Na. Mwandishi Wetu
Uwepo wa mawakala wa vyama vya siasa wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni kielelezo cha uwazi na ni muhimu kwa kuwa mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akijadili jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani (kulia) wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyoanza leo Machi 06,2025 na yanataraji kumalizika kesho Machi 07, 2025 na kufanyika Ubungo mkoani Dar es salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Christophrer Anania akiwasilisha mada ya uraia.
Washiriki wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo hayo.
Washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo hayo ya siku mbili ikiwa ni maandaliazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon