Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
jana Novemba 15, 2016 alimtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Seongnam,
Jae-myung Lee kumshukuru kwa namna ambavyo ameipokea timu ya taifa ya
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti
Boys.
Serengeti Boys walioko Korea kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa
ambako Jiji la Seongnam ni mshirika wa klabu ya Seongnam FC ambao ndio
wenyeji wa timu yetu ya vijana ambayo ilifanya michezo miwili ya
kirafiki ya kimataifa.
Katika mazungumzo kocha huyo, Meya Jae-myung Lee aliiakikishia TFF
kuwa jiji lake litaendelea kushirikiana na shirikisho katika kuendeleza
mpira wa vijana wakike na wakiume.
Katika kumtembelea Meya huyo, Rais Malinzi aliambatana na Mkurugenzi
wa Ufundi, Salum Madadi na benchi nzima la ufundi, linaloongozwa na
Kocha Bakari Nyundo Shime na msaidizi wake, Muharami Mohammed Sultan
pamoja na Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya soka la vijana, Kim Poulsen.
Baadaye jioni ya Novemba 15, 2016 Rais Malinzi alikutana na Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Korea Kusini (KFA), Chung Mong-Gyu
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Hyundai.
Rais wa KFA Mong-Gyu naye alihakikishia TFF kuwa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Korea litasaidia kuendeleza soka la vijana Tanzania sambamba na
kusaidia mafunzo ya makocha..
EmoticonEmoticon