Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

TFS WATUMIA MICHEZO KUHAMASISHA JAMII KUHIFADHI MISITU

November 03, 2024 Add Comment

 


  


Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Nchini (TFS) wameeandaa bonanza la michezo lenye lengo la kujenga mahusiano, ushirikiano na kuhamasisha jamii katika uhifadhi wa misitu ambalo limewakutanisha washiriki zaidi ya mia mbili (250) kutoka katika kanda nane za Uhifadhi nchini.

Akizungumza wakati akizindua bonanza hilo Jijini Arusha KamshinaMsaidizi Mwandamizi wa TFS CPA (T) Peter Mwakosya akimwakilisha kamishna wa Uhifadhi wa misitu nchini amesema washiriki wametoka katika kanda zote nane na wanashiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mikono pamoja na riadha.

"Nipende kuelekeza katika kila kanda kutenga bajeti ambazo zitaweza kuwezesha shughuli za michezo kwa askari wetu wa uhifadhi ikiwa ni njia pekee ya kuendelea kuimarisha afya kwa askari wetu" Aliongezea

Kwa upande wake Mratibu wa bonanza hilo Afisa Muhifadhi Mwandamizi kutoka TFS Marcel Bitulo ameeleza kuwa bonanza hilo litatumika katika kuandaatimu ambayo itawawakilisha kwenye mashindano ya SHIMUTA yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi novemba mkoani Tanga.

Ramia Konyo ni mmoja ya wawakilishi wa baadhi ya kanda ambapo amepongeza hatua hiyo na kudai ina tija kubwa katika kuongeza ufanisi katika utendaji kati wao ambao utaongeza umoja na ushirikiano wa watumishi sambamba na kujenga afya zao mahala pa kazi.

Hata hivyo Meneja Uhusiano kutoka TFS  Johari Kachwamba ameeleza kuwa mashindano hayo yanalengo la kujenga mahusiano mazuri kwa wafanyakazi wa TFS kutoka katika kanda zote za Tanzania na kuhamasisha watumishi hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi.

Mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza kwa kushirikisha kanda zote nane ambazo ni shamba la miti SAOHIL,nyanda za juu kusini,kanda ya mashariki,kanda ya kati,kanda ya kaskazini,kanda ya ziwa pamoja na kanda ya magharibi. 


DKT.MPANGO KUFUNGUA MICHEZO YA SHIMMUTA 2024 JIJINI TANGA

November 03, 2024 Add Comment

Na Andrew Charle
 
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) Novemba 16, 2024 jijini Tanga.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Shirikisho hilo, Dkt.Maswet Masinda wakati wa zoezi la kupanga droo ya makundi ya timu zitakazokutana katika michezo zaidi ya 12 ambayo itashindaniwa na timu zaidi ya 91 zilizojitokeza mwaka huu.

"Maandalizi yote yamekamilika na tayari mlezi wetu ambaye ni Makamu wa Rais Dkt. Mpango anatarajiwa kufungua rasmi Novemba 16, 2024. Uwanja wa ufunguzi tutautangaza rasmi hapo baadae.

Kwa sasa timu zote zipo hapa kushuhudia droo ya wazi kabisa kuona timu zao zitakuwa kwenye kundi lipi tayari kwa michezo rasmi itakayoanza Novemba 10 hadi 24, Jijini Tanga."Amesema Dkt. Masinda

Aidha, Dkt. Masinda ametoa wito kwa timu zote 91 kufika Jijini Tanga Novemba 8, ambapo Novemba 9 watakuwa na kikao cha pamoja kisha michezo kuanza kutimua vumbi Novemba 10.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIMMUTA Taifa, Roselyne Massam amesema mwaka huu Shirikisho hilo limevunja rekodi kwa kupata timu nyingi zilizojitokeza hali ambayo inaleta mwamko na hamasa katika kuimarisha afya kwenye michezo pamoja na kuleta umoja hapa nchini kupitia michezo hiyo.

