Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts
RAIS MWINYI ARIDHIA UWANJA WA AMAAN KUITWA “NEW AMAAN SPORTS COMPLEX”

RAIS MWINYI ARIDHIA UWANJA WA AMAAN KUITWA “NEW AMAAN SPORTS COMPLEX”

December 28, 2023 Add Comment




Na, Brown Jonas – WUSM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina uwanja wa Amaan na kuitwa “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya Uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 20203 kisiwani humo

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya Kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium” alisema Dkt. Ndumbaro.
- Advertisement -

Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na Burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” na Timu ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar “Zanzibar Heros ambazo zilitoka sare ya bila kufungana.

BANDARI QUEENS BINGWA NETIBOLI DARAJA LA PILI, MENEJIMENTI YA TPA YAPONGEZWA

November 06, 2023 Add Comment

 Timu ya Netiboli ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA “ Bandari Queens” imetwaa Ubingwa wa Mashindano ya ligi Daraja la pili Taifa baada ya kupata ushindi wa magoli 38 kwa 31 dhidi ya Mapinduzi Dodoma Katika mchezo wa tamati uliochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Nsimbo, Mpanda Mkoani Rukwa.


Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph amekabidhi kombe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi









WAZIRI NAPE AIONGOZA TTCL KUZINDUA HUDUMA YA WI-FI BENJAMIN MKAPA

November 06, 2023 Add Comment

 


Na Mwandishi wetu Dar es salaam

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kutaka uwanja wa Benjamin Mkapa uwekewe huduma ya Mtandao yaani Inteneti ikiwa ni sehemu ya ukarabati katika uwanja huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya Mtandao katika uwanja huo leo Novemba 5,2023 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye amesema kutekelezwa kwa agizo hilo la Dkt.Samia linakwenda kuwasaidia mashabiki wote wanaoingia kutazama mpira kufurahia kwa kutumia mtandao wenye kasi zaidi.


“Leo tunaanza kuzindua huduma hii ya mtandao wenye kasi katika Uwanja huu wa Mkapa na kwa maagizo ya Rais Samia ni kwamba viwanja vyote vipate huduma ya mtandao ili wanaohudhuria viwanjani wafurahie Mtandao,” amesema Nape

Katika hatua nyingine Mhe.Nape amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya Mkurugenzi wake Mhandisi Peter Ulanga kwa kufanikisha uwekaji wa huduma hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Pigeni makofi ya kutosha kwa TTCL kwa kufanikisha hili la kuweka huduma hii ktaika uwanja huu na naamini kiwanja hiki ni ch kwanza na viwanja vingine vitafuata sasa mnawafanya mashabiki wafurahie kuja uwanjani kwa sababu wanafurahia huduma ya mtandao ambao nimefanyia majaribio na una kasi kwelikweli,”amesema Nape

Nape ameipongeza Azam Media Kwa kuendelea kurusha Matangazo ya mpira Kwa ubora Huku akiamini kuwa uwepo wa Mtandao WA uhakika kutoka TTCL itaendelea kunogesha Matangazo yao.

Hafla hiyo pia imeshuhudiwa na Naibu Waziri Mhe. hamis Mwinjuma, Katibu mkuu Bw. Gerson Msigwa Naibu katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa Mkurugenzi mkuu wa TTCL Mhandisi Peter ulanga mashabiki pamoja na wapendasoka waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga.

PILSNER LAGER SASA NI MDHAMINI MKUU WA SIMBA SC

November 01, 2023 Add Comment


"Kampuni inayoongoza ya kuzalisha bia, Serengeti Breweries Limited (SBL), imesaini makubaliano ya miaka mitatu kudhamini Klabu ya Michezo ya Simba ambapo klabu hiyo itapokea ufadhili wa shilingi bilioni 1.5 kutoka kwa kampuni kupitia bia yake - Pilsner Lager.


Awali ilikuwa mdhamini mkuu wa Taifa Stars hadi katikati ya mwaka huu na sasa ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Taifa ya Tanzania kupitia bia yake nyingine, Serengeti Premium Lite. Ahadi ya SBL ya kusaidia soka nchini Tanzania inaendelea kukua kwa kasi.

"Wakati fursa ya kudhamini Simba SC ilijitokeza, tulihisi wajibu na fahari kubwa katika kutoa msaada wetu kwa moja ya vilabu bora vya Tanzania, ambavyo vinajulikana kwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki nchini. Leo, tunafuraha kutangaza makubaliano ya udhamini ya miaka 3 na Simba SC kupitia bia yetu bora, Pilsner Lager.

Tuna dhamira ya kutoa rasilimali muhimu kwa Simba Sports Club ili kufikia mafanikio makubwa zaidi. Ushirikiano huu unazidi kuwa zaidi ya kukuza tu bidhaa zetu; ni kuhusu kuendeleza urithi unaovuka vizazi," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, alipoanzisha udhamini huo leo.

Mkurugenzi Mtendaji pia alieleza shukrani zake kwa TFF kwa dhamira yao isiyo na kifani ya kusaidia vilabu vya mpira wa miguu nchini Tanzania na michezo kwa ujumla, na kuhakikisha dhamira hiyo hiyo kutoka kwa udhamini wa Serengeti Breweries Limited kwa Simba SC kupitia chapa yake ya bia ya Pilsner Lager.

"Udhamini huu umekuja wakati muafaka wa kupunguza baadhi ya vikwazo vya kifedha tulivyonavyo katika klabu yetu ambavyo vimezuia utekelezaji wa baadhi ya mikakati ya kimkakati. Udhamini huu pia bila shaka utaiwezesha klabu yetu kufanya vizuri katika ligi ya kitaifa na pia katika Ligi ya Mabingwa ya Afrika," alisema Imani Kajura.

SBL ni mdhamini mzoefu wa mpira wa miguu nchini Tanzania, akiwa ameanzisha mkataba wa miaka minne na Taifa Stars kuanzia 2017 hadi 2011, na kisha miaka sita ya kuwasaidia timu ya taifa ya soka kuanzia 2017 hadi Juni 2023. Katika muda wa miaka kumi, Taifa Stars imefanikiwa kufuzu mara kadhaa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika na kuboresha nafasi yake katika viwango vya FIFA.






LAKE MANYARA MARATHON 2023 FURSA MPYA YA UTALII HIFADHI YA TAIFA ZIWA MANYARA

October 30, 2023 Add Comment

 Na. Jacob Kasiri - Manyara.


Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari ameshiriki mbio za Lake Manyara Marathon 2023 na kusema kuwa ni fursa mpya ya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara, hifadhi inayosifika kwa kuwa na Simba wengi wanaoparamia miti.

Mhe. Nassari alisema "kwa mara ya kwanza Wilaya ya Monduli imeandaa Marathon hii kwa lengo la kufungua fursa mpya ya utalii katika hifadhi yetu na kuongeza mzunguko wa fedha katika wilaya yetu".

"Kwakuwa eneo la Mto wa Mbu liko kimkakati wa kiutalii ndio imekuwa sababu kubwa ya kuvuta watu wengi kiasi hiki. Na tumeona kuanzia tarehe 27.10.2023 wakimbiaji walianza kuwasili hii yote imeongeza pato kwa taifa na mtu mmoja mmoja", aliongeza Mhe. Nassari.

Mbio hizi ndefu (Marathon) licha ya kuongeza fursa za kifedha kwa jamii pia, huimarisha afya na kuondoa magonjwa nyemelezi na kutoa mwanya kwa makampuni makubwa ikiwemo TANAPA kujitangaza na kupata wateja wanaowahitaji.

Afisa Mhifadhi Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Biashara Makao Makuu - TANAPA, Augustine Massesa alisema utalii huu wa michezo umeanza kushika kasi kwa miaka ya hivi karibuni. "Hivyo, niwaase na kuwashauri watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki, licha ya kuimarisha afya pia inakuza utalii".

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Eva Mallya alisema mbio hizi ni fursa kwetu kwa sababu baadhi ya washiriki wamehamasika kuingia hifadhini na kuliingizia Taifa mapato.

"Kwa niaba ya hifadhi tunamshukuru Mkuu wa Wilaya yetu Mhe. Joshua Nassari na waandaaji wa Marathon hii, kwa kipindi chote cha uamasishaji kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imeleta tija kwa hifadhi yetu.

Mbio hizo zenye lengo la kuhamasisha utalii zilizobeba kaulimbiu "Tukimbie Tukitalii" zimefanyika leo tarehe 29.10.2023 zikianzia katika Lango la Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara iliyopo Mto wa Mbu mkoani Manyara.