiapo kwetu. Ni jukumu la kufa na kupona .Kinachotuumiza kichwa  CCM usiku na mchana ni kupata maendeleo ya nchi na watu"Alieleza Mbeto

VYAMA VYA SIASA WILAYA YA TANGA VYAPONGEZA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

November 30, 2024 Add Comment

Na Oscar Assenga,TANGA

Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 27 mwaka huu katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, vimetoa tamko la pamoja na kupongeza mchakato wa Uchaguzi huo huku vikitaka dosari chache zinazotakiwa zifanyiwe kazi na Tamisemi.

Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM),Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,vyama vyengine ni (ACT-Wazalendo) CUF, ADC,TLP na NCCR-Mageuzi.


Vyama hivyo vimetoa tamko la pamoja leo Novemba 29 mara baada ya matokeo ya jumla kutangazwa hapo Novemba 28 mwaka huu ambapo CCM katika Jiji la Tanga kimeibuka kidedea kwa kushinda viti vyote vya kuanzia wajumbe na wenyeviti wa mitaa yote.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa tamko la pamoja,Mussa Mbarouk ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Tanga alisema kwamba uchaguzi ulifanyika kwa njia ya amani japo kulikuwa na dosari ndogondogo ambazo wanaamini zitafanyiwe kazi,

"Mchakato wa Uchaguzi huu ulienda vizuri, tulikuwa tukishirikiana na Serikali ya Mkoa na Jiji, kulikuwa na dosari ndogondogo lakini hata sisi vyama vya siasa tunatakiwa tukae na tuungane ili yale maeneo yote yenye Wagombea wanaokubalika tumuunge mkono" Alisema Mbarouk


Mbarouk alisema kwamba chama chake pamoja na vyama vyote shiriki katika Uchaguzi huo vimesikitishwa na matokeo ya jumla ambapo hakuna chama cha upinzani kilichoshinda kiti hata kimoja.

" Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2019 tulipata walau viti 61,lakini safari hii haijawahi kutokea kiukweli ni lazima tujipange vizuri Uchaguzi Mkuu Ujao mwaka 2025" Alisisitiza Mbarouk

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Chadema Hemed Bakari alisema kuna umuhimu mkubwa kwa vyama vya siasa kuongeza nguvu ya ushawishi kwa wapiga kura,

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tang Shaban Kalaghe alisema mchakato wa Uchaguzi huo ulienda vizuri na kuwashukuru watu wote waliojiandikisha na kupiga kura,

“Kwa kweli niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi huu ulienda vizuri tulikuwa na wagombea kwenye mitaa yote na tumeshinda kwa asilimia 100 lakini pia tunawashukuru wenzetu wa vyama vingine kwakukubali matokeo ni jambo zuri na linaonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba uchaguzi huu umeisha na sasa wanakwenda kufanya kazi lakini pia kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025


CCM YATAJA SIRI USHINDI SERIKALI ZA MITAA, YAWAPELEKA UJUMBE UPINZANI

November 29, 2024 Add Comment

 Na Said Mwishehe


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetoa sababu nne ambazo zimefanya Watanzania kuendelea kukiamini na kuchagua wagombea wa Chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na miongoni mwasababu ambazo zimefanya washindi ni uwepo wa migogoro katika vyama vya ipi upinzani.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla amesema wamekuwa katika kampeni kwa siku saba kuanzia Novemba 20 mpaka Novemba 26 na Novemba 27 uchaguzi umefanyika na kupiga kura.

“Ahadi yetu wakati wa kampeni ni kwamba CCM imeongozwa na 4R za Rais Samia Samia Suluhu Hassan za uvumilivu, ustahimili, kuheshimiana lakini pia kuhakikisha tunaendelea kujenga nchi yetu.CCM imeonesha kuheshimu kwa kufanya kampeni za kistaarab, kuheshimu ratiba wakati wa kampeni,”amesema.

Akitaja sababu za Chama hicho kushinda katika uchaguzi huo wa Serikali wa Serikali za mitaa ni kwamba wanaamini wamepewa imani hiyo ambayo wamepewa CCM imetokana na sababu mbalimbali na sababu ya kwanza wananchi wameridhika na utekelezaji mzuri wa Ilani ,miradi ya maendeleo, utatuzi wa kero mbalimbali.

“Hii imejenga imani kwa Watanzania kukiamini Chama Cha Mapinduzi lakini kikubwa miradi mbalimbali inayotekelezwa iko katika mitaa,Vitongoji,vijiji, kwa hiyo tunaamini mafanikio yaliyopatikana yalijenga imani kwa wananachi.”

CPA Makalla amesema sababu ya pili ni maandalizi ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwa walijua kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa , hivyo walifanya na maandalizi ya kutosha kwa kuanza kwa kufanya tathimini ya viongozi waliopo katika mitaa , vijiji na vitongoji.

“Kwahiyo kila eneo kila wilaya tuliwafanyia tathimini viongozi walioko madarakani lakini na kutambua changamoto na maoni ya wananchi.CCM haikukosea kuteua wagombea safi ambao wabakubalika na hiyo imekuwa siri ya ushindi lakini nyie ni mashuhuda kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka ngazi ya Mashina uchaguzi huu tuliuchukulia kwa uzito mkubwa , hivyo maandalizi ya kuandaa wananchi yalikuwa makubwa na tunaamini tulikuwa na maandalizi mazuri.”

CPA Makalla amesema hatarajii mtu akaja akahoji CCM imeshindaje kwani Watanzania ni mashuhuda vyama vingine havikuwa na maandalizi,vyama vingine havijaonekana kwa wananchi miezi Saba ,wengine wamewekeza katika maandamano .

“Unafanya maandalizi kwa siku tatu unatarajia unaweza kushinda? CCM imefanya maandalizi ya kutosha kupitia viongozi wake.Changamoto ambayo wapinzani wameipata ni kutokana na kutakuwa na maandalizi ya uchaguzi.Tusitafute sababu yoyote.Sababu hakukuwa na maandalizi.”

Pia amesema sababu ya Tatu CCM imefanya kampeni zake kisayansi kuanzia uzinduzi ,kufunga kampeni pamoja uratibu na ushirikishwaji kwa viongozi wa Chama kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya shina.

Sababu ya nne iliyowafanya CCM kushinda,CPA Makalla amesema imechangiwa vizuri na migogoro ya vyama vya siasa na kuelez adui yako muombee njaa.Kwahiyo katika vyama vya siasa migogoro imefanya CCM kushinda ingawa kuna sababu nyingine nyingi.

Ametumia nafasi hiyo kuvitaka vyama vya upinzani kuendelea kuvumiliana na kujiepusha na migogoro kwani Chama chenye Mgogoro ni ngumu kushinda katika uchaguzi akitolea mfano CHADEMA ambayo kwa sasa kuna Mgogoro mkubwa na wameshuhudia Arusha wanachama wakivurugana na kupigana wakati wakielekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

“Najua vyama vya upinzani leo vinaongea lakini watakachoweza ni kutoa propaganda tu kwa kuituhumu TAMISEMI na CCM lakini ukweli wameshindwa uchaguzi kwasababu ya kutakuwa na maandalizi na migogoro kwa viongozi wao.Mengine yote watakayosema hayana ukweli.”


DC SUMAYE AONGOZA WANANCHI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

November 27, 2024 Add Comment

 

 

Na Ashrack Miraji 

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Zephaniel Sumaye, leo tarehe 27 ameongoza wananchi katika zoezi la kupiga kura la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo wanachagua viongozi wa Serikali ya Mtaa, kitongoji na vijiji katika kituo cha Chake Chake, kilichopo wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

Akizungumza baada ya kupiga kura, Mhe. Sumaye aliwashukuru wananchi wa wilaya ya Lushoto kwa ukomavu wao wa kisiasa na kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, akieleza kuwa ni ishara ya maendeleo katika demokrasia. Aliwataka wananchi kuendelea kushiriki kwa wingi ili kuchagua viongozi wanaowataka, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linatakiwa kuwa la amani na utulivu.

“Tunashuhudia ukomavu mkubwa wa kisiasa kutoka kwa wananchi wa wilaya ya Lushoto. Kampeni zilifanyika kwa amani na hakuna malalamiko kutoka kwa vyama au wagombea,” alisema Mhe. Sumaye. “Ninawaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaowaongoza katika maendeleo ya jamii yetu.”

Mhe. Sumaye pia aliwasisitizia vyama vya siasa na wanachama wao kuheshimu kanuni za uchaguzi, akieleza kuwa malalamiko yoyote kuhusu uchaguzi yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Mhe. Sumaye aliwataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wakati wa uchaguzi, akiwataka waendelee na shughuli zao  baada ya kupiga kura, ili kuepuka msongamano na usumbufu. na Alisisitiza kuwa hii ni siku ya mapumziko iliyotengwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.

Kwa upande mwingine, Dkt. Ikupa Mwaysoge, Msimamizi  wa Uchaguzi wilaya ya Lushoto, alisema vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza hadi sasa. Alisema wananchi wamejitokeza kwa wingi na hali ni shwari katika maeneo yote ya uchaguzi.

“Tunawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi. Hii ni fursa muhimu ya kutimiza wajibu wa kikatiba, kuchagua viongozi bora watakaoweza kuleta maendeleo kwa jamii,” alisema Dkt. Mwaysoge.

Linoss Mwita, mkazi wa Lushoto, ambaye ni kijana, alisema kuwa aliona ni muhimu kushiriki katika uchaguzi huu, kwani ni haki yake ya kikatiba. Alisema kuwa ili kupata viongozi bora, ni lazima wananchi wawe na ushiriki mkubwa katika mchakato wa uchaguzi.

“Leo ni siku ya kupumzika, kama alivyosema Rais wetu, hivyo tunatumia siku hii kutekeleza wajibu wetu wa kikatiba. Napenda kuwahimiza vijana wengine kujitokeza kwa wingi ili kuchagua viongozi bora,” alisema Mwita.

Kauli mbiu ya uchaguzi wa mwaka huu ni: “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.”




 

TAYARI NIMEPIGA KURA,WEWE JE?

November 27, 2024 Add Comment




Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato leo Tarehe 27 Novemba 2024 amepiga kura kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha Chuo Huria Mtaa wa Migera - Nshambya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.