Amesema rekodi hiyo inatokana na kuongezeka kwa idadi ya timu na sasa kufiki 91 zitakazochuana katika kuwasaka mabingwa kupitia michezo watakayoshindaniwa.

Aidha, katika zoezi hilo wamejipanga hakuna mamluki atakaye chezeshwa kwenye timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwani watahakikisha wanasimamia sheria, kanuni na taratibu zinazowaongoza katika michezo yote.

Michezo hiyo 12 itakayochezwa katika mashindano hayo ni pamoja na michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa pete, wavu, kikapu, dats, pool table, vishale, drafti, kukimbia kwa magunia, riadha, kuvuta kamba, bao na mingineyo, lengo kuu likiwa kuimarisha uhusiano na kuimarisha afya za wafanyakazi kupitia michezo.


TPDC MDHAMINI MKUU MBIO ZA MWL NYERERE MARATHON MWANZA

October 12, 2024 Add Comment

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekuwa Mdhamini Mkuu wa Mbio za Mwl. Nyerere Marathon zilizofanyika leo Jumamosi Oktoba 12, 2024 Igoma Mkoani Mwanza. Mbio hizo zimefanyika zikiwa na lengo la kuenzi falsafa ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Maendeleo na Ustawi wa Taifa letu.

Akiongea katika hafla hiyo Bw. Donald Aponde ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC ameeleza kuwa: -

"TPDC tunajivunia kudhamini mbio hizi kwani Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifanya mambo mengi ikiwemo kuanzishwa Kwa TPDC (1969) ambapo hadi sasa Shirika letu linafanya vizuri kwenye shuguli za utafutaji na uendelezaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia nchini.




BMT YAWAFUNDA VIONGOZI WA SHIMUTA

October 05, 2024 Add Comment

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha akizungumza wakati akifunga mafunzo ya  ya Saikolojia na Uongozi Michezoni Jijini Tanga 
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shimuta na Mwenyekiti wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Elinaike Nabur
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo  Mwenyekiti wa Michezo kutoka TFS na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Shimuta Marcel Bitulo 


Na Oscar Assenga, TANGA.

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha amelitaka Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) kutengeneza kanuni na miongozi mizuri ili kuondoa migogoro wakati wa Mashindano ikiwemo kuachana, Mamluki na makandokando ya kubadilisha ratiba mara kwa mara.

Neema aliyasema hayo Jijini Tanga wakati akifunga mafunzo ya Saikolojia na Uongozi Michezoni Jijini Tanga ambapo alisema hawatarajii kuona mambo kama hayo yanajitokeza kwenye mashindano hayo badala yake muhimu wakazingatia kanuni na miongozo.

Alisema pia uwepo wa kanuni na miongozo imara itasaidia kuwaepusha na mitafaruku ambayo haina tija wakati wa mashindano na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea

“Hatutarajii kukutana na mambo hayo tuzingatie kanuni na miongozi tuliojiwekea na matarajio yetu ni kuona Shimuta inakuwa na matarajio makubwa ya kuacha alama kwenye mashindano hatuwezi kupeleka malalamikio hayo mbele ya kwa viongozi”Alisema

Katibu huyo alisema kwamba wanatarajia kuona shirikisho hilo kinakuwa na mipango mikubwa ikiwemo kuona namna ya kununua eneo Tanga kwa ajili ya kujenga kituo cha Mashindano wakiwa kazini watoto watacheza pale.

“Lakini pia tunatarajia kuona kama Shimuta mwaka ujao tunachanisha watu fedha zitakazoptikana tutanunua mipira na kupeleka kwenye shule 56 za michezo zilizoteuliwa na Serikali na mambo mengine ya kimaendeleo na sio suala la mamluki”Alisema

Hata hivyo aliwataka watumishi kuwa na mahusiano mazuri na waajiri vizuri katika kutetea suala la Shimuta na wasiende kugeuka kuwa kero kwao.

“Niwapongeza viongozi wa shimuta kwa kuweza kubuni na kufanya vitu ambavyo vitasaidia kuleta maendeleo kwenye michezo yao mahali pa kazi tunafahamu kwamba nini katiba yenu inaeleza majukumu yenu tunapaswa kuyafanya”Alisema

Alisema lakini mashirikisho mengi wamekuwa wakijipanga kwa kufikiria mashindano na ndio maana kwenye kufanya mashindano mambo mengi hayaendi sawa kutokana na kwamba kuna masuala wanakuwa hawajapata uelewa nayo ndio maana mkagundua ipo haja ya kufa ya mafunzo hayo.

Alitoa wito kwa washiriki mafunzo hyo kuzingatia walichofundishwea ili wanapokwenda kwenye kazi waweze kuongeza thamani ya uwepo wao kwenye mafunzo hayo huku akieleza kwamba kila mtu anaweza kucheza na sio kusimamia michezo.

“Mafunzo mliyoyapa hapa yakawe chachu na mjitofautishe na wale ambao hawajahudhuria lakini uhai wa binadamu upo kwenye michezo na ndio maana wanawake ukienda hospitalini ukiwa mjamzito unaulizwa mtoto amecheza tumboni michezo ndio kiini cha uhai wa binadamu “Alisema

Aliongeza kwamba sasa kiini hicho watu wanakichukulia rahisi kwamba kila mtu anaweza kuisimamia bila kutambua kwamba ili uweze kusimamia lazima upewa mafunzo kwani michezo ni utaalamu kama ilivyo utaalamu mwengine wowote

“Naomba tukazingitie mafunzo tulioyapata Mahali pa kazi ni kituo kilicholetwa kama ziara kusaidiaa watumishi afya, kutengeneza connection na tuzingatie yale tuliofundishwa tuzingatia maadili ya kazi tunapokuwa kwenye sehemu ya michez ili kutowapa sababu ya watu wanaopiga vita michezo kupata vya kuongea”Alisema

“Lakini wakati wa mashindano Shimuta tumekuwa tukipokea malalamiko mengi kwamba mara ratiba,mamluki,wakijua dhumuni la kuanzishwa Shimuta hawataleta mamluki,kwanini tunawabania watumishi wenzetu na kuwaleta watu ambao sio watumishi na kusababisha uvunjifu wa tabia hivyo nataka tuachana na hilo”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Shimuta Roselyn Masambu alisema lengo la mafunzo hayo ni muhimu kwa viongozi wa michezo ambao wanaongoza wafanyakazi katika taasisi zao na hivyo wanaamini yatakuwa chachu kubwa kwa maandalizi ya michuano hiyo msimu huu lakini pia kuwa chachu katika michezo kwenye maeneo yao .

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Michezo kutoka TFS na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Shimuta Marcel Bitulo alisema kwamba kwa kutambua sera ya nchi ambayo inataka kila taasisi kutenga bejeti ya michezo kama unavyotambua ili uweze kuwa na tija kwa wafanyakazi lazima utoa kipaumbela suala la michezo na wao wanatambua na wamekuwa wakilifanya mara kwa mara.

Hata hivyo kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shimuta na Mwenyekiti wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Elinaike Nabur
alisema michezo ni sehemu muhimu kwa watumishi ambao muda mwingi wanatumia mahali pa kazi kuhakikisha wanasaidia serikali kufikia jamii kutimiza malengo yao iliyokusudia katika nchi.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA VNA WACHEZAJI WA SIMBA NA VIONGOZI WAO IKULU ZANZIBAR

September 25, 2024 Add Comment

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhia Jezi ya Timu ya Simba na Nahodha wa Timu hiyo Mohammed Hussein, baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024.



WACHEZAJI wa Timu ya Simba na Viongozi wao wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wachezaji hao katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 25-9-2024, kwa ajili ya mazungumzo na kumsalimia, wakiwa Zanzibar kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Timu ya Azam utakaofanyika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar 26-9-2024.(Picha na Ikulu)