CCM TANGA KUSHIRIKIANA NA TFF KUBADILISHA MUONEKANO WA UWANJA WA CCM MKWAKWANI
habari michezo
Na Oscar Assenga,TANGA
KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wamefanya ziara maalumu ya ukaguzi wa uwanja wa CCM Mkwakwani ambao umefanyiwa maboresho makubwa na hivyo unaweza kutumika kwenye mchezo wa nusu fainali wa CRDB Federation Cup kati ya timu ya Yanga na JKT.
Akizungumza mara baada ya kuutembelea uwanja huo,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman alisema kwamba uwanja huo kutokana na maboresho makubwa upo tayari kwa ajili ya mchezo huo utacheza Mei 18 mwaka huu.
Alisema kwamba walifanya maboresho makubwa ya uwanja huo sehemu ya kuchezea ambayo ilikuwa na changamoto awali kwa jitihada walizifanya viongozi kwa kushirikiana na TFF kupitia Rais Karia waliwaunga mkono CCM kwa jitihada za kufanya ukarabati wa uwanja wao na TFF kugharamia majani sasa mambo yapo vizuri.
Aidha alisema lakini matarajio yao kwa kushirikiana na TFF wameshaandaa michoro namna ya kuubadilisha muonekano wa uwanja huo uwanja wa Mkwakwani kwa kuweka viti na kutengeneza jukwaa la kisasa.
“Lakini pamoja na hilo pia tutabadilisha muonekano wa vyumba vya kubadilisha nguo,vyoo nk na sasa hivi tumeshakamilisha michoro na tupo kwenye mchakato wa kutafuta wadau ili waweze kutuunga mkono
Hata hivyo alisema kwamba mchezo wa Nusu Fainali hiyo kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga ni heshima kubwa kwao na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuweza kuipa sapoti nusu fainali hiyo .
WMA YAHAKIKI VIPIMO ASILIMIA 99 YA LENGO
habariTANZANIA,MOROCCO KUCHOCHEA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI
habari.jpg)
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu, Mhe. Leila Benali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco, Mazungumzo hayo yamefanyika leo Mei 14, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati nchini Morocco.
📌 Matumizi ya teknolojia kupewa kipaumbele Sekta ya Nishati
📌 Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Tanzania na Ufalme wa Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa matumizi ya teknolojia katika Sekta ya Nishati ili kuiwezesha sekta hiyo kuwa na mchango endelevu nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipokutana na Mwenyeji wake Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco.
"Mwaka 2016 Tanzania na Morocco zilisaini hati ya makubaliano (MoU) ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya umeme, mafuta na matumizi ya nishati mbadala ili yapewe kipaumbele katika nchi hizo, ". Amesema Dkt. Biteko
Mhe. Dkt. Biteko amesema pamoja na maendeleo ya nishati yaliyofikiwa, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati mbadala ikiwa na matarajio ya kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda na madini jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.
Ametaja mambo mengine ni pamoja na kubadilishana uzoefu miongoni mwa wataalam katika sekta ya nishati ikilenga kuifanya kuwa na tija kwa taifa na uchumi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali amesema kuwa Tanzania inaweza kubadilisha sura yake kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi.
Amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana gizani hivyo, njia ya kuleta maendeleo na ustawi wa watu ni kuwaangaza maisha yao kwa kupitia sekta ya Nishati.
Aidha, Mhe. Benali amepongeza kwa dhati juhudi za Rais Samia kuwa kinara wa maendeleo ya nishati safi ya kupikia, Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi katika eneno la Morocco, Mhe. Ally Mwadini, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).
Mwisho.