HAYAWI HAYAWI PUNDE YATAKUWA

December 20, 2025


*Macho na masikio tuyaelekeze ndani ya Hifadhi ya Taifa ya tano kwa ukubwa Tanzania.*


Tukio lililosubiriwa kwa hamu na bashasha tele la uzinduzi wa Kampeni yetu ya *“Shangwe la Sikukuu na TANAPA”* msimu wa pili linazinduliwa rasmi leo Desemba 20, 2025 ndani ya Hifadhi ya Taifa Katavi iliyopo mkoani Katavi.

Shangwe hilo mbali na uzinduzi rasmi pia litajumuisha utalii wa ndani wa kutembelea vivutio vya utalii, burudani kedekede na milindimo ya Wagongwe na wabembe sanjali na nyamachoma usiku!

Hii ni kali ya kufungia mwaka 2025 na kufungulia mwaka 2026. Ni ruksa kuja na umpendaye.

*“Asiye na mwana aeleke jiwe”.*


*Tukutane tambarare ya Katsunga ndani ya Hifadhi ya Taifa Katavi*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »