Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi muungano na Mazingira
Mheshimiwa Luhaga Mpina, amewataka wakazi wa Mkoa wa Morogoro kutunza
Vyanzo vya maji na Mazingira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameokoa
maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.
Naibu Waziri
Mpina ameyasema hayo leo alipikuwa katika zoezi la usafi kitaifa Mjini
Morogoro ambapo amesisitiza kwa kufanya hivyo wakazi wa mkoa huo
watakuwa wamesaidia wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam Pamoja na pwani
ambao vyanzo vyao vyingi vya maji vimetokea mkoani Morogoro.
Kulia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwna Kebwe Steven Kebwe
akimkabirisha Naibu Waziri Mpina kabla a kuanza kwa zoezi la Usafi
kitaifa Mjini Morogoro siku ya Jumamosi ya Mwisho wa mwezi wa nne.
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina akitoa Mchanga katika moja ya Mtaro Mijini Morogoro wakati wa
kufanya usafi, Leo.
Moja ya Mtaro Uliosafishwa katika zoezi la usafi wa mazingira leo Mjini Morogoro |
Mpina
pia aliweka msisitizo katika zoezi zima la upandaji miti ambapo kila
wilaya inatakiwa kupanda miti milioni moja na nusu, "kutakuwa na
ufuatiliaji wa hali ya katika utekelezaji wa zoezi hiyo katika ngazi ya
Wilaya." Alisisitiza Mpina.
Aidha Mpina aliunga Mkono
Jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika suala zima la utunzani na
usafi wa mazingira , "Mnae Mkuu wa Mkoa anaetosha, anaujua mkoa vizuri
na hwa ndiyo viongozi wa mkoa tunaowataka, wachapakazi na wenyekujituma.
Alisema Mpina."
Akiongelea suala la kuhamishwa
wananchi katika milima na vyanzo vya maji, NW Mpina Alisema kuwa "
Tunapowaondoa wananchi katika maeneo hayo aimaaninishi kwamba
tunawatesa. tunawapenda ndo maana tunawahamishia katika maeneo salama na
rafiki kwa mazingira, RC watoeni wananchi wanaokaa katika maweneo
Hatarishi." Alisema.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Bwana Kebwe Steven Kebwe, akizungumzia hali ya mazingira ya
mkoa huo, alisema kuwa mkoa utajitahidi kupambana na hali ya uharibifu
wa mazingira, pamoja na changamoto mkoa unazokumbana nazo akitolea mfano
upungu wa vifaa vya kuzolea taka.
Jumamosi
ya usafi wa Mazingira Mkoani Morogoro kwa Jumamosi ya Mwishho wa mwezi
wa nne ni utegelezaji wa Agizo la Mhe. Rais la Usafi wa Mazingira.
EmoticonEmoticon