Benki ya NMB, Mastercard yawaingiza wakulima kidijitali

March 10, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) pamoja na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra wakisaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali. Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra (wa pili kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali.

 Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin.

 BENKI ya NMB imesaini makubaliano na Kampuni ya Mastercard kufanya kazi kiushirikiano ili kuhakikisha inaiinua sekta ya kilimo nchini Tanzania kwa kuanzishwa kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu waliokuwa wakiupata wakulima hapo awali.

 Huduma hiyo ya 'eKilimo’, ni jukwaa la kidigitali ambalo litamsaidia mkulima kupata uwazi na usalama wa bidhaa zake kimasoko na hata urahisi wa upatikanaji taarifa, huku ukiondoa urasimu uliokuwa ukifanywa na madalali sokoni, jambo ambalo wakulima wengi wamejikuta wakishindwa kunufaika kiufasaa kwa bidhaa zao. 

Ushirikiano huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Raghu Malhotra, ambapo kwa pamoja wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema huduma hiyo itawainua wakulima kwa kiasi kikubwa endapo itatumiwa na wakulima. 

Kwa upande wake, Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra, alisema kupitia huduma hiyo mkulima anaweza kufanya mauzo na kulipwa kwa kutumia simu iliyo na programu maalum huku benki ikipata taarifa, jambo ambalo litamrahisishia shughuli zake na kuokoa muda mwingi wa kuzunguka.

 Alisema takwimu zinaonesha kilimo kinachangia kiasi kikubwa cha fedha katika pato la taifa 'GDP', ambapo takribani shilingi bilioni 13.9 ikiwa ni takribani asilimia 30, hivyo kuna kila sababu ya kuinua sekta hiyo ili iendelee kufanya vizuri na pia kuwainua wakulima.

 "Kwa kutumia teknolojia ya kidigitali huduma hii italeta uwazi kwenye mchakato wa mauzo na ununuzi na kuongeza ufanisi katika eneo la ugavi, hivyo kuleta manufaa ya kiuchumi.

Teknolojia inapaswa kusaidia wakulima kupata ufumbuzi kwa huduma za kifedha, hivyo kuwawezesha kuwa na maisha bora na familia zao hata baadae," alisema Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra. 

Akizungumzia huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema lengo kubwa ni kumuwezesha mkulima kunufaika zaidi na kilimo anachokifanya, huku benki ikiendelea kujenga mazingira ya mteja kupata huduma bora na kuaminika ili aendelee kupata mikopo kwa shughuli za kilimo. 

Alisema mkulima anapokuwa na uhakika wa kupata taarifa sahihi za masoko na kuweza kufanya mchakato mzima pasipo na urasimu hunufaika zaidi na kuendelea kuaminika kwa taarifa zake benki jamboa ambalo ananufaika moja kwa moja kupata mikopo ya kilimo, ambayo humuongezea tija.
 "Nia yetu sisi ni kukua sekta ya kilimo Tanzania, na ndio maana tumeshirikiana na Mastercard na kuja na teknolojia ambayo inaweza kubadilisha maisha ya wakulima. 

Uzoefu wetu katika sekta ya kifedha unatufanya kutafuta wadau kama Mastercard ambapo tumeona wamefanya vizuri nchini Kenya kuwasaidia wakulima kupitia programu ya '2KUZE'. 

Ndio maana nasi tumeungana kuhakikisha wakulima wadogo, wanunuzi na mawakala wananufaika kiuchumi," alisema Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Bussemaker. -- ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »