NEMC YAPEWA MWEZI MMOJA KUKAMILISHA RIPOTI YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MTWARA

July 28, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina kushoto akipata Maelezo  kutoka kwa  Bw. Joseph ambaye ni Meneja uendeshaji wa kiwanda hicho kuhusu uchataji wa taka unaofanywa na kiwanda cha SBS wakati alipofanya ziara ya kukitembelea .(Picha na Evelyn Mkokoi)
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kulia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kushoto ni  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda wakigagua Dampo mpya la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira, wakati wa ziara yake.

Pichani ni Dampo la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira lililojengwa kwa hisani ya bank ya Dunia kwa thamni ya shilingi bilioni 8.8, mara litakapoanza kutumika litakuwa na uwezo wa kutengeza nishati mbadala.
Na Evelyn Mkokoi,MTWARA
 Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mzingira NEMC limepewa mwezi mmoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kupima vumbi, Moshi na Maji yanayotoka katika kiwanda cha kuchakata taka cha SBS kilichopo katika maeneo ya Mangamba Mjini Mtwara ili kujirisha kama vina madhara kwa mazingira na viumbe hai.

Naibu Waziri Mpina alitoa agizo hilo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira na kuangalia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa wenye viwanda nchini .

Amelitaka baraza hilo kufanya kazi zake kwa umakini na kutokukubali majibu ya vipimo toka kwa mwekezaji bila NEMC pia kufanya vipimo na kupatamajibu sahihi kutokana na sababu kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara juu ya uchavuzi wa mazingira unaofanywa na wenye viwanda unavyo hatarisha maisha yao na mazingira kwa ujumla.

Katika ziara hiyo ya mjini Mtwara, Naibu Waziri Mpina pia alitembelea Dampo la kisasa la lilijengwa kwa ufadhili wa Bank ya Dunia lenye thamani ya shilingi Bilioni 8.8 na kuwapongeza wana Mtwara kwa kupata Dampo la kisasa ambalo ni rafiki wa Mazingira, na kuwashauri waratibu wa mradi huo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kuanza kulitumia ambapo taka zitakazowekwa  pia zinaweza kutumika kutengeneza nishati mbadala.

Awali, akitoa taarifa ya Mazingira ya Mkoa wa Mtwara, katibu Tawala wa Mkoa huo,Afred Luanda, alisema kuwa Mkoa huo unakabiliana na changamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu wa kutumia mabomu, ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa, vifaa vya uondoshaji taka pamoja na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Katika ziara ya naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara leo ilihusisha pia kutembelea Bandari ya mtwara ili kujionea utekelezaji wa sheria ya mazingira katika uingizwaji wa viwatilifu na kemikali hatarishi kwa mazingira zinazoingizwa  kupitia bandari hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »