DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Hussein Abbas Tayebji
Na Oscar Assenga, Tanga
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Hussein Abbas Tayebji amewashauri wananchi wanapopata shida ya macho wasikimbilie kwenye duka la kununua dawa badala yake wafike hospitalini wachekiwe wanashida gani na watapewa dawa sahihi au miwani.
Dkt Hussein aliyasema hayo leo wakati akielezea matatizo macho ambapo alisema kwamba wagonjwa wanaowapokea kati yao wanawatibu na kutoa ushauri ikiwemo kuwaeleza umuhimu wa kujenga utaratibu wa kucheki macho yao angalau mara moja kwa mwezi.
Alisema kwa sababu dawa nyengine zinaweza kuwaletea shida wakiweke ovyo ovyo kwenye macho ni sumu kwenye macho hivyo iwapo wanakumbana na matatizo ya macho ni vema wakafika hospitalini wachekiwe wanashida gani na watapewa kupewa dawa sahihi.
“Ni muhimu sana kwa wananchi wanapopata tatizo la macho wafike Hospitalini wachekiwe wanashida gani na watapewa dawa sahihi au miwani kama unashida ya miwani kwani sio kila shida ya macho ni miwani”Alisema Dkt Hussein
Dkt Hussein alisema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa mwezi wanawaona wagonjwa zaidi ya 600 wenye matatizo mbalimbali ya macho.
Alisema katika magonjya ya macho kuna matatizo mengi sana na kati yao wanatibu wanatoa ushauri,kupima miwani na upasuaji wa aina zote mtoto wa jicho ikiwemo kuondoka kinyama cha macho
“Kwa wagonjwa tunaowaona wana presha ya macho sana ndio wanapata kwa sababu haina dalili zozote ukija Hospitali unakuwa umeshachelewa ni vema wananchi waweke utaratibu wa kuchungyza macho yao kila wakati ili kuweza kuepukana na matatizo ya macho ikiwemo mtoto wa jicho”Alisema
EmoticonEmoticon