TUZINGATIE MATUMIZI YA RASILIMALI ZETU KATIKA KUTEKELEZA MPANGO WA KUZALISHA UMEME WA NYUKLIA NCHINI -PROF. NAJAT

December 19, 2025


📌Lengo ni kuhakikisha Mpango huu unatekelezwa na Wataalamu wazawa


📌Wananchi watakiwa kushirikishwa katika Mpango huo


📌Ni Mwelekeo wa Serikali katika Kukidhi Mahitaji ya Umeme Ifikapo 2030


Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Prof. Najat Mohammed amewataka wajumbe wa Kamati tendaji ya uratibu  Mpango wa uzalishaji umeme wa Nyuklia l kuhakikisha wanaanza maandalizi mapema ya namna mpango huo utakavyotekelezwa Nchini huku akiwasisitiza kuhakikisha wanazingatia matumizi ya rasilimali zinazopatikana Nchini Tanzania katika utekelezaji wa mpango huo.

Hayo ameyabainisha Disemba 19,2025 wakati akifungua kikao cha Kwanza cha Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa kuzalisha umeme kwa kutumia Nishati ya Nyuklia (NEPIO) kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati, Mtumba Jijini Dodoma.


Akifungua kikao hicho Prof. Najat Mohammed ameitaka kamati hiyo kuhakikisha wanaanza maandalizi mapema ili kukamilisha mpango huu ndani ya miaka saba

“Matayarisho ya Mpango huu yanachukua miaka 10 lakini sisi tunataka tuende miaka saba ili kupata umeme huu kwa muda mfupi zaidi hivyo niwatake muanze maandalizi mapema ili mfanye utafiti wa rasilimali zitakazotumika ili kama rasilimali hizo zinapatikana hapa nchini zitumike rasilimali zetu.”Amesisitiza Prof. Najat.

Amesema kuwa kuwepo na mnyororo wa ugavi(supply chain) thabiti na endelevu katika mpango wa kuzalisha umeme wa nyuklia nchini kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, na wadau wa kimataifa. 

“Katika kutekeleza Mpango huu tuhakikishe upatikanaji wa vifaa, teknolojia, na malighafi muhimu kwa wakati unaofaa, pamoja na kujenga uwezo wa ndani wataalamu kupitia mafunzo mbalimbali lakini pia kuhakikisha tunapoalikwa kushiriki mikutano na warsha mbalimbali za masuala ya Nyuklia tunashiriki kikamilifu ili kujifunza zaidi”. Amesisitiza Prof. Mohammed.

Aidha, ameitaka Kamati hiyo kuhakikisha wananchi wanashirikiahwa katika mpango huu ili kuzingatia mifumo madhubuti ya usimamizi wa hatari, viwango vya usalama, na sera rafiki za kisheria kwani wananchi wakishirikishwa na kupewa elimu mpango huu utatekekezwa kwa ufanisi, gharama nafuu na kwa kuzingatia ulinzi wa mazingira pamoja na maendeleo endelevu ya kiuchumi.


Awali akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mpango wa Nishati ya Nyuklia(NEPIO) Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Wizara ya Mishati Mha. Innocent Luoga ameeleza kuwa kulingana na taratibu za Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu(IAEA) ambapo Tanzania ni mwananchama Nchi zinazotarajiwa kuzalisha umeme wa nyuklia ni lazima kuwa na kamati hiyo hivyo Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na TAEC pamoja na Wizara ya Maji, Nishati na Madini - Zanzibar, TANESCO, ZECO, EWURA, NEMC na ZURA zimekua zikishiriki katika maandalizi ya mpango huu kwa kuzingatia uzoefu na umuhimu wa Taasisi hizo katika kutekeleza mpango huo.


“ Nishati ya Umeme ni muhimu katika maendeleo ya nchi yetu na dunia kwa ujumla hivyo kutokana na ongezeko la shughuli za kiuchumi na maendeleo mengine mahitaji ya umeme yanakadiriwa kufikiwa Megawati elfu 8,000 ifikapo mwaka 2030 kutoka Megawati 4,352.13 za sasa hivyo kutokana na ongezeko Rais wa Jamuhuri   ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan alielekeza kuhakikisha azma hii inatekelezwa ili kuhakikisha tunakua na umeme wa kutosha na kuondokana na mgao wa umeme.”Ameeleza Mha. Luoga.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »