Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kulia), akipeana
mikono na Katibu Tawala Msaidizi (anayeshughulikia masuala ya serikali
za mitaa), jijini Dar es Salaam, Bi. Merry Assey, baada ya kufungua
semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Dar es
Salaam, iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika Januari 3, 2017 kwenye
makao makuu ya PSPF Golden Jubilee Towers jijini.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umeendesha semina ya mafunzo kwa watumishi wa
Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwajengea uwezo wa
kushughulikia matatizo ya wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo.
Mafunzo
hayo ya siku mbili, yameanza leo Januari 3, 2017, na kufunguliwa na
Katibu Tawala Msaidizi (sehemu ya serikali za mitaa), Bi. Merry Assey
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ea Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Niipongeze
PSPF kwa kuandaa semina hii ambayo inatoa fursa ya watumishi hawa
waliohudhuria katika mafunzo haya kuelewa huduma na shughuli
zinazofanywa na Mfuko huu na kwa maana hiyo iwe rahisi kwenu kutatua
kero za wananchi wanaofika pale Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta
ufumbuzi hususan kwa wanachama wa Mfuko huu,.” Alisema Bi. Assey, wakati
akifungua semina hiyo.
Akimkaribisha
mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, alisema, PSPF
ilifikia uamuzi wa kuandaa semina hiyo kufuatia wazo la Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, ambaye alitaka kujengewa uwezo kwa watumishi wa Ofisi
yake ili waweze kuwahudumia vema wananchi wakiwemo wanachama wa PSPF.
“Nililipokea
wazo hilo na sisi PSPF tukaona ni fursa nzuri kwa kuwaelimisha
watumishi hawa ambao, ninahakika baada ya mafunzo haya, watakuwa
mabalozi wetu wazuri lakini pia na wao watajiunga na Mfuko huu.” Alisema
Bw. Mayingu.
Mada
mbalimbali zilitolewa kwa wanasemina hao ikiwa ni pamoja na ile ya
shughuli za Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko huo, Bi.
Neema Muro, Kaimu Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi na Maafisa wengine wa
Mfujko huo.
Bi. Merry Assey, akifungua semina hiyo
Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza wakati wa semina hiyo
Mkurugenzi
wa Huduma wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Neema Muro akitoa mada juu
ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Pensehni wa PSPF
Kaimu Meneja Mafao wa PSPF, Bw.Haji Moshi, akitoa mada ya namna mwanachama wa Mfuko huo anavyoweza kupata mafao yake
Bw. Haji Moshi akitoa mada
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitoelwa na viongozi na maafisa wa PSPF
Baadhi ya washiriki wakipitia vijarida vyenye maelezo ya kina kuhusu huduma zitolewazo na PSPF
Mshiriki akisoma kijarida cha PSPF
Mkurugenzi
wa Huduma wa PSPF, Bi. Neema Muro, (wapili kulia), akiongozana na
Mameneja na maafisa wa Mfuko huo wakati wakielekea chumba cha semina
kutoa mafunzo kuhusu huduma za Mfuko
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa PSPF na Ofisi ya RAS, Dar es Salaam
Picha ya pamoja
Baadhi ya mameneja wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja na "meza kuu"
EmoticonEmoticon