Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

VIJANA ZAIDI YA 350 KATIKA JIJI LA TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA INCLU-CITIES PROJECT

June 11, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga, TANGA

ZAIDI ya Vijana 350 Jijini Tanga wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Inclu-Cities Project uliopo chini ya Programu ya SASA kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya .

Hayo yalisemwa leo wakati wa uzinduzi wa utambulisho wa mradi huo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa taarifa yake wakati wa utambulisho wa mradi huo ,Mkuu wa Chuo cha Veta Tanga Gidioni Lairumbe alisema wakiwemo wanawake asilimia 50 katika Jiji la Tanga bila kusahau uchumi wa bluu ambapo program hiyo ni kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kujiajiri au kuajiwa vijana 150 asilimia 50 wasio na ujuzi kabisa katika fani mbalimbali.

Alizitaja fani hizo ni usindikaji na uandaaji wa chakula,Umeme wa Sola,Uchomeleaji na uungaji wa vyumba pamoja na utengenezaji wa mkaa mbadala ikiwemo mpango wa kuwapa ujuzi vijana walio sokoni ambao utawagusa vijana 150 ikilenga asilimia 50 ya wanawake katika fani.

Mkuu huyo wa chuo cha Veta alizitaja fani hizo ni Usindikaji na uandaaji wa chakula,uvuvi,Umeme wa sokla na uchomeleaji na uungaji wa vyuma sambamba na program ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo usio rasmi ambao utawagusa vijana 150 ukilenga wanawake kwa asilimia 50 katika fani za usindikaji na uandaaji wa chakula,uchomeleaji na uungaji wa vyuma,matengenezo ya pikipiki za umeme na matengenezo ya siku za mkononi.

Alisema kupitia mradi wa utekelezaji wa mradi huo wa Inclu –Cities uliopo chini ya Programu ya SASA kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) kwa ufadhili wa umoja wa ulaya pia kitaanzishwa kitengo cha utoaji wa ushauri wa masuala mbalimbali yahusuyo ujuzi na huduma mbalimbali kwa wanafunzi ,Ukarabati wa jengo la mgahawa pamoja na jiko kama eneo la kujifunzia wanafunzi wa mapishi na kupata vifaa mbalimbali vya kujifunzia

“Lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi kwa lengo la kuzalisha wahitimu wanaohitajika katika soko la ajira na kuifanya VETA Tanga kuwa kituo cha Umahiri wa Utoaji wa Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Sekta husika waweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kukamilika mafunzo hayo “Alisema Mkuu huyo wa chuo cha VETA Tanga.

Alisema kwamba wanaimani kwamba elimu ya vitendo na ushirikiano kati ya waajiri na wadau mbalimbali wa maendeleo itasaidia kuelekea kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza kipato kwa wahitimu na kuwategemea baada ya mafunzo haya zaidi ya asilimia 75 ya wahitimu watakaopata ujuzi watakuwa katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye soko kwa kujiamini.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian alisema kwamba wanaendelea kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa mambo makubwa anayoyafanya yanayopelekea kuungwa mkono na nchi mbalimbali wakiwemo umoja wa ulaya na wamefurahi mradi huo ambao una jumla ya Uero milioni 75 ambazo ni sawa na Bilioni 190 ni jambo kubwa ambalo litasaidia katika mipango ya program mbalimbali

“Lakini niwapongeze Veta kama sehemu ya mradi mliwasiliana na Umoja na Ulaya walipokuja kuwaona wakawa tayari kutekeleza mradi na Jiji na Veta Makao Makuu ambao walikubali mpango huo kuweza kufanyika kwenye maeneo yao na Tanga kwa moja wapo na sisi tunashukuru na kuwapongeza kwa hatua hii nzuri na muhimu kwa maendeleo na huo ndio umuhimu wa uwepo wa chuo hiki”Alisema

Aidha alitaka mchakato wa kuwapata walengwa katika mradi huo wapate vijana wanaotoka kwenye familia ambazo hazina uwezo na ambao watakaotoka wataweze kuwasaidia familia wachague mchanganyiko na wasaidiane na madiwani kuwaibuua watu ambao watakwenda kuwaheshimisha fursa hiyo na kupata kitu baadae cha kubadilisha maisha yao.

Alisema kwamba katika miaka 50 ya chuo cha Veta ndio ambao ambacho kitawakomboa watanzania hasa vijana katikati kulikuwa na wimbi la vyuo vyote za ufundi kuwa kuwa vyuo vikuu lakini misingi ya Baba wa Taifa na dhana ya ujamaa wa kujitegemea ilikuwa ni kupitia mifumo ya vyuo vya ufundi lakini na shule za amali ambazo sasa serikali imerudisha zitawakomboa vijana

Aliongeza kwamba vitawakomboa kwa sababu watatoka wakiwa na maarifa ya jinsi ya kumudu mazingira yao na kinachofanyika ni kuzuri kitasaidia vijana wao huku akiwataka chuo hicho kuendelea kuwapika vijana vizuri waandalieni stadi mbalimbali ikiwemo bustani za maua za kisasa.


Naye kwa upande wake Mshauri Mtaalamu wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) Thomas Aikaruwa Aliwapongeza Veta Tanga kwa kuamua kuanza safari ya maboresho kwenye chuo chao na kuwa kituo cha umahiri kwenye maeneo walioyaainisha.

Alisema kwamba Umoja wa Ulata kupitia Mpango wa Green City chini ya Mpango wa SASA watafanya kazi na Serikali ili kuchangia kwenye mikoa ya Tanga,Mwanza na Pemba lengo kusaidia kuboresha maisha ya watanzania wa kawafikia kwenye miji hiyo mitatu kwa kuboresha miundombinu inayozingatia mabadiliko ya tabia ya nchi.

Alisema pia katika kuboresha hudumu za kijamii kwa wananchi wanaopatikana kwenye mikoa hiyo kwa kuongeza ukuaji uchumi wa mwananchi wa kawaida katika mikoa hiyo katika ukuaji wa uchumi wa mwananchi huyo ambapo mradi huo chini ya shirika la Ujerumani Enable linafanya kazi kwa ukaribu na wadau muhimu katika sekta hiyo ya kukuza ujuzi hasa wadau wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo hayo wanafanya kazi.

Aidha aliwataja wadau hao kuwa ni Veta na Veta ya Pemba na Sido Tanga na Mwanza ikiwemo sekta binafsi ambazo zinapatikana kwenye mikoa hiyo mitatu chini ya uangalizi wa Halmashauri zinazopatikana kwenye mikoa hiyo ya Tanga,Ilemela ,Nyamagana-Mwana na Chakechake-Pemba na nyengine ambazo zinavutiwa kuingia kwenye mpango huo.

Hata hivyo alisema kwamba ujuzi ni dhana muhimu katika kipindi waliochopo hasa ukizingatia mabadiliko ya mitaala ya elimu na wanategemea kutoka na ujuzi hasa mabadiliko ya kisasa na kuibua na kutengeneza ajira ili kuimarisha zilizopo ili viweze kuwa na tija na maeneo yanayotazamiwa kufikiwa.

“Maeneo tunayotazamiwa kufikiwa ni utumiaji huduma za kibiashara na kifedha na uwekezaji kuwe na ubora na mafunzo ya ujuzi yanayotolewa na taasisi zilizotajwa yanayozingata mahitaji ya sasa na ujasiriamali na bajeti ya shughuli zao ni Bilioni 190 ambazo ni kama euro milioni 75 na muda wa mradi huo ulianza mwaka 2022 na utakwenda mpaka mwaka 2027”Alisema

Mwisho.

BENKI YA CRDB YANG'ARA KATIKA TUZO ZA AFRICAN BANKER 2025,YATWAA TUZO YA BENKI BORA KWA WAJASIRIAMALI

June 05, 2025 Add Comment

 


Dar es Salaam, 05 Juni 2025 – Benki ya CRDB imeandika ukurasa mpya wa mafanikio baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya Benki Bora kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME) katika hafla ya tuzo za sekta ya benki barani Afrika ‘African Banker Awards 2025,’ iliyofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jijini Abidjan, Côte d’Ivoire.

Kaulimbiu ya mwaka huu wa tuzo hizo ilikuwa “Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo Endelevu,” ikiakisi umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchochea ukuaji wa kijani, ujumuishi wa kijinsia na uhimilivu wa kiuchumi barani Afrika.

Katika mwaka huu ambapo Benki ya CRDB inaadhimisha miaka 30 ya huduma ubunifu, ilipata heshima ya kutajwa katika vipengele vinne vikuu, vikiwemo: Benki Bora kwa Wajasiriamali (Mshindi), Banker of the Year – kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki, Abdulmajid Mussa Nsekela, Benki Bora kwa maendeleo endelevu, Benki Bora ya mwaka (AFAWA).

Tuzo hiyo ya Benki Bora kwa Wajasiriamali ilipokelewa na Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa, ambaye alieleza kuwa ushindi huo ni kielelezo cha dhamira ya Benki hiyo ya kuwapatia wateja na watanzania kwa ujumla wake huduma bunifu za fedha. Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, benki hiyo imeendelea kuwa nguzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wajasiriamali, hususan vijana na wanawake. “Ushindi huu si wetu pekee, bali ni wa jamii nzima tunayoihudumia,” ameeleza Raballa.

Benki ya CRDB imejidhihirisha kuwa mshirika mkubwa wa wajasiriamali nchini ikitoa uwezeshaji wa hadi shilingi bilioni 5. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2024 mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.2 imetolewa kwa zaidi ya wajasiriamali 230,000 kutoka sekta mbalimbali.

Benki ya CRDB imekuwa kinara katika huduma bunifu kwa wajasiriamali nchini, ikiwa Benki ya kwanza kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhudumia kundi hili la wateja mwaka 2000.

Mwaka 2024, Benki ya CRDB ilifanya maboresho makubwa ya akaunti ya wajasiriamali ‘Biashara Akaunti’, ikiboresha pia fursa za uwezeshaji kupitia mikopo, pamoja na kutoa suluhisho za kidijitali kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa upokeaji malipo kwa wateja kupitia huduma za ‘LIPA HAPA’ na mashine za manunuzi (PoS).

Aidha, Benki hiyo pia inazo bidhaa mahususi kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashra wanaogaiza bidhaa nje ya nchi kama ‘Mkopo wa Komboa,’ ukisaidia wateja kutoa mizigo yao bandarini kwa wakati. Hatua ambayo imeondoa ucheleweshaji katika uzalishaji na usambazaji wa bidhaa sokoni.

Sambamba na huduma, Benki pia inatoa huduma za ufadhili wa biashara (trade finance) na ufadhili wa rasilimali (asset financing), ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wateja katika kukuza na kuimarisha biashara zao.

Benki ya CRDB pia imekuwa ikiwapatia wajasiriamali uzoefu wa biashara kimataifa kwa kuwapeleka nchi mbalimbali duniani ili kuwapa fursa za kujifunza na kuongeza thamani kwenye biashara wanazozifanya, huku ikiwajengea uwezo wa kushindana katika masoko ya kimataifa. Hii ni hatua muhimu katika kukuza ushindani wa bidhaa na huduma za Kitanzania.

Aidha Benki ya CRDB imekuwa ikishirikiana kimakakati na tasisi za kimataifa zinazolenga kuwasaidia wajasiriamali kama vile AGF, PROPARCO, DFC, GuarantCo na GCF pamoja na taasisi za hapa nchini kama vile PASS na TADB. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Benki hiyo imeweza kukusanya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 700, ikionyesha imani ya washirika wa kimataifa katika uwezo na utayari wa benki katika kuwawezesha wajasiriamali nchini.

“Katika miaka 30 ya uwepo wetu, tumejifunza kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila kuwainua wajasiriamali. Tunaendelea kujipanga kufikia wengi zaidi kupitia mikakati madhubuti ya ujumuishi, hasa kwa wanawake na vijana, kama sehemu ya kusaidia ajenda ya serikali ya maendeleo jumuishi,” aliongeza Raballa.
Tuzo hii ni ushahidi mwingine wa jinsi Benki ya CRDB imejikita kwa dhati katika kuwa daraja la mafanikio kwa maelfu ya wajasiriamali nchini. Kuelekea mbele, Benki hiyo imeendelea kuonyesha utayari wake katika kuwahudumia wajasiriamali kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa kundi hilo la wateja katika Mkakati wake wa Muda wa Kati wa Biashara wa 2023 – 2027.