MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA WILAYANI MUFINDI WAPIGWA MSASA NA POLICY FORUM

December 05, 2016

 Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alikuwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA


Madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga wilayani mufindi wameongezewa makali ya kiutendaji  na uwajibikaji na shirika lisilo la kiserikali la policy forum kutoka jiji Dar es salaam.
Akizungumza na blog hii mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alisema kuwa mafunzo wanayopewa madiwani yanalengo la kuwaongezea uwezo wa utendaji wa kazi katika kata zao.
Aidha Chumi alisema kuwa ili kupata maendeleo ya halmashauri ya mji wa Mafinga ni lazima madiwani wawe na uelewa wa kuzishughulikia kero za wanachi na kuwa wabunifu wa kupanga mipango ya kuleta maendeleo.
“Ukiangalia madiwani wengi bado hawavijui baadhi ya vitu na kuhoji kutokana na kanuni na sheria za halmashauri hivyo nimeleta semina hii kuwaongezea uwezo madiwani wa jimbo la mafinga”.alisema Chumi
Nao baadhi ya madiwani walimshukuru mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi kwa kuwatafutia watu wa kuwapa elimu ya kiutendaji na kujua majukumu ya madiwani katika kuisimamia miradi ya halmashauri.
“Angalia tulikuwa hatujui mambo mengi na ndio chanzo tulikuwa tunamuingilia majukumu mkurugenzi kama tulikuwa tunakagua barabara za mji wa mafinga kumbe tulikuwa kinyume na utaratibu”.walisema madiwani wa mafinga
Kwa upande wake meneja uwajibikaji wa shirika lisilo la kiserikali la policy forum Richard Angelo alisema kuwa madiwani wengi wanakumbana na changamoto za kuisimamia halmashauri hivyo wameamua kuwa elimu ya kujua wajibu wao.
Hata hivyo Angelo alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madiwani na wabunge karibia wote lengo likwa ni kukuza uelewa na uwezo wa kuongoza maeneo wanayowaongoza.
“Hivi karibu tumetoa elimu kwa wabunge mjini Dodoma na ndipo mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi alituomba tuje kutoa elimu kwa madiwani wa jimbo lake na ndio maana ndio tupo hapa mjini Mafinga”.alisema Angelo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »