Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

BALOZI ADADI AWATAKA WANAFUNZI WA SHULE YA MUHEZA MUSLIM KUSOMA KWA BIDII

October 26, 2022 Add Comment
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akizungumza wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muheza Muslimu
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab  katikati akiwa na wadau wa maendeleo na wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari Muheza Muslim wakati wa maafali hayo


Na Oscar Assenga,MUHEZA

KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi katika shule ya Sekondari Muheza Muslim kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili wataalamu mbalimbali waweze kupatikana kupitia huko.


Balozi Adadi aliysema hayo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Muheza ambapo alisema lazima wanapokuwa shuleni waweze kujiandaa na  kuzingatia nidhamu ,malengo na kusoma vizuri ili baadae waje kufanikiwa kupitia elimu.

Alisema kwamba  mitihani inahitaji maandalizi mazuri ili waweze kufanya vema hivyo hawana budi kuhakikisha wanajiandaa ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao.

Katika Mahafali hayo Balozi Adadi aliendesha Harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule hiyo ambapo huku akihaidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanapata mafanikio.

Kamishna huyo aliuomba uingozi wa shule kwamba hiyo maabara utakapo kamilika ipewe jina la Bahoza Laboratory ili kuwaenzi kwa juhudi kubwa ambazo wamezifanya kufanikisha maabara hiyo.

Hata hiyo Balozi Adadi alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imefanya mambo makubwa na kuleta maendeleo huku akieleza fedha ambazo zinakuja zinatokana na kurudisha mahusiano ya na mataifa mengine ambayo yalikatika na ameyarudisha kwa kasi kubwa.

Alisema kutokana na kurejesha mahusiano hayo yamewasaidia kupata fedha nyingi za kujenga shule, maabara,barabara na kila Jimbo kuhakikisha maendeleo yanapatikana  ule ufufuaji wa mahusiano na  mataifa mengine.

Katika hatua nyengine Balozi Adadi aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kuhakikisha wana buni  mbinu zinazoweza kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono nchini.

Balozi Adadi alisema kwamba vitendo vya rushwa ya ngono vimekuwepo na  Takukuru wamepewa jukumu la kudhibiti  vitendo hivyo ni wakati sahihi kuhakikisha wanakuja na mwarobaini wake.

Alisema kwamba wao wanapaswa kuona namna nzuri ya kubuni mbinu ambazo zinaweza kupelekea 
 kudhibiti badala ya kusubiri matukio yanatokea ndio waweze kuanza kupambana nayo.

" Haya mambo yapo kwa sababu kwenye vyuo hivyo ni jinsi ya vyombo vilivyo kabidhiwa kufanya kazi hiyo wanafanya nini ili kuweza kuondokana na tatizo hilo"Alisema Balozi Adadi.

Aidha alisema kwamba wanataka wanaofanya vitendo hivyo wakamatwe ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo kuweza kubadilika hivyo suala hili lina umuhimu wake  hasa chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia.



WATUMISHI WA SERIKALI TANGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA NYONGEZA YA MSHAHARA,WASEMA AMEUPIGA MWINGI

August 05, 2022 Add Comment

 



Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja

 Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja



Mtumushi wa Jiji la Tanaga Mwanaidi Mashaka






Na Oscar Assenga,Tanga.

WATUMISHI wa Serikali Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 23 ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo ambalo miaka ya nyuma halikufanyika na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Tanga jambo ambalo amelifanya kwao ni kubwa mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.

Akizungumza mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka alisema wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo limefanyika.

“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii”Alisema

Naye kwa upande wake mtumishi mwengine Waziri Ally ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Elimu ya Msingi alisema wana mpongeza Rais kwa mengi aliyoyafanya kwa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23 imewagusa moja kwa moja wao kama watumishi.

Alisema asilimia 23 sio ndogo wanaweza kufanya jambo kubwa kama watumishi na wana morali wa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza malengo yaliyotarajiwa yanafikiwa.

“Kwa kweli ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara na ongezeko la watumishi sasa tumekuwa wengi na tunafanya kazi bila kuwepo kwa mzigo mkubwa”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake Stella Siang’a ambaye ni mtumishi wa Jiji Kada ya Elimu alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewafanyia mengi mno jambo la kwanza ni kuongeza wafanyakazi miaka mingi watu walikuwa hawajaajiriwa walikuwa mitaani iliyokwenda sambamba na ongezeko la mishahara ambalo litawawezesha kufanikisha majukumu yao.

Halikadhalika mtumishi mwengine Kasim Bashiru Lyimo kutoka Idara ya Elimu Sekondari alisema kwamba wanampongeza Rais Samia ameupiga mwingi kwa mambo mazuri aliyoyafanya kwa kuweza kuwaongezea asilimia 23 ya mshahara.

“Hili jambo sisi tumelifurahia sana na tupo pamoja na Rais na tuna hari ya kufanya kazi na atakapokuwepo mama na sisi tutakuwepo kuhakikisha tunamuunga mkono”Alisema

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Joshua Kiula alisema wana mpongeza Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuifungua nchi na inakwenda na imetulia .

Alisema pia amefanikiwa kufungua biashara zilikuwa zimefungwa na kurudisha na kuhuisha mahusiani na mataifa mengine ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha madaraja.

“Kwa kweli Rais Samia ameupiga mwingi kubwa ni kupandisha madaraja ambayo ni haki ya Msingi ya wafanyakazi na nyongeza ya mishahara jambo hilo ni nzuri na limewapa faraja kubwa kwetu”Alisema

Hata hivyo alisema nyongeza hiyo hawakuitegemea kama wataipata walidhani walipopandisha huo ndio ungekuwa mwisho lakini akaje na jambo lingine kwao la kuwaongezea asilimia 23 wamelipokea kwa moyo mkunjufu.

KITUO CHA SAYANSI CHA STEMP PARK CHA JIJINI TANGA KIMELETA MAGEUZI MAKUBWA

May 30, 2022 Add Comment

Meneja wa kituo cha Sayansi Maxi George akizungumza wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kilipoanzishwa
Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali


Na Oscar Assenga,TANGA

Kituo cha Sayansi cha Stemp Park kilichopo Jijini Tanga kimeleta Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya elimu ambapo kimeweza kuwa kichocheo kwa Wanafunzi kuhamasika kupenda kusoma Masomo ya Sayansi na kuongeza ubunifu.

Stemp Park ipo katika kata ya Kisosora na imeleta mapinduzi makubwa katika masomo ya Sayansi kwa Wanafunzi pamoja na Walimu.

Wanafunzi wanaotumia kituo hicho katika mambo ya Sayansi ni kianzia Chekechea hadi shule za Sekondari.

Akizungumza juzi katika wiki ya Sayansi Afrika Meneja wa kituo hicho Maxi George wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa Kwake iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya sayansi katika bara la Afrika

Ambapo alisema idadi kubwa ya ubunifu wa kisayansi katika jiji la Tanga umekuwa mkubwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakienda kituo hicho na kufanya shughuli zao za ubunifu ambapo wanafanya wa nadharia zaidi.

"Hapa vijana wanapata nafasi ya kuelezwa umuhimu wa Sayansi katika maisha ya kawaida,na katika maisha ya shule kwa kujifinza mambo mbalimbali ya sayansi kwa vitendo na kwa kuona"alisema George

Katika hatua nyingine kituo hicho pia kinawanufaisha walimu wa mkoa wa Tanga kwa kuwapa ujuzi katika kuwafundisha wanafunzi shuleni

"Walimu wanaprogram maalum ambayo inaitwa TOT hii imekuwa chachu ya kuwapa ujuzi katika kuwafundisha vijana,lengo likiwa ni kuchagiza ufaulu kwa masomo ya sayansi"alisema George

Pia aliwaasa wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wajifunze masomo ya Sayansi kuwa sio ngumu bali watu waliaminiashwa kuwa ni ngumu

"Tunatoa wito kwa Wazazi,kuwaachia watoto wajifunze zaidi,pale mtoto anapofanya jambo la ubunifu mzazi amwache akifanye ili apate njia sahihi ya kutengeneza kitu anachokitaka ambacho badae kinaweza kuwa na manufaa"alisema George

Aidha Wanafunzi wanaoenda kwenda kujifunza katika kituo hicho wameeleza kuwa kituo hicho kimewajenga zaidi kwa kuwa wabinifu.

Mmoja wa wanafunzi wa kike Rukia Omari wa Masechu Sekondari anayenda kupata elimu ya Sayansi katika kituo hicho alisema wao wanakabiliwa na changamoto pindi wanapotaka nafasi ya kwenda kujifunza katika kituo hicho kwa kuwa wazazi wanawabana kupatamuda wa ziada ya kujifunza Sayansi

"Mazingira tunayoishi inatufanya wasichana tusiwesawa na wavulana katika kujifunza,ukiomba ruhusa kwenda kujifunza huwezi kupewa,utaambiwa bora umsaidie Mama kazi hivyo kufanya mua wa kusoma usiwepo lakini kwa wanaume iko tofauti akirudi hana kazi"alisema