SERIKALI ,WADAU WAJIKIYA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATOTO WA KIKE NCHINI .

October 04, 2024

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Amon Mpanju amesema Serikali,kupitia wizara za kisekta kwa kushirikiana na wadau wamejikita kuhakikisha wanalenga kutatua changamoto zinazowakabili watoto wa kike nchini,ambazo zinatokana na kiwango kikubwa na mifarakano na migogoro kwa ngazi ya familia.

Ameyasema hayo Octoba 3,2024  jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya siku ya mtoto wakike duniani inayotarajia kufanyika wilayani Bahi Mkoani Dodoma,Oktoba 11,2024 alisema migogoro hiyo ya ngazi ya familia inapelekea kuwa na malezi duni na uangalizi hafifu kwa watoto hususan watoto wa kike.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa hali ya Afya ya uzazi na mtoto pamoja na viashiria vya maralia ya mwaka 2022 ilihainisha kwamba changamoto zinazowakabili watoto zimechangiwa kwa kiwango kikubwa na mifarakano na kutoelewana kwa ngazi ya familia na kupelekea malezi duni kwa watoto na kuwa katika uhatarishi huku wengine kuanza kufanya vitendo vya ngono mapema kabla ya umri halisi.

Mpanju amesema kwa mujibu wa taarifa hiyo inaonesha kwamba watoto wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 takribani asilimia 22 walipata mimba za utotoni ukilinganisha na asilimia 27 kwa mwaka 2015/16 utafiti wa namna hiyo ulipofanyika.

“Kwa mujibu wa utafiti huo ,inaonesha hali ya mimba vijijini kwa watoto ni asilimia 25 ukilinganisha na asilimia 16 kwa watoto wa mijini,watoto wetu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo vitendo vya ubakaji ,ulawiti na mimba na ndoa za utotoni,”amesema na kuongeza

“Kwa mujibu wa taarifa ya makosa ya ukatili wakijinsia na unyanyasaji ya Jeshi la Polisi kuanzia January hadi Disemba 2023 inaonesha matukio ya ukatili wa watoto yalikuwa 153001 ukilinganisha na matukio ya vitendo vya ukatili vya watoto kwa kipindi hicho kwa mwaka 2022 ambayo yalikuwa 12,163 na kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi yenye matukio makubwa ya ukatili dhidi ya watoto mkoa wa kwanza Arshad, Morogoro,Tanga,Kinondoni pamoja na mjini maghharibi,”amesema Mpanju.

Amesema kwa upande wa matukio ya hali ya mimba za utotoni ni pamoja na mkoa wa Songwe asilimia 45,Ruvuma asilimia 37 ,Katavi 34,Mara 31 na Rukwa asilimia 30 kwa hali hii inaonesha matukio ya vitendo vya ukatili vinaendelea kuongezeka kwa watoto na hivyo kuna umuhimu wa jamii kuhakikisha wanaweka mifumo na kutimiza wajibu wetu wa kuwalinda watoto hususan watoto wa kike.

“Kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi matukio yaliyoongoza kwa wingi katika ukatili wa watoto ni matukio ya ubakaji ambapo ni 8185,matukio ya ulawiti ni 2382 na matukio ya mimba kwa wanafunzi 1437 na mengine yanafutwa,”amesema na kuongeza

“Sisi kupitia Serikali maadhimisho ya mwaka huu ambayo kilele chake kitakuwa October 11,2024 Dodoma ,tumejikita kuhakikisha kauli mbiu isemayo “Mtoto wa Kike na Uongozi tumshirikishe,wakati ni sasa” inatekelezwa kwa ngazi zote na kuhakikisha mtoto analindwa Serikali kwa kushirikiana wizara za kisekta wameanzisha majukwaa maalum mahususi yanayohimiza ulinzi wa watoto na ushiriki wa watoto wa kike katika kuwa viongozi wa kisasa,”amesema Mpanju.

Kwa upande wake Mwanafunzi Kutoka Chuo cha National Institute of Transport na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wasichana kutoka Msichana Initiative,Letisia Mswaki amesema wasichana wanapata changamoto mbalimbali na kuona haki za msingi hawazipati na namna ya upatikanaji wake.

“Wasichana 200 kutoka mikoa mbalimbali walishiriki katika utafiti wa kuona namna wasichana wanavyopitia changamoto mbalimbali katika maeneo yao,lengo likiwa kuona utekelezaji wa agenda ya msichana kama imefanikiwa na kuona ni jinsi gani msichana anaweza kufanikiwa na agenda hiyo ya masuala ya uongozi na sasa Sheria zinamlindaje huyu msichana ili aweze kufikia malengo yake ya kusimama kama kiongozi,”amesema.

Naye Successfully Ufahama Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Godwin Gondwe kidato cha kwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Flaviana Matata Foundation amesema vijijini wasichana wengine wanakosa elimu kwa sababu ya umbali wa maeneo waliyopo inapelekea kukosa elimu ya kujikinga na masuala ya ukatili ili kusaidia waweze kuepukana na changamoto.

Anaoomba Serikali kufanyia kazi msaada huo ambayo tayari umepitishwa ili kuwa kuokoa wasichana waliyopo mijini au vijijini ambayo wanateswa na kitendo cha ukatili wanachofanyiwa kila siku cha kuozeshwa wakiwa na umri mdogo.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »