KUSHIRIKI SHEREHE ZA NANENANE NI DARASA MUHIMU KWA WAKULIMA

August 05, 2017

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akiwasili katika banda la wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi wa Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi wa Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi


Na Mathias Canal, Lindi
  
Wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wameombwa kushiriki kwa wingi katika Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yanayofanyika kwa siku 8 katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho.

Mhe Wangabo alisema kuwa Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini hivyo wananchi kushiriki kwao kutawahakikishia elimu mbadala ya kilimo chenye tija kwao na Taifa kwa ujumla.

Maonesho hayo yanabebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati" ikiwa imedhamiria kwa kiasi kikubwa kumkwamua mwananchi na mkulima wa kawaida kuondokana na uduni wa mazao wakati wa mavuno.

Katika Maonesho hayo Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo wanatekeleza jukumu kubwa la kuwaelimisha wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

Teknolojia/Bidhaa zinazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

Hivyo kwa wingi wao wananchi waishio Kanda ya kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanapaswa kutumia fursa hii ambayo inatokea katika kipindi kimoja pekee katika kila mwaka.
Mhe Wangabo alisema kuwa Tatizo kubwa linalokabili sekta ya kilimo na ufugaji nchini kutozingatia kanuni bora na za kisasa za kilimo na Ufugaji. Nimefurahishwa sana kuona kwamba katika maonyesho haya kuna Taasisi za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa.

Alisema kuwa zipo changamoto zinazokabili sekta ya kilimo na mifugo nchini ikiwa ni pamoja na ukame, upungufu wa madawa ya mifugo, uchache wa maafisa mifugo, upungufu wa majosho, uvuvi haramu na miundombinu duni ya kusafirisha mazao ya mifugo.

Hata hivyo Serikali itaendelea kutatua changamoto hizo kwa kuongeza maafisa  ugani ili wawawezeshe wakulima kuzingatia kanuni za kilimo na ufugaji bora; kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji, kuvuna maji ya mvua, kuchimba malambo, kuongeza majosho, kuongeza madawa ya mifugo na kuhamasisha wakulima na wafugaji kutumia zana bora za kilimo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »