Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

WAZIRI MCHENGERWA ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI WA MICHEZO,ATAKA WABADILIKE

May 27, 2022 Add Comment




Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati wa akifunga kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kilichoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)



Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa amewataka  viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kutotumia taasisi wanazoziongoza kujinufaisha kwa  vipato tu na badala yake wawe wabunifu na wazalendo ili kuleta  mapinduzi kwenye  michezo  na kuendana  na maono ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ya kutumia michezo kuleta uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.


 Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Mei 27, 2022 wakati akifunga  kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini  kilichoratibiwa  na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatia  maelekezo yake aliyoyatoa wakati akiisimika Bodi  ya BMT hivi karibuni ya kutaka kuwa na utawala bora kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili kuendeleza michezo.


 Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa yapo  mataifa  mbalimbali duniani ambayo  hayana miundombinu ya michezo na  yana idadi ndogo ya watu ukilinganisha  na Tanzania  lakini yamekuwa yakifanya  vizuri kwenye  michezo hivyo amewataka kubadili fikra  potofu ili wanaowaongoza waige  mifano kutoka  kwao hatimaye kuleta mapinduzi makubwa kwenye michezo. 


 “Hatutaweza kupiga hatua kwenye michezo kama   sisi viongozi hatutaweza kubadilika na kuendelea kuwa na fikra potofu ya kudhani vyama na mashirikisho ni mahali pa kujipatia vipato tu. Nawaomba tubadilike mimi katika kipindi changu sitaweza kuruhusu kutokea hayo. Mpango wa matumauni ya kesho lazima tuanze kujenga leo”. ameongeza Mhe. Mchengerwa.


Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeelekeza nguvu kubwa kuendeleza sekta za utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo maana iliunda upya Wizara hii ili iweze kujitegemea, kuongeza bajeti, kutoa punguzo kwenye nyasi bandia ili kuimarisha viwanja vya soka pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo.


Ameongeza kuwa mfuko huo umepewa chanzo madhubuti ambacho  ni fedha za asilimia tano ya mapato yatokanayo na michezo ya kubashiri matokeo ya michezo.


Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kwa kina vigezo   vya muongozo wa kusaidia timu za taifa  kwa kutumia fedha za mfuko wa maendeleo ya michezo na kuja na mawazo ambayo yatafanyiwa  kazi na serikali ili kuwa na uwazi katika usaidiaji wa  timu hizo katika michezo mbalimbali.  


Aidha, amewasihi viongozi hao kufuata  miongozo na taratibu za nchi  sambamba na kuziheshimu  mamlaka  na taasisi zinazosimamia michezo nchini,  kuimarisha  utawala bora na weledi  katika kazi.


Mambo mengine ni pamoja na kuimarisha eneo la utaalamu na taswira za    taasisi zao kwa kuwa na mikakati yenye dira.


Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kujenga miundombinu mipya na ya kisasa ya michezo ambapo kwa upande wake Naibu Waziri, Mhe, Pauline Gekul amewataka wadau washirikiane na kupendana ili kuongoza kwa mafanikio.


Naye Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi amewataka viongozi hao kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato badala ya kutegemea Serikali pekee.

WAZIRI MCHENGERWA ATOA SALAMU AFRIKA

May 25, 2022 Add Comment

 



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa

Na Shamimu Nyaki - WUSM, Dodoma 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amewaasa watanzania kulinda na kuhifadhi rasilimali na kumbukumbu ambazo ni ushahidi wa Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika maeneo waliyopo ambayo kumbukumbu hizo zinapatikana.

Katika taarifa aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari leo  Mei 25, 2022 jijini Dodoma, Mhe. Mchengerwa amesema  Siku ya Afrika ambayo huazimishwa Mei 25 kila Mwaka,ni siku muhimu kwa waafrika wote ambapo kwa mwaka huu  imebebwa na Kauli Mbiu isemayo "Urithi wa Ukombozi, Fahari ya Afrika na Kazi Iendelee".

"Kuthamini utanzania wetu  ni jambo la msingi na ndiyo kielelezo na sifa iliyosababisha Umoja wa Afrika (AU) zamani (OAU) kuichagua Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika na kuipa hadhi ya kuwa Mratibu wa Harakati za Ukombozi hadi nchi zote za Afrika zilipopata Uhuru mwaka 1994" amefafanua Mhe.Mchengerwa.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, ni wajibu wa jamii ya waafrika kuenzi kwa vitendo mashujaa wa Tanzania waliojitoa mhanga Kwa ajili ya Afrika chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika kuadhimisha siku hiyo, watanzania wameaswa kutembelea Ofisi ya Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika  ili kujifunza na kuona ushahidi waTanzania katika kuikomboa Afrika.

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

December 04, 2017

 


Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.