KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YARIDHISHWA NA HATUA ZA UTEKELEZAJI MRADI WA TAZA
habariNaibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Tanzania na Zambia (TAZA) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikikagua miradi ya Umeme katika Mkoa wa Iringa tarehe 19 Machi 2025
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mathayo Davidi akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Kiseda wilayani Mafinga wakati Kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa Umeme wa Tanzania na Zambia (TAZA) katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikikagua miradi ya Umeme katika Mkoa wa Iringa tarehe 19 Machi 2025
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Tanzania na Zambia (TAZA) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ikikagua miradi ya Umeme katika Mkoa wa Iringa tarehe 19 Machi 2025



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Tanzania na Zambia (TAZA) unaohusisha njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 pamoja na Vituo 5 vya kupoza umeme kikiwamo kituo cha Kisada.Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza kuridhishwa .kwake na hatua ya utekelezaji wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.David Mathayo amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika Mkoa wa Iringa tarehe 19 Machi 2025 ukiwemo mradi wa TAZA.
Mhe. Mathayo amesema Mradi huo ni muhimu kwa kuwa una manufaa makubwa kwa nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika ambapo utawezesha nchi hizo kuuziana umeme kupitia Tanzania.
Ameeleza kuwa, mradi huo utakapokamilika utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe pamoja na kufikisha umeme wa Gridi katika Mkoa wa Rukwa.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme wenye msongo wa Kilovolti 400, kutoka Sumbawanga kupitia Mpanda na ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme katika eneo la Kidahwe mkoani Kigoma hali itakayoimarisha umeme katika Mkoa wa Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amesema kuwa tayari Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliopisha eneo la ujenzi wa mradi pamoja vituo vya kupoza umeme.
Kapinga amesema tayari zaidi ya shilingi Bilioni 17 zimeshalipwa kwa Wananchi zaidi ya elfu 6 ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Mradi huo.
Amefafanua kuwa mradi huo unajengwa kwa fedha za Watanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) na Umoja wa Ulaya(EU).
Akizungumzia ujenzi wa Kituo cha Kisada, Kapinga amesema zaidi ya wakazi 70 wanaozunguka eneo hilo watapata ajira za muda mfupi, huduma ya maji safi na salama pamoja na kuboreshewa Barabara ya kutoka Nyororo kwenda Kisada yenye urefu wa kilomita 15 kutoka Barabara kuu iendayo Mbeya.
Amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo muhimu ili ukamilike kwa wakati na kuleta matokeo Chanya yaliyokusudiwa ikiwemo upatikanaji wa umeme wa uhakika na wakutosha kulingana na mahitaji ya nchi.
DKT.BITEKO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI
habari📌 Azindua taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji mwaka 2023/24
📌 Upotevu wa maji wasababisha hasara ya shilingi bilioni 114.12
📌 Maganzo yaibuka kidedea, Rombo yavuta Mkia utoaji wa huduma
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24 na kusema upatikanaji wa huduma za maji ni haki ya msingi hivyo ni muhimu kulinda vyanzo vya maji kuwezesha upatikanaji wake.
Dkt. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam Machi 19, 2025 ambapo amesema pamoja na jitihada zinazoendelea jamii ina wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira, kupanda miti na kuhifadi misitu ili kuendelea kupata na kutumia rasilimali maji.
“Tusipotunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira tutajikuta katika mtanziko mkubwa (water Stress),” amesema na kuongeza kukosekana kwa rasilimali maji kwa baadhi ya watu kinaweza kuwa chanzo cha migogoro na machafuko katika jamii husika.
Ili kukabilikana na hali hiyo na kumwezesha kila Mtanzania kupata huduma za maji na usafi wa mazingira, Dkt. Biteko amezielekeza mamlaka za maji kupunguza kiwango cha upotevu maji ili kuepusha hasara ya shilingi bilioni 114.12 iliyotokana na upotevu huo kwa mwaka huu.
Hadi sasa asilimia 84 kwa mijini na asilimia 79.6 kwa maeneo ya vijijini zimeunganishwa na huduma ya maji ambapo kuna ongezeko la asilimia 7 kutoka kipindi cha mwaka uliotangulia.
Awali, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amesema kumekuwa na ongezeko la ubora wa viwango vya maji na udhibiti wa upotevu wa maji ambao unasababisha hasara kubwa hasa unapothamanishwa kifedha.
Hata hivyo ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri na kutoa taarifa inayoonesha uhalisia wa mambo huku akisema mamlaka zinazofanya vizuri zinapata tuzo ikiwa ni motisha ya ushindani wa kimaendeleo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele na kuongeza bajeti ambayo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 206 mwaka 2010/11 hadi shilingi bilioni 558 mwaka 2024/25
Amesema uwekezaji wa katika sekta ya maji unaleta faida zaidi ya mara saba ya mtaji ambapo uwekezaji wa dola 1 unaweza kuleta faida ya dola 7 katika Uchumi wa taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andelile amesema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa bado kuna changamoto kadhaa zinazotokana na utegemezi wa Mamlaka za maji kwa Serikali.
Pia amesema changamoto nyingine ni uchakavu wa miundombinu ya maji inayosababisha upotevu wa maji na hasara kwa serikali.
Mamlaka za maji zilizofanya vizuri katika udhibiti wa upotevu wa maji na asilimia ya maji yanayopotea ni Maganzo 4%, Nzega 6%, Kashuwasa 11%, Biharamulo 12% na Mwanuzi 13%.
Mamlaka zilizoshindwa kudhibiti upotevu huo kwa kiwango kikubwa ni Rombo 70%, Handeni 69%, Mugango/kyabakari 68%, Ifakara 56% na Kilindoni 55%.
Dkt. Biteko akiwa Mgeni rasmi ametoa tuzo na vyeti kwa mamlaka za maji zilizofanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mwisho.
WATUMISHI WA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPEWA MAFUNZO KUHUSU MATUMIZI YA MFUMO WA E-MREJESHO
habari Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ndugu Hassan Kilenza akitoa mada kuhusu Mwongozo wa ushughulikiaji wa mrejesho kwa wajumbe wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa mafunzo ya Mwongozo huo yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
![]() |
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndigu Hangi Chang’a akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
TUME KUONGEZA BVR VITUO VYENYE WATU WENGI DAR
habari
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa Mzambarauni Kata ya Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa Mzambarauni Kata ya Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Machi 18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katiuka siku ya pili.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo Machi 18, 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katika siku ya pili.



Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema itaongeza mashine za BVR na watendaji katika vituo ambavyo vimebainika kuwa na watu wengi ili kufanikisha uandikishaji na uborteshaji wa taarifa katika Daftari la Kudumu lka Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika siku ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati akikagua vituo Mkoani Dar es Salaam.
“Leo katika siku ya pili ya zoezi nimetembelea vituo vya uboreshaji na waliojitokeza wamekua wengi mmno kiasi kwamba vifaa vinaonekana ni vichache, nimeagiza vifaa kwamba viongezwe na vituo viongezwe ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Mhe. Jaji wa Rufani Mwambegele.
Jaji Mwambegele akiwa katika Kituo cha Lukooni Chanika Jijini Dar es Salaam alishuhudia uwepo wa wananchi wengi waliojitokeza kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandikisha na kutoa maagizo ya kuongezwa kwa mashine za BVR katika kituo hicho.
“Hapa Lukooni eneo la Chanika katika Wilaya ya Ilala kulikua na kituo kimoja katika siku ya kwanza, lakini baada ya kubaini kwamba watu wanakua ni wengi na wanatumia muda mrefu nikaagiza vifaa viongezwe na leo nimepita bado nimeona BVR mbili hazitoshi kwahiyo nimeagiza ziongezwe ili kuweza kukabiliana na changamoto hii,” aliongeza Jaji Mwambegele.
Aidha, Jaji Mwambegele amepongeza wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika siku za mwanzo za zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu kwani kufanya hivyo kunawezesha wao kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.
Nae afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Faraja Nakua amesema katika Majimbo matatu yaliyopo katika Halmashauriu ya Jiji la Dar es Salaam yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea zoezi linakwenda vyema na wao wamejipanga kufanikisha zoezi hilo.
“Nizidi kuwahamasisha wananchi wa Majimbo ya Ukonga, Ilala na Segerea Jijini Dar es Salaam kuendelea kujitokeza kwa wingi na sisi tumejipanga kutekeleza zoezi hili kama ambavyo Tume imeagiza na vifaa tulivyotakiwa kuongeza vipo tutavipeleka katika maeneo yote yenye changamoto,” alisema Nakua.
Nae Atness Shayo mkazi wa Ukonga Mzambarauni na Hassan Said Mmanga wa Chanika wamepongeza ujio wa zoezi hilo kwani walipoteza kadi zao za mpiga Kura na sasa wameoata kadi zao mpya zitakazoweawezesha kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataraji kuandikisha Wapiga Kura wapya 643,420 mkoani Dar es Salaam ambapo jumla ya vituo 1,757 vinatumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 96 katika vituo 1,661 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Aidha Tume imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa wanaandikishwa kwani BVR zaidi ya 5,000 na watendaji wa kutosha wapo kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 29. Kwa mujibu wa ratiba, leo Tume inaanza uboreshaji katika mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kailima amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura 4,071,337 idadi ambayo inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari linahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine.
Uboreshaji wa Daftari pia unahusu kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo.