Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la
Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya
kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama
Janeth Magufuli wakifurahia ngoma ya asili iliyokuwa ikipigwa na watoto
wa nchini Uganda katika eneo la mpakani la Mutukula kabla ya kurejea
nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
mpakani Mutukula upande wa Tanzania mara baada ya kuwasili akitokea
Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Mpakani mwa Tanzania na Uganda (Mutukula) kuhusu ujenzi wa barabara ya
Kutoka Miziro hadi Mutukula bila kupitia wilayani Misenyi. Pembeni yake
ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
akisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wakuu
wa Majeshi ya Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa
mpakani Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya
siku tau nchini Uganda.
PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon