Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo
habariWATANZANIA WATAKIWA KUACHANA NA DHANA POTOFU KWAMBA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI GHARAMA
habariSADC:SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI
habari Uchumi📌 *Yasisitiza utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya Nishati*
📌 *Kapinga ataka SADC kuweka dhamira thabiti na mikakati madhubuti ya utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia*
Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wametaka Sekta ya Nishati kuwa kichocheo cha kuiunganisha Afrika katika kujenga uchumi wake.
Wamesema hayo leo Julai 4, 2025 wakati wakihitimisha mkutano wa SADC jijini Harare nchini Zimbabwe ambao ulilenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.
Akizungumza wakati akihitimisha mkutano huo, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Umeme wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. July Moyo, ameitaka jumuiya hiyo ya SADC kuipa kipaumbele sekta ya nishati na maji ili kuifanya kuwa na tija kwa wananchi katika kukuza uchumi wao kwa kuwa nishati ni chanzo kikubwa cha maendeleo.
Aidha, ameipongeza Tanzania kwa kuandaa na kuwa mwenyeji wa kufanikisha Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati Afrika wa Misheni 300 (M300) ambao ulifanyika kwa mafanikio. Pia, Dkt. Moyo amezishukuru Nchi wanachama zilizohudhuria katika mkutano huo muhimu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola ameitaka SADC kuhakikisha inaiendeleza miradi yote ya kipaumbele katika jumuiya ili kuifanya sekta ya nishati kuwa kimbilio katika kujenga uchumi wa nchi zao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameitaka SADC kuhakikisha inakuwa na mikakati madhubuti ya utekekezaji wa maazimio mbalimbali wanayofikia katika makongamano ya umoja huo ili yawe na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na kuifanya sekta ya nishati kuwa chachu na mkombozi ndani ya SADC.
Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira thabiti na mikakati madhubuti ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi katika SADC.
Mkutano huo uliohitimishwa leo, umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
![]() |
NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AGENDA YA DUNIA,WIZARA INAITEKEKEZA KWA VITENDO - DKT.KAZUNGU
elimu habari*📌Apokea Magari Mawili kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanza kampeni ya kutoa elimu ya uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia nchi nzima*
*📌 Amshukuru Dkt Samia kwa kuwa kinara wa nishati safi na kuibeba ajenda hiyo*
*📌 Umoja wa Ulaya waridhishwa na jitihada za Tanzania kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia*
*📌UNCDF yaahidi kushirikiana na Wizara kuhakikisha watanzania wanafikiwa na elimu ya nishati safi*
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati Jadidifu, Dkt Khatibu Kazungu leo 04 Julai, 2025 amepokea magari mawili yatakayotumika kwa ajili ya kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia chini ya kampeni ya nishati safi ya kupikia Okoa Maisha na Mazingira itakayoendeshwa nchi nzima na Wizara ya nishati kwa kushirikiana na UNCDF.
‘’ Ajenda ya Nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia na sisi Wizara ya Nishati tuko tayari kwa utekelezaji ili kumuunga mkono Mhe. Rais Samia’’ Amesema Dkt. Kazungu
Aidha, ameishukuru Umoja wa Ulaya, na UNCDF kwa kutekeleza mradi wa nishati safi ya kupikia chini ya mfuko wa Cook fund kwa kuwa umesaidia kubadili maisha na mitazamo ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya Nishati safi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Christine Grau amesema umoja wa Ulaya uko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye utekelezaji wa Nishati safi ya kupikia na tayari EU imetoa kiasi cha Euro Milioni 19.4 sawa na shilingi Bilioni 59 kutekeleza miradi ya nishati safi ya kupikia kwa mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro na Mwanza.
Kuhusu magari amesema magari hayo mawili yana thamani ya Euro 130,000 na amewataka wizara ya Nishati kuhakikisha wananchi wa vijijini wanafikiwa na nishati safi ya kupikia
Tanzania inajipanga kutekeleza kwa vitendo mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia chini ya mkakati wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa elimu kwa wananchi na kufikia lengo la Serikali la asilimia 80 ya watanzania kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.