Naibu Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Kinyasi Millya (Mb) na Mhe. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb) wanekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ajili ya kutambulisha baada ya kuteuliwa kushika nyadhifa hizo hivi karibuni.
Utambulisho huo umefanyika katika Ikulu ya Zanzibar Desemba 19, 2025 ambapo Dkt. Nwinyi aliwapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa kushika nyadhifa hizo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Rais Mwinyi alitoa maelekezo na miongozo mahususi inayohusu upande wa Zanzibar kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ni moja ya Wizara za Muungano.
Aliwataka Naibu Mawaziri hao kufanya kazi kwa bidii, huku wakitambua umoja wa Serikali ya Tanzania kwa kuchangamkia fursa zinazogusa pande zote za muungano katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Diplomasia ya Uchumi, Utalii na Uwekezaji.
Utambulisho ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mhe. Dkt Saada S. Mkuya; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, na Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.









EmoticonEmoticon