Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija (Kushoto) ambaye kachaguliwa kuwa katibu wa Wakurugenzi nchini
Na Mathias Canal, Dodoma
Wakurugenzi
wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kote nchini kwa kauli moja
wameridhia na kuwachagua viongozi watakaowawakilisha katika kufikisha
changamoto zao mbalimbali katika ngazi za juu ili kupungunza
uwasilishaji wa kila Mkurugenzi kufikisha changamoto zake ngazi za juu.
Uchaguzi
huo umefanyika hii Leo katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma kwa
maridhiano ya Wakurugenzi wote kwa asilimia 100% ya kura zote.
Uchaguzi
huo umejili Mara baada ya kumalizika kikao cha kazi kilichoongozwa na
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa
(TAMISEMI) Eng Musa Iyombe kilichohudhuriwa na Wakurugenzi wote 185.
Wakurugenzi
hao wamefanya uchaguzi kwa nafasi nne ambazo ni Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti sambamba na Katibu pamoja na Muweka Hazina.
Wakurugenzi waliochaguliwa katika nafasi hizo ni
1. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti
2. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndg Rachel Chuwa ambaye kachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
3. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija, ambaye kachaguliwa kuwa katibu. Na
4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA
Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika Viongozi hao
waliochaguliwa wameeleza namna bora ya kuhumiza uwajibikaji kwa
Wakurugenzi wote sambamba na kuwawakilisha vyema kufikisha changamoto
zao kwa ngazi za juu.
Wameueleza mtandao wa www.wazo-huru.blogspotm.com kuwa
imani kubwa waliyopatiwa na Wakurugenzi wote nchini ya kuwachagua kuwa
wawakilishi wao ni kubwa hivyo wana kila sababu ya kuitumikia kwa weledi
na usawa.
"Kupitia
Wawakilishi hao waliochaguliwa Wakurugenzi nchini wataraji utendaji
uliotukuka na uwakilishi unaostahili kulingana na changamoto
zinazowakabili katika maeneo yao" Alisema MD Kayombo John L.
EmoticonEmoticon