Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

DKT. YONAZI AKUTANA NA UJUMBE WA IFAD NA TIMU YA WATAALAM NA WATEKELEZAJI WA PROGRAMU YA AFDP

April 11, 2025 Add Comment


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025


NA. MWANDISHI WETU - DODOMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Sera,Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Majumuisho (wrap-up) cha Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo  (IFAD) na Timu ya Wataalamu wanaotekeleza Programu ya Kuendeleza  Kilimo na Uvuvi (AFDP) baada ya kukamilika kwa ziara ya kutembelea na kukagua maeneo yanayotekeleza programu hiyo.

Timu hiyo ya IFAD na wataalam ilitembelea maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa Programu ya AFDP kwa sekta za kilimo na uvuvi Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Aidha, timu hiyo ilitembelea pia Mradi wa Kuimarisha na Kuendeleza Upatikanaji wa Lishe kwa Wafugaji Wadogo wa Viumbe Maji na Wakulima wa Mwani (ARNSA).

Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Aprili, 2025 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Nchini (IFAD) Bw. Sakphouseth Meng akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025

Katika kikao hicho Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alipongeza maendeleo mazuri ya utekelezaji program hiyo na kusema kazi zinazofanywa na mradi kwa sasa zinaonekana huku akiwasihi kuendelea kuimarisha mafanikio hayo na kuahidi kushirikiana  na TAMISEMI kwa lengo la kuwafikia wanufaika wa program hii.

Baadhi ya wajumbe wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025
Baadhi ya wajumbe wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025


“Serikali kwa kushirikiana na IFAD itahakikisha inaleta matokeo chanya kwa kuzingatia mipango na mikakati inayotekelezwa na Program hii inawanufaisha walengwa,” Akisema Dkt. Yonazi 

Aidha, akieleza umuhimu wa Mradi Mkurugenzi Mkaazi wa IFAD Nchini Bw. Sakphouseth Meng amelezea kuwa upo umuhimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa sehemu ya utekelezaji wa programu ili kuwafikia walengwa na kueleza umuhimu wa sekta binafsi  kushirki katika Programu ili kuweza kuwafikia walengwa wengi zaidi na pia kuwa endelevu.


=MWSISHO=

TANZANIA YASAINI MKATABA MPYA WA USAFIRI WA BAHARINI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA

April 11, 2025 Add Comment


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini rasmi Mkataba Mpya wa Usafiri wa Baharini wa Afrika wa mwaka 2010, hatua muhimu inayoashiria kuimarika kwa dhamira yake ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya bahari kikanda na kimataifa. 


Hafla ya utiaji saini imefanyika, leo tarehe 11 Aprili 2025 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mashirika ya Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick Salum, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba huu ulipitishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1994 na Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU), na ukafanyiwa marekebisho mwaka 2010 na Umoja wa Afrika ili kuakisi changamoto na matarajio mapya katika sekta ya usafiri wa baharini. Lengo kuu la Mkataba huu ni kukuza mfumo wa usafiri wa baharini barani Afrika ambao ni shirikishi, salama, unaotegemewa, unaozingatia mazingira na unaochochea maendeleo ya kiuchumi.

Kwa kusaini Mkataba huu, Tanzania inathibitisha upya kujitolea kwake kwa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya bahari, sambamba na malengo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) ya kuimarisha usimamizi wa bahari duniani, usalama wa vyombo vya majini na ulinzi wa mazingira ya baharini.

Katika hotuba yake baada ya utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Malick Salum, alisema:


“Hili ni tukio la kujivunia kwa Tanzania. Kwa kusaini Mkataba Mpya wa Usafiri wa Baharini wa Afrika, hatuchangii tu ajenda ya bara la Afrika bali pia tunafungua milango ya ushiriki mpana katika majukwaa ya kimkakati yanayokuza maslahi yetu ya kitaifa na kikanda. Ni tamko kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana, kubuni na kuongoza katika sekta ya bahari barani Afrika.”

Moja ya manufaa makubwa ya kusaini Mkataba huu ni kwamba TASAC sasa inapata fursa ya kuwa mwanachama rasmi wa Chama cha Mamlaka za Usafiri wa Baharini Afrika (AAMA), taasisi iliyoanzishwa chini ya Mkataba huu kwa ajili ya kuratibu, kuoanisha na kukuza sera na utekelezaji wa usafiri wa baharini barani Afrika.



NSEKELA APOKEA MAELEKEZO YA SERIKALI KUIFUFUA SEKTA YA CHAI

April 08, 2025 Add Comment

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Chai Tanzania (TBT) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB pia, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akipokea vitendea kazi vya majukumu yake kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (wa kwanza kushoto) katika mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa sekta ya chai nchini uliofanyika jijini Dodoma leo. Wengine katika picha ni wajumbe wa bodi hiyo ya wakurugenzi ambao ni Imani Kajula (wa pili kulia) na Nashon Kamnyungu (wa kwanza kulia).
======   =======

Dodoma. Tarehe 8 Aprili 2025: Katika mkakati wa kuongeza mchango wa sekta ya chai nchini, serikali imemuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB pia, Abdulmajid Nsekela kuhakikisha anatumia uzoefu wake katika sekta ya fedha pamoja na uzoefu walionao wajumbe wake kushughukia changamoto zinazorudisha nyuma maendeleo ya chai nchini.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe alipozindua bodi mpya ya wakurugenzi ya TBT kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa tasnia ya chainchini uliofanyika jijini hapa.

Bashe amesema tangu awe waziri wa kilimo haridhishwi na maendeleo yaliyopo kwenye zao la chai kutokana na mambo mengi yanayoendelea ikiwamo kushuka kwa mapato yatokanayo na mauzo yake nje ya nchi, wasafirishaji kutoelewa kwa uwazi kiasi wanachokipeleka nje ya nchi na kushuka kwa kiasi kinachozalishwa nchini kilamwaka.

“Tulipokuwa tunatafuta mwenyekiti mpya wa Bodi ya Chai Tanzania tulisema tumpate mtu anayetoka sekta ya fedha atakayeijua sekta ya chai ambayo changamoto yake kubwa ni upatikanaji wa mikopo ili ashiriki kuitatua changamoto hiyo na kuifanya sekta hii ikue na kuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye kipato cha wakulima na wadau wa sekta ya chai pamoja na kuchangia zaidi kwenye pato la taifa,” amesema Mheshimiwa Bashe.

Baada ya kumpata mwenyekiti, amesema waliwatafuta wajumbe wenye ujuzi na uzoefu katika sekta tofauti ikiwamo masoko ili wasaidie kuweka mkakati wa kuitengenezea nembo imara chai ya Tanzania itakayoiwezesha kushindana kimataifa.
Kwenye maelekezo yake kwa bodi hiyo ya wakurugenzi pamoja na menejimenti ya TBT, Waziri Bashe amesema changamoto zote zilizopo kwenye sekta ya chai ni mfumo wake hivyo ameitaka bodi ya wakurugenzi kuupitia mpango mkakati waTBT pamoja na sera ya chai na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuziondoa kero zilizopo.

“Hakikisheni kunakuwa na uwazi wa taarifa kwa sababu wapo baadhi ya wasafirishaji ambao hawaisajili mikataba yao yote hivyo kuinyima serikali taarifa sahihi. Kwa msafirishaji atakayebainika kutotoa taarifa za mzigo anaosafirisha afutiwe leseni. Sekta ya chai inao wadau wasiopenda kukutana, kila mmoja anataka afanye mambo yake kivyake. Undeni kamati itakayowahusisha wadau wengine kuangali namna ya kuyashughulikia matatizo tuliyonayo ili tuwe na chai bora zaidi,” amesisitiza Waziri Bashe.

Akionyesha utayari wa kuyatekeleza maelekezo hayo, Nsekela aliyeteuliwa Februari 2025 kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TBT amesema anayo imani watazishughulikia kero zilizopo na kuifanya sekta ya chai kuwa na mchango mkubwa zaidi kuanzia kwa wakulima mpaka viwanda vinavyolichakata zao hilo.

“Tunahitajia maridhiano kwa kuwajumuisha wadau wote katika sekta ya chai. Asiwepo anayefaidi zaidi ya mwenzake. Ni lazima tufanye mabadiliko ya uwazi. Kila mdau awe na atoe taarifasahihi. Katika hatua hizo zote, tutahitaji ustahimilivu wa kuleta maboresho tunayoyakusudia. Tutafanya marekebisho muhimu katika mnyororo mzima wa zao la chai na tukisikilizana, tutafanikiwa kujenga pamoja,” amesema Nsekela akizinukuu 4R za Rais Samia Suluhu Hassan na kusisitiza kwamba zikitumika katika maeneo tofauti zinaweza kubadili hali iliyopo na kuleta maisha bora kwa Watanzania.
Licha ya uzoefu wake mkubwa katika sekta ya fedha nchini, Nsekela pia anaifahamu sekta ya kilimo kwani alikuwamwenyekiti wa Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHTDA) kabla haujaunganishwa na TBT hivi karibuni na ni mwenyekiti wa Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.

Tanzania kuna zaidi ya wakulima wadogo 32,000 wa chai huku wananchi wengine zaidi ya milioni 2 wakipata ajira zisizo za moja kwa moja katika sekta hii.
Kuanzia Disemba 2024 hadi Machi 2025, Tanzania imeingiza zaidi ya Shilingi bilioni 50.25kutokana na vibali vya kusafirisha chai nje ya nchi vinavyotolewa na TBT.

Kwa mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imewavutia wawekezaji waliowekeza katika maeneo ya Kilolo, Njombe na Mbeya.Aidha, wawekezaji na wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali duniani wameendelea kujitokeza ili kuwekeza na kununua chai ya Tanzania. 
Akizungumzia baadhi ya kero zilizopo, Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya kutoka halmashauri zinazolima chai nchini, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mheshimiwa Jaffer Haniu ameitaja bei ndogo ya majani mabichi ya chai na kuchelewa kwa malipo ya wakulima pamoja na kufungwa kwa viwanda vya chai kuwa kunawakatisha tamaa wakulima.





RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AWASILISHA SALAMU ZA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA RAIS WA UGANDA MHE YOWERI KAGUTA MUSEVENI JIJINI KAMPALA LEO

April 08, 2025 Add Comment

 

Pembenzoni mwa Mkutano wa Uongozi wa Afrika wa nane jijini Kampala Uganda leo, Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kama mjumbe maalum, amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. 


Rais Museveni alimshukuru Dkt Kikwete kwa kumtembelea na kumuomba amfikishie salamu zake kwa Mheshimiwa Rais Samia na watu wa Tanzania.



MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI UTOAJI WA TUZO ZA UANDISHI BUNIFU

April 07, 2025 Add Comment

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo itafanyika Aprili 13,2025 kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam..

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 7, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama amesema vigezo vilivyotakiwa kutumika katika kushiriki kushindania Tuzo hiyo vilitangazwa kna pia mwitikio mwaka huu ni kama ilivyokuwa miaka miwili ya nyuma, umekuwa mzuri.

Amesema Tuzo hiyo kwa Mwaka huu wa 2024 /25 inahusisha nyanja nne za ushairi, riwaya, hadithi za watoto na tamthiliya.

"Utaratibu wa zawadi kwa washindi utabaki kama ilivyokuwa miaka iliyopita yaani, Mshindi wa kwanza Shilingi milioni 10, Muswada wake utachapishwa na serikali na kusambazwa shuleni na maktaba za taifa, Ngao na Cheti. Mshindi wa Pili atapata Shilingi milioni 7 na Cheti, pia Mshindi wa tatu nae atapata Shilingi milioni 5 na Cheti". Ameeleza Prof. Mlama.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa serikali inataka kuhamasisha utamaduni wa kusoma vitabu nchini ndio maana wanaelea kuhamasisha watu waweze kutenga muda wa kujisomea vitabu.

"Watanzania wengi hawana utaratibu wa kujisomea vitabu, hivyo tunaamini kwa kutumia waandishi wetu nchini wataweza kuandika vitabu na kuhamasisha watu kusoma vitabu". Amesema Prof. Mkenda.

Amesema kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa mwandishi mzuri aliweza kuandika vitabu mbalimbali  na namna amechangia kukuza lugha ya kiswahili hivyo kumuenzi kwake wameamua siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kuwepo kwa utoaji wa tuzo hizo.