Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa
kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika
Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya
kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika
Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na
Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani)
atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania
(TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni
mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro
Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati
ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016
ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars.
Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka
EmoticonEmoticon