TAMASHA LA KIZIMKAZI KUFUNGUA FURSA KIUCHUMI

August 12, 2026




NA MWANDISHI WETU- ZANZIBAR


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga ameshiriki katika uzinduzi wa Viwanja vya Kufurahisha Watoto vya Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 12 Agosti, 2026 vilivyozinduliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 


Uzinduzi huo ni miongoni mwa matukio yatakayofanyika wakati wa  Tamasha la Kizimkazi 20226 linalofanyika wa siku tatu Kuanzia Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.

Katika tamasha hilo ambalo limejizoelea umaarufu mkubwa pia kutakuwa maonyesho, burudani na programu mbalimbali za kuvutia zinazolenga kutangaza utalii, uwekezaji na utamaduni wa Kizimkazi.

Kizimkazi Festival ni tamasha la wananchi wa Kizimkazi. Dhamira yake ni kuitangaza Kizimkazi kama eneo lenye historia, utamaduni, vivutio vya utalii na fursa nyingi za uwekezaji kwa manufaa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla.

Aidha malengo ya Tamasha la Kizimkazi ni kutangaza fursa za uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii pamoja na kuhifadhi na kuenzi utamaduni wa Kizimkazi.

Wakati kwa upande wa fursa za uwekezaji ni Utalii na hoteli, Uchumi wa Buluu, Uvuvi, Biashara na huduma mbalimbali, pamoja na miradi mingine ya mandeleo.


Miradi itakayozinduliwa wakati wa tamasha la Kizimkazi ni uzinduzi wa mradi wa maji Kizimkazi, uzinduzi wa kiwanja cha watoto KibuTeni,ufunguzi wa nyumba za kuishi Bopar Enterprises, Jiwe la msingi Salaam Cane Restaurant-K/Dimbani.


Miradi mingine itakayozinduliwa ni mradi wa mabweni mapya -Hasnu Makame Sekondari-Kibuteni ,jiwe la msingi jengo la maendeleo Kibuteni na uzinduzi wa hoteli la kitalii ya Johari-K Mkunguni.


Kauli mbiu”KIZIMKAZI Kumenoga”

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »