Mkuu
wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi
wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili
kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa Viongozi wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Uvuvi
na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu kutoka Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za wananchi wa vijiji
viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha mradi mkubwa wa
Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.
Mradi
wa bwawa la Farkwa ni mradi mkubwa ambao huenda ukawa ni mkubwa katika
Ujenzi wa mabwawa makubwa kuliko yote barani Afrika. Mradi huu
uliasisiwa na baba wa Taifa tangu mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya za
Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma Manispaa na utegemea kutumia pesa za
Tanzania zaidi ya Tilioni 2.
Kufuatia
umuhimu wa mradi huu na uwijio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma,
serikali imezamilia ifikapo mei mwaka huu zoezi la Uthamini wa mali za
wananchi wanaohama kupisha mradi huu mkubwa katika Vijijini vya Mombose
na Bubutole vilivyopo Wilayani Chemba pamoja na vijiji vinavyopitiwa na
njia Kuu ya bomba linalopeleka Maji eneo la Kilimani mjini Dodoma liwe
limekamilika tayari kwa kuwalipa wananchi ili Ujenzi wa bwawa uanze.
Ujenzi
wa mradi huu unategemea kuchukua miaka mitatu 2017-2021 mpaka
kukamilika kwake. Hivyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa
Wataalamu wa uthamini kwa kuwa wameusubiri mradi huu kwa zaidi ya miaka
47 na leo serikali imepata fedha ya kuutekeleza.
Mhe
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Odunga wamewataka wananchi hao
kujiepusha na watu wasiopenda maendeleo yao na nchi yetu kwa ujumla wa
anaopita pita huko na kujifanya watetezi wa haki za wananchi. Swali hao
watetezi walikuwa wapi tangu 1970 waje leo ambapo mradi unaanza
kutekelezwa.?
Aidha,
amesisitiza wananchi ambao ni wamiliki halali wa maeneo husika ndio
wajitokeze kwenye uthamini huo ili kuepusha udanganyifu na migogoro
isiyo ya lazima wakati wa malipo yatakopoanza. Kwani kuna baadhi ya
wananchi zi waaminifu na atakayefanya hivyo akibaini sheria kali dhidi
yake zitachukua mkondo.
Kwa
upande wa Wataalamu Mkuu huyo wa Wilaya amewataka kutumia akili, uweledi
na taaluma zao katika kuhakikisha kila mwananchi wa maeneo hayo anapata
haki yake stahiki kwa mujibu wa sheria za uthamini.
Katika
Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mhe Rajabu
Muheshimwa ameongea kwa kupongeza juhudi za Serikali kwa kuamua kuanza
mradi huu na zaidi kusihi wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalamu, hali
kadhalika Mhe Diwani wa Kata ya Farkwa Ndugu, Suleiman Gawa amesisitiza
kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu pia Wataalamu wahakikishe
wanaorodhesha mali zote za wananchi zinazotambulika kisheria ili
kuepusha migongano hapo baadae.
Naye
Katibu Tawala wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji na vitongoji
kusimamia zoezi hili kikamilifu kwani wao ndio wanaowafahamu wananchi
wao pia watoto ambao wanamiliki mali lakini hawatambuliwi kisheria
kutokana na umri wao.
EmoticonEmoticon