Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts
MKURUGENZI MKUU REA AISISITIZA BODI MPYA YA ZABUNI KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU
habari-Aipongeza Bodi ya Zabuni iliyomaliza muda wake kwa kazi nzuri iliyofanya
BENKI YA DUNIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI WA MIRADI YA REA
habari-Yaahidi kuendeleza ushirikiano
-Ni miradi ya usambazaji umeme vitongojini na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
RAIS STUBB AZINDUA MRADI WA EURO MILIONI 20 WA UHIFADHI WA MISITU – FORLAND
habari
Rais wa Jamhuri ya Finland, Mhe. Alexander Stubb, leo amezindua rasmi Mradi wa Kusimamia Uhifadhi wa Misitu, Matumizi Bora ya Ardhi na Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu (Forestry, Land Use, and Value Chains Development in Tanzania – FORLAND), wenye thamani ya Euro milioni 20.
Mradi huo unalenga kukuza kanuni endelevu za uhifadhi wa misitu, kuboresha maisha ya wananchi, kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania, pamoja na kuendeleza usimamizi wa misitu katika jamii, upandaji miti, na maendeleo ya mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Mei 16, 2025 katika Bustani ya Botanical Garden jijini Dar es Salaam, Rais Stubb ameshiriki katika zoezi la upandaji miti na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Tanzania na Finland katika sekta ya misitu.



“Nina imani mti nilioupanda utakua kama yalivyo mashirikiano kati ya nchi zetu katika sekta ya misitu, hususan kupitia mradi huu wa FORLAND,” amesema Rais Stubb.
Aidha, Rais Stubb ameeleza kuwa Finland ina misitu inayochukua asilimia 70 ya eneo la nchi hiyo, na kwamba bidhaa zake za misitu zinatambulika kwa ubora na uimara wake.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), amesema kuwa mradi wa FORLAND unatekelezwa katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimali za misitu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii zinazozunguka misitu hiyo.

“Nchi yako (Finland) imekuwa mshirika muhimu kwa Tanzania katika sekta ya misitu, ikiwa imesaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile Mpango wa Usimamizi wa Eneo la Hifadhi ya Usambara Mashariki (1988–2002), vyuo vya misitu nchini Malawi, Tanzania na Zambia (1999–2005), Programu ya Kitaifa ya Misitu (2005–2010), pamoja na Biashara ya Kibinafsi ya Misitu na Kaboni (2010–2011),” amesema Mhe. Chana.
Ameongeza kuwa Finland pia imeisaidia Tanzania kupitia Programu za Kitaifa za Misitu na Nyuki (2013–2016), pamoja na Ufuatiliaji na Tathmini ya Rasilimali za Misitu (NAFORMA) tangu mwaka 2009.
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wanadiplomasia na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania na Finland.


WAZIRI AWESO ACHAGULIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA ZAMCOM 2025/2026
habariBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia Mhe Caesar Chacha Waitara, amemwakilisha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb), Waziri wa Maji katika Mkutano wa 12 wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission-ZAMCOM) uliofanyika tarehe 15 Mei 2025 jijini Windhoek, Namibia.
Katika mkutano huo wa ZAMCOM unaojumuisha nchi nane za Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia na Zimbabwe, Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ZAMCOM katika kipindi cha mwaka 2025/2026.

Subscribe to:
Posts (Atom)