Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

TPAWU YATAKA MCHAKATO KIMA CHA CHINI SEKTA BINAFSI UHARAKISHWE

May 27, 2025 Add Comment

 

 Mwenyekiti TPAWU Taifa Daniel Bariyanka Joachim akizungumza kwenye kikao hicho

Na Godwin Myovela, Morogoro

CHAMA cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo nchini (TPAWU) kupitia kikao cha Baraza Kuu la chama hichoTaifa, kimeomba kuharakishwa kwa mchakato unaoendelea wa kupanga kima cha chini cha mshahara sekta binafsi, kuzingatia maoni ya wadau-sambamba na kuhakikisha kima hicho kutopungua Tsh. 350,000 kwa mwezi, ili kusaidia kumudu gharama za maisha.

Mwenyekiti TPAWU Taifa, Daniel Joachim, alitoa tamko hilo wakati wa kikao hicho kilichofanyika mkoani hapa mwishoni mwa wiki, ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza baraza hilo limezingatia hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi mwaka huu, kuhusu utaratibu wa kisheria unaoendelea kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.

“Kufuatia tamko la Rais mkoani Singida, tunamuomba waziri mwenye dhamana kuharakisha mchakato wa utafiti wa kima cha chini cha mshahara sekta binafsi na kitangazwe kwenye gazeti la serikali ili kianze kutumika sambamba na kile cha watumishi wa umma kitakachoanza Julai Mosi mwaka huu,” alisema Joachim  na kuongeza;

“Wakati wa mchakato huo baraza linamuomba waziri mwenye dhamana pamoja na bodi ya kima cha chini cha mshahara sekta binafsi ifanye maandalizi hayo kwa kuzingatia maoni ya wadau ambao ni waajiri na wafanyakazi.”

Aidha, baraza hilo limewaomba waajiri wote kuzingatia takwa la sheria la majadiliano mahali pa kazi ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi kupitia mikataba ya hali bora za kazi kwa mujibu wa kifungu cha 68 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini sura ya 366.

Katika hatua nyingine, Tpawu imekemea na kulaani vitendo vya baadhi ya waajiri ambao hutumia kima cha chini cha sekta husika kama sababu ya wao kutoongeza mishahara, jambo ambalo halikubaliki.

“Huu ni mtazamo potofu sababu unakwamisha lengo la kutungwa kwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, pamoja na Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani Na. 98 vinavyotoa haki ya majadiliano mahali pa kazi,” alisisitiza Joachim

Hata hivyo, alimsihi Rais Samia kusaidia wafanyakazi wa sekta binafsi hasa sekta ya kilimo kupata mshahara unaoweza kuwasaidia kumudu gharama za maisha ya kila siku-mathalani-ikiwa sekta ya umma watalipwa kima cha chini Tsh.500,000 basi sekta binafsi kima cha chini kabisa kisipungue Tsh.350,000 kwa mwezi.Katibu Mkuu TPAWU Taifa John Vahaye akizungumza kwenye kikao hicho.Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye kikao hicho

Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakifuatilia ajenda mbalimbali kwenye kikao hicho.Wajumbe Baraza Kuu TPAWU Taifa wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye kikao hicho 

Nyongo Ashuhudia Utiaji Saini wa Makubaliano ya Ushirikiano kati ya TIC na Axcel Africa

May 26, 2025 Add Comment
Osaka- Japan 26 Mei, 2025

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, ameshuhudia tukio muhimu la utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kampuni ya Axcel Africa. 

MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO

May 26, 2025 Add Comment

Na Mwandishi Wetu, OR- TAMISEMI


Mkuu wa Kitengo Cha Mawasilino Serikali na Msemaji Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI, John Mapepele ametoa wito kwa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutanguliza uzalendo na weledi wakati wa utoaji wa taarifa ili habari hizo ziwe na tija kwa taifa.

MBEKI AWAASA VIONGOZI WA AFRIKA KUWA WAZALENDO KATIKA KULINDA MASLAHI YA BARA LAO

May 24, 2025 Add Comment

 Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Thabo Mbeki, amewahimiza viongozi wa Bara la Afrika kuwa wakweli na waaminifu katika kulinda maslahi ya bara lao, ili kufanikisha malengo ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Waafrika.


Mheshimiwa Mbeki ameyasema hayo katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika tarehe 23 Mei, 2025 jijini Dar es Salaam .

Mheshimiwa Mbeki amesisitiza kuwa maendeleo ya Bara la Afrika yatapatikana endapo viongozi wataweka mbele maslahi ya nchi zao na kuongoza kwa uadilifu, uwazi, na dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya kwa Waafrika wote.

“Tunapoadhimisha Siku ya Afrika mwaka huu kwa kaulimbiu ‘Haki kwa Waafrika na Watu wa Asili ya Kiafrika Kupitia Fidia: Kuangazia Historia Yetu, na Kuunda Mustakabali Wetu,’ tunakumbushwa kuwa haki siyo mwisho, bali ni dai endelevu la ukweli, heshima, na uongozi unaoakisi hali halisi za watu wetu. Tuwekeze katika elimu, ubunifu, ushirikishaji wa vijana katika maamuzi, na kupambana na ufisadi unaoharibu maendeleo,” alifafanua Mheshimiwa Mbeki.

Ameongeza kuwa Bara la Afrika lina utajiri na uwezo mkubwa ambao unahitaji Viongozi wanaowaza zaidi ya uchaguzi, wasioogopa uwajibikaji, wenye maono, na wanaotanguliza maslahi ya wananchi wao na Taifa, kuliko matakwa yao binafsi.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo alisema kila mwafrika lazima atakafari mafanikio, changamoto na matarajio ya kuinua maendeleo ya Afrika kwa amani ya utulivu.

Amesisitiza umuhimu wa kuwaenzi viongozi walioendeleza fikra za Uafrika na wanaoendelea kupigania ukombozi wa kiuchumi na mshikamano wa Bara la Afrika kwani wameacha urithi mkubwa kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

“Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, nichukue nafasi hii kusema kuwa tunawakumbuka na kuwapongeza waanzilishi wa Umoja wa Afrika (OAU) — ambao ndoto yao ya kuunganisha na kushirikisha zaidi mataifa ya Afrika imeendelea kuishi hadi leo. Tunawakumbuka pia kwa heshima kubwa viongozi waliowafuata, ambao waliendeleza dhima ya Uafrika (Pan-Africanism) na wanaoendelea kupigania ukombozi wa kiuchumi na mshikamano wa bara letu tukufu,” alisema Mhe. Kombo

Hafla hiyo iliwakutanisha pamoja mabalozi , viongozi wa Serikali, Mabalozi wastaafu, viongozi wa serikali, wanadiplomasia, wasomi, pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia na kijamii kwa ajili ya kusherehekea mshikamano, utofauti na maendeleo ya Afrika.

Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali za kitamaduni, vyakula kutoka nchi za Afrika, pamoja na tafakuri juu ya mchango wa mataifa ya Afrika katika historia na maendeleo ya sasa kuelekea amani na kujitegemea.

Hafla hiyo ilifanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 62 ya Umoja wa Afrika, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya Siku ya Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 25 Mei ya kila mwaka.
.







RAIS DKT. SAMIA ATOA BILIONI 42.34 KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA

RAIS DKT. SAMIA ATOA BILIONI 42.34 KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA

May 24, 2025 Add Comment








Na Prisca Libaga RAS Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa kiasi cha shilingi bilioni 42.34 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha ili kumaliza migogoro ya ardhi na uendelezaji wa maeneo mbalimbali katika mkoa huo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Moshono, Jijini Arusha, Mhe. Makonda amesema fidia hiyo imetolewa kwa maeneo kadhaa yaliyoguswa na miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara, uwanja wa ndege, maeneo ya jeshi, na uchimbaji wa madini.

Katika Jiji la Arusha, eneo la Losirwa lililokuwa chini ya matumizi ya Jeshi limepewa fidia ya shilingi Bilioni 2.27, ambapo fidia hiyo imekwishalipwa, eneo la Oloresho kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya AFCON, limetengewa fidia ya shilingi bilioni 7.27, barabara ya Mianzini – Ngaramtoni nayo imelipwa fidia ya shilingi bilioni 3.49 ambapo fedha hizo zimelipwa tayari pamoja na eneo la barabara ya Mirongoine – Olmot limepokea fidia ya shilingi milioni 591.64 ambayo nayo imelipwa.

Aidha, Wilaya ya Arumeru, fidia kwa eneo la Jeshi lililopo Duluti imetolewa kwa kiasi cha shilingi bilioni 7.9 na tayari imelipwa yote kwa walengwa.

Wilaya ya Karatu imepata fidia ya shilingi bilioni 5.9 kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Manyara uliopo katika eneo hilo, hatua inayolenga kufanikisha uboreshaji wa miundombinu ya usafiri wa anga.

Kwa upande wa Wilaya ya Monduli, eneo la Engaruka, ambalo linahusishwa na shughuli za uchimbaji wa madini ya magadi soda, limetengewa fidia ya shilingi bilioni 14.9, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya madini.

Katika hatua nyingine, Mhe. Makonda amewataka viongozi wote wa Mkoa huo kuacha mara moja tabia ya kuwaondoa wananchi kwenye maeneo yao bila kuwapa fidia stahiki, akisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita inalenga haki, usawa na maendeleo ya watu na ndiyo dhamira ya Rais Dkt. Samia katika kulinda haki za wananchi na kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya Taifa.