Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

PROFESA MKENDA -SERIKALI IMEWEKA MSUKUMO KATIKA MASOMO YA SAYANSI

September 08, 2024 Add Comment








Serikali imeweka msukumo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.

Hayo yamesemwa hii leo tarehe 8.Sep. 2024  na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwenye  Marathon ya ERB (Bodi ya usajili wa Wahandisi Nchini)

Waziri Mkenda ameongeza kuwa Serikali imeanzisha Skolashipu kwa wanafunzi wa kidato cha sita watakao faulu vizuri zaidi masomo ya Sayansina kwenda chuo kikuu kusoma masomo ya Uhandisi, Tehama, Hisabati na Elimu tiba ambao kupitia ufadhili huo wanalipiwa gharama kwa asilimia mia moja huku lengo la Serikali ni kuchochea wanafunzi wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi.

Profesa Mkenda ameongeza kuwa hakuna Nchi Dunianj inayoendelea bila Sayansi ya Teknolojia hivyo Serikali itaendelea  kuongeza nguvu kwenye masomo ya Sayansi ili kupata wanafunzi waliobora kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.


Lengo la mbio za ERB ni kuwainua na kuwawezesha wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi na kuwezesha, Walimu wanaofundisha masomo ya Sayansi kwa Mkataba.


Huu ni msimu wa kwanza wa ERB Marathon na mbio hizi zitakuwa zinafanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa tisa huku wakimbiaji mia saba na kuendelea wakialikwa kushiriki mbio hizi.


Waziri Mkenda ameweka historia ya aina yake kwa kuweza kumaliza kilomita kumi jambo ambalo limewafurahisha wanariadha wengi zaidi.


Mbio hizo zilianzia katika uwanja wa UDASA kupitia Samu Nujoma, Makomgo juu na mwisho ni katika viwanja vya UDASA vilivyopo katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.

SERIKALI IMEPOKEA TAARIFA YA MWISHO YA UPEMBUZI YAKINIFU WA UJENZI WA CHUO MAHIRI CHA TEHAMA-DTI, DODOMA

September 05, 2024 Add Comment

 

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Dodoma

Serikali imepokea taarifa ya mwisho ya upembuzi yakinifu wa ujenzi Chuo Mahiri cha TEHAMA (Digital Technology Institute - DTI) katika eneo la NALA, Dodoma kutoka kwa Mshauri elekezi kutoka Muungano wa Chuo Kikuu cha Hanyang kinachojumuisha Chuo Kikuu cha Hanyang, Kampuni za Uhandisi na Usanifu Majengo za Yooil Engineering & Architects, na Moon Engineering.

Taarifa hiyo imepokelewa tarehe 05 Septemba, 2024 katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Washauri Elekezi hao kutoka Korea Kusini.

Akiongoza Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw. Nicholaus Mkapa amesema mradi huo unalenga kuimarisha mafunzo ya ujuzi na ubunifu katika TEHAMA, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidigitali nchini Tanzania. 
“Serikali inatarajia kuwa uwepo wa chuo hiki utapunguza uhaba wa wataalamu wa TEHAMA, hasa katika teknolojia zinazochipukia (emerging technologies), na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utaalamu na uvumbuzi wa kidigitali kwa ukanda wa Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Naibu Katibu Mkuu Mkapa.

Lengo la kikao hicho kilichofanyika tarehe 04 Septemba, 2024, lilikuwa ni kupokea na kujadili wasilisho la kukamilishwa kwa upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA, na kufungua fursa ya kuendelea na hatua muhimu za kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho.
Uanzishwaji wa Chuo hicho cha kisasa ni matokeo ya maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuimarisha utaalamu na kuandaa wataalamu wa TEHAMA nchini, hususan katika teknolojia zinazoibukia (emerging technologies). 

Ujenzi wa Chuo hicho pia ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo (2021-2026).

Akitoa wasilisho hilo lililojumuisha masuala muhimu yanayohusu elimu, mifumo ya TEHAMA, na usanifu wa majengo ya chuo, mbele ya uongozi wa Wizara, Meneja mradi wa mshauri elekezi huyo, Prof. Taejoon Park, ameshukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha upembuzi yakinifu na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa hatua zinazofuata.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Chuo hicho wizarani, Mhandisi Dkt. Seleman Daudi Arthur amesema mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa viwanda na ukuzaji wa ajira, hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Dr. Arthur amesema kukamilika kwa Ujenzi wa Chuo hicho Mahiri cha TEHAMA - DTI kutawezesha kuwa kitovu cha umahiri katika TEHAMA nchini, kikiwa na vifaa vya kisasa vya mafunzo na maabara za ubunifu katika maeneo ya teknolojia zinazoibukia, kama vile Roboti, Akili Mnemba (AI), Mtandao wa Vitu (IoT), Uchambuzi wa Takwimu (Data Analytics), na Usalama wa Mtandao. 

Vyuo Vikuu Vyote vya Afya na Sayansi Shirikishi Nchini Vyatakiwa Kutumia Mtaala Mmoja Wa Elimu

August 27, 2024 Add Comment

 


Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msofwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa  kongamano la mradi wa kufundisha wataalamu wa Afya (THET), ambapo mbali na mambo mengine wamejadili  kuanzishwa kwa Academy ambayo itatumika kuboresha mafunzo ya walimu wa vyuo vikuu katika sekta ya afya, kutengenezwa na kuanza kutumika kwa mitaala linganifu kwenye vyuo vikuu vya afya nchini na kutengenezwa kwa mfumo wa kuunganisha wahitimu wa afya nchini. Kongamano hilo imefanyika leo Agosti 26,2024 MUHAS Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Prof.  Apollinary Kamuhabwa akizungumza wakati wa kongamano la wa THET leo Agosti 26,2024 jijini Dar es Salaam.
Prof. Blanding Mbaga kutoka kutoka  Kilimanjaro Christian Medical University College,  akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mratibu wa mradi wa mapitio wa namna ya kufundisha wataalamu wa afya  (THET) Profesa Gideon Kusigabo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika leo Agosti 26,2024 katika chuo cha MUHAS Jijini Dar Es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imevielekeza vyuo vyote vya Afya na Sayansi Shirikishi nchini kutumia mtaala mmoja ili kuwa na watoa huduma wenye ujuzi na ubora unaolingana baada ya mtaala wa awali kuonekana kutotosheleza mahitaji.

Hayo yamesemwa leo Agosti 26,2024 jijini  Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msofwe wakati wa kongamano lililoandaliwa na Mradi wa THET.

Mradi huo wa mapitio wa namna ya kufundisha wataalamu wa afya (THET)  ulishirikisha vyuo vikuu vya Afya na Sayansi  Shirikishi vya Muhimbili (MUHAS), KCMC, Chuo cha Katoliki CUHAS, San Francisco na Chuo Kikuu cha Duke.

Ameeleza kuwa wadau walipendekeza kutumika kwa mbinu za kibunifu kwa ajili ya kuhakikisha elimu ya juu kwa upande wa vyuo vya Afya vinakuwa na ubora ili kuondoa mashaka kwa wagonjwa pindi wanapohudumiwa.

"Tuna Sera ya Elimu ya mwaka 2023 imebadilisha mitaala kwa ngazi zote kuanzia shule ya msingi hivyo nasisitiza vyuo vya Afya viwe na mtaala mmoja," alisema Profesa Msofwe.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Profesa Apollinary Kamuhabwa amesema kuwa mradi huo uliangalia namna wanavyowatahini madaktari wa binadamu na wauguzi.

Alisema kuwa mtaala huo utainua ubora na mafunzo ya elimu ya juu nchini kwa madaktari na wauguzi watakuwa na uelewa wa pamoja.

"Teknolojia imebadilika magonjwa yamekuwa mengi na watu wengi hupitia kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kwenda kuonana na daktari hivyo ni lazima wataalamu wa afya wajiandae na mabadiliko haya," amesema Profesa Kamuhabwa.

Naye, Mratibu wa THET Profesa Gideon Kusigabo amesema kuwa mtaala wa awali waliokuwa wanautumia haukuwa vizuri kwani walimu walikuwa wanashindwa jinsi ya kuandaa mafunzo kwa vitendo.

Pia amesema wanalenga kuhamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa ajili ya kutekeleza mtaala na kuongeza uwezo wa walimu wawe bora katika masuala ya afya.

"Tunalenga kuendeleza tafiti ndani ya ufundishji ili tuwe na walimu bora kwani walimu wengi wanaingia kufundisha lakini hawana viwango bora na athari zake ni kutoweza kutahini wauguzi na madaktari wazuri na kutoweza kufundisha vizuri," amesisitiza.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kwamba watoa huduma za afya hususan wahitimu wa udaktari na uuguzi kutokuwa na ubora unaotakiwa.

SERIKALI YATANGAZA NAMNA WALIMU WAPYA WATAKAVYOAJIRIWA

May 30, 2024 Add Comment


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo akiungumza  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed akizungumza 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza 
Meza kuu wakifuatilia 


Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI imetangaza mkakati wa uboreshaji wa elimu nchini huku ikieleza walimu ambao wataajiriwa ni wale wataokuwa wamefanya mitihani yao na kufaulu vizuri tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wizara ilikuwa ikijaza nafasi zilizokuwa zikihitajika bila kupitia mchakato huo .

Mkakati huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi

Alisema kwamba wanaoona jambo hilo sio jema kwao lakini wajiulize kwanini madaktari wanapomaliza Shahada ya kwanza wanalazimika kufanya mitihani ndio wanafanya kazi hivyo suala hilo linapelekwa kwa walimu ili kuweza kupata walimu bora.

Waziri Profesa Mkenda alisema kwamba wanaamini kigezo hicho ndio ambacho kitalivusha Taifa na watahakikisha wanachukua walimu waliobora zaidi na watakaofanya mitihani na kufaulu vizuri.

“Kama tunataka tuboresha elimu lazima twende kwa ujasiri tunapojaribu kuajiri walimu tujiulize tunapigania mwanao apata mwalimu bora sasa tutakapo ajiriw lazima wafanye mtihani na watakaofeli hawatapata nafasi”Alisema

Alisema lakini walimu waliopo watalindwa mpaka watakapostaafu na tutaendelea kuwajengea uwezo kwani Rais anatenga fedha nyingi kwenye elimu halafu tujitenge, haiwezekani lazima tathimini tunayoifanya lazima iendelee na hatua nzuri za baraza hatufurahii kufutia mitihani watahaniwa na waliojaribu kuiba mitihani”Alisema .

Aidha alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa Sheria mpya ambayo itawabana watu watakaobainika kuiba mitihani watakamatwa kushtakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi na kwenye hilo niwashukuru Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa kufanya kazi nzuri wanayoifanya.

“Katika jambo hilo tuzidi kuwa makini tusijikuta tukazubaa tukaanguka Necta msilegeze kamba nendeni kuhakikisha mnalisimamia na takwimu ni muhimu zitatueleza vizuri tunakwendaje na katika hilo tunataka kuimarisha takwimu za elimu Tanzania na kazi hii imeanza na timu ipo kazini”Alisema Waziri Profesa Mkenda

Awali akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo alilipongeza Baraza la Taifa Mitihani (Necta) kwa taarifa yao ya uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya ujifunzaji kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Alisema kwamba taarifa iliyowasilishwa inatoa picha halisi kuhusu na ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Sekondari na msingi nchini na mapendekezoo yaliyotolewa yanaonyesha dira ya nini cha kufanya ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji na tathimini katika ngazi ya shule unaimarika.

Alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wote wa elimu na baraza la mitihani kuhakikisha masuala yote ya ufundishaji na tahimini yanaimarishwa kwa lengo la kukuza umahiri wa wanafunzi katika masomo hayo.

“Vile Wizara kupitia Baraza la mitihani tutaendelea kuhakikisha kuwa tathimini ya ujifunzaji wa wanafunzi wa kidato cha pili awamu ya pili ya mwaka 2025 itafanyika kwa ufanisi mkubwa”Alisema

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed alisema suala la kufanya tathimini ni muhimu ili kuboresha kiwango cha elimu na wamekuwa wakifanya tathmini na mitihani na kueleza tahimini hiyo katika maeneo mbalimbali ni kutaka kujua maendeleo ya wanafunzi wamesoma na wanataka kufika wapi.

Alisema wamesema wameanza kufanya tathimini na masomo manne ambayo yameyafanya wakianzia na somo la kwanza ni Hisabati,Sayansi huku akieleza kwamba katika somo hilo katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu utakuwa hauna maswali ya kuchagua

Aidha alisema pia alisema hali ya ufauli nchini ukiangalia takwimu upimaji darasa la nne kwa miaka 10 uliopo ufaulu wa jumla umekuwa juu ya asilimia 80 itapanda kidogo na kushuka,miaka 10 hiyo utaona namna ya watahiniwa imekuwa ikiongezeka .

“Mfano mwaka 2015 darasa la nne laki tisa sasa kwenye usajili wanafikia mpaka 1,800,000 na ufaulu wameendelea kubakia 80 asilimia na namba ya watahiniwa imeongezeka mwaka hadi mwaka”Alisema

Katibu huyo alisema kwa upande wa Daraja la saba ulikuwa ni asilimia 67 mwaka 2015 na umeendelea kupanda na kufikia asilimia 80 mwaka 2023 kimahesabu huo ni ufaulu unaoafanana na bado wameendelea kufika asilimia 80 huku akieleza kwa upande wa Sekondari kidato cha pili ufaulu 2015 mpaka 2023 umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 67 2015 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka jana.


PAC YAIMIMINIA PONGEZI VETA KWA UJENZI BORA WA CHUO CHA VETA IKUNGI

March 30, 2024 Add Comment

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore akitoa maelezo kwa kamati ya bunge ya PAC wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ujenzi wa miundombinu wa Chuo ch VETA Ikungi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Ndombo akizungumza kwenye kamati ya PAC kwenye mradi wa VETA.


Baadhi ya picha ya wajumbe wa kamati ya PAC walipotembelea ujenzi wa VETA Ikungi

KAMATI  ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipa pongezi nyingi Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa ujenzi bora wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ikungi. Mradi huo ulitekelezwa na VETA kwa kutumia nguvukazi za ndani (Force Account).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baada ya kukagua chuo hicho, leo, tarehe 28 Machi 2024, wajumbe wa PAC wameonesha kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa majengo, miundombinu ya chuo na gharama za ujenzi zilizotumika, huku wakirejea na kuzungumzia tofauti na miradi mingine waliyoitembelea.


“Mmetutia moyo, tumetoka na moyo ulionyooka. Tulikuwa tumesononeka sana baada ya kutembelea miradi mingine iliyojengwa kwa utaratibu huu wa force account,” amesema Makamu Mwenyekiti wa PAC, ambaye pia ni Mbunge wa Vwawa, Mheshimiwa Japhet Hasunga.

Naye Mbunge wa Katavi na mjumbe wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ametumia muda mwingi kukagua majengo na miundombinu mbalimbali na kubaini kuwa kiwango cha ujenzi wa chuo hicho ni cha ubora wa hali ya juu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti (wa PAC), nimezunguka maeneo mengi, kwenye karakana, vyoo na madarasa, kazi hii ni nzuri sana. Kwa force account, kazi hii ni excellent (bora kabisa). Hata majengo yamejengwa kwa spacing (kuacha nafasi), jambo ambalo linasaidia hata kupunguza madhara inapotokea majanga kama moto,” amesema.

Wajumbe wa Kamati hiyo ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kutathmini thamani ya matumizi ya fedha za Serikali (Value for money), wamesema kuwa wameridhika kuona kuwa suala la thamani ya matumizi ya fedha limezingatiwa kwa kiasi kikubwa, hasa kwa kuangalia kiwango cha fedha kilichotumika na pamoja na chuo kuanza kudahili wanafunzi.

“Wakati naingia hapa, mimi nilistuka na kudhani kuwa wametumia pesa nyingi sana. Maana nikiangalia majengo yalivyojengwa kwa ubora, magrili kwenye milango na madirisha yalivyo mazito, nikadhani pesa nyingi sana itakuwa imetumika. Nilivyokuja kusikia taarifa kuwa imetumika shilingi 3 tu nimestaajabu sana. Ni kiwango kidoigo sana cha pesa ukilinganisha na majengo na miundombinu iliyojengwa. Hapa ndipo unaona value for money,” amesema Mheshimiwa Joseph Kakunda, Mbunge wa Sikonge na Mjumbe wa PAC.

Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chuo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema mradi huo wenye majengo 17 umetekelezwa na VETA kupitia chuo cha VETA Singida na ofisi ya VETA Kanda ya Kati katika hatua tofauti tofauti na kwamba utekelezaji wake umefikia asilimia 99.4.

“Majengo yote yamefikia asilimia 100 ya ujenzi, shughuli iliyobakia ni kuunganisha umeme (tail wire) kwa kila jengo kutoka kwenye nguzo za umeme zilizosambaza umeme katika eneo la chuo pamoja na kazi za nje,” amesema.

Amefafanua kuwa utekelezaji wa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi 3,004,013,405.56, ambapo fedha za ujenzi ni shilingi 2,653,915,038.00 na utengenezaji wa samani ni shilingi 350,098,367.56.