Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua
mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar
es Salaam.
Mwimbaji Alfonsina Samweli
wa kanisa la Assemblies of God la Kinziga Salasala Jijini Dar es Salaam
akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kablasha lenye DVDs zenye nyimbo za
Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina akikata Utepe
katika CD kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya Nyimbo za Injili za mwimbaji
Alfonsina Samweli.
Sehemu ya waumini wa
kanisa la assemblies of God la Salasala. Wakisikiliza hotuba ya Mgeni
rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Hayupo Pichani wakati wa ibada maalumu ya kuiombea
Taifa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na Evelyn Mkokoi wa
OMR)
Na
Evelyn Mkokoi – Salasala DSM
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Luhaga Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za
Mungu katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.
Pia amesema Serikali ya awamu ya Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba
katika kutenda yaliyomema kwa maendeleo ya nchi kwa kuogopa maneno ya
watu ya kuwakatisha tamaa.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu
na Kuabudu na kuliombea Taifa la Kanisa la Tanzania Assemblies of God
lililopo katika eneo la Kinzugi Salasala, alisema Serikali itaendelea
kusimamia misingi yake bila kuogopa maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa
kwani Sheria na Katiba za nchi zinatokana na maneno yaliyopo katika
vitabu vya Mungu.
Alisema watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda
kazi zao kwani uongozi waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na
sio kwa nguvu za mtu yeyote.
" Uongozi unatokana na Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa
Waziri nilimaliza siku mbili sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri
kipindi hicho nilikuwa shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa
,nikasema ni uweza wa Mungu,"alisema na kuongeza kuwa
"Utawala wa awamu ya tano tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba
muendelee kutuombea tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo
mbalimbali katika kutekeleza majukumu yetu,"alisema Mpina
Aidha aliziomba familia za wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji
wa mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata
nafasi katika jamii.
"Familia za Kikristo lazima ziwe mfano wa kuigwa katika utunzaji
wa mazingira, hizi faini tunazowapiga watu kutokana na ukiukwaji wa
sheria za mazingira kwa uchafuzi wa Mazingira, sio kama tunawaonea
bali kuwakumbusha wajibu wao "alisema
Kwa Upande wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni
alisema watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya
awamu ya tano na viongozi wake.
Alisema roho za uadui zilizopo na watu kusema vibaya na kuwakatisha
tamaa kusiwavunje mioyo kwa kusikiliza maneno ya watu katika kuleta
maendeleo ya nchi kwa manufaa ya taifahili na watu wake.
"Makanisa na Misikiti tupo pamoja nanyi katika kuwaombea na kama
serikali hii ikiendelea hivi ndani ya miaka mitatu nchi yetu itabadilika,"alisema
Mch.Sabuni.
Ibada maalum ya Kuliombea Taifa, kusifu pamoja na kuimba, ilienda
sambamba na uzinduzi wa Ablum ya nyimbo za injili za mwimbaji Alfonsina
Samweli pamoja na mnadawa kuuza DVDs zenye nyimbo za injili.
EmoticonEmoticon