Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika
picha ya pamoja na Wakuu wa Idara, taasisi na vitengo vilivyo chini ya
Wizara hiyo mara baada ya kumaliza kikao kazi na viongozi hao leo jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(katikati
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi
za wizara hiyo leo jijini dar es salaam baada ya kumaliza kikao kazi
na viongozi hao.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia)
akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.Assah
Mwambene(kushoto) mara baada ya kikao kazi kilichofanyika leo hii jijini
Dar es Salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Mwandishi Maalum – Maelezo
Vyombo vya habari nchini
vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa taarifa kwa wananchi
wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa 10 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa leo na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na viongozi wa menejimenti ya
wizara na taasisi zake kwenye kikao cha kazi kilichofanyika jijini Dar
es Salaam.
Prof. Gabriel alisema kipindi cha
uchaguzi vyombo vya habari vilifaya kazi kubwa ya kuwahabarisha
wananchi habari za uchaguzi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao na
hivyo kuwawezesha wananchi kujua mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea
hapa nchini.
Katibu Mkuu huyo ambaye hicho
kilikuwa ni kikao chake cha kwanza tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa
wizara hiyo mwishoni mwa mwezi wa kumi aliahidi kuwatumikia na
kuwaheshimu wafanyakazi wa wizara yake huku akisimamia majukumu ya kazi
kwa kufauata kanuni, taratibu na sheria za utumishi wa Umma.
“Hiki ni kikao chetu cha
kujipanga kwa ajili ya kazi, ni vyema tukajipanga huku tukijuwa
matarajio ya Mhe. Rais kwetu ni yapi, wananchi tunaowatumikia
wanategemea kupata nini kutoka kwetu na mimi kama Katibu Mkuu natarajia
kupata nini kutoka kwenu”, Prof. Gabriel alisema.
Akimkaribisha Katibu Mkuu huyo
kuongea na viongozi hao Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu
Titus Mkapa alisema kikao hicho ni maalum kwa ajili ya wizara kujadili
utekelezaji wa mipango ya wizara kwa kasi.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati
tofauti viongozi hao waliiomba Serikali iangalie upya bajeti ya wizara
hiyo ambayo ni ndogo ili iweze kuongezwa na kuwawezesha kufanya kazi
zao kwa ufaisi zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TasuBa) Michael Kadinde
alisema chuo hