WANAFUNZI 250 WAPATA MAFUNZO YA GIRL GUIDES TEMEKE

November 11, 2017
 Baadhi ya  Girl Guides ambao ni wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Manispaa ya Temeke wakionesha moja ya alama muhimu za Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), baada ya kupata mafunzo ya awali  katika Shule ya Msingi Mbagala, Dar es Salaam leo. Wanafunzi wa kike 250 walishiriki mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke,  Leonida Komba ( wa tatu kushoto waliosimama)

Girl Guides hao walipata mafunzo kuhusu historia ya Girl Guides duniani, kanuni, malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Pia hufundishwa ujasiri, ukakamavu, mambo ya uongozi, maadili, kujitolea pamoja na uzalendo.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (kushoto) akiwahamasisha Girl Guides wakati wa mafunzo hayo




 Girl Guides wakiwa na furaha baada ya kupata mafunzo ya chama hicho kuhusu kanuni, historia ya Girl Guides Duniani, malengo na madhumuni yake.
Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (wa pili kulia waliosimama) akiwa na walimu ambao ni walezi wa Girl Guides wa shule walikotoka wanafunzi hao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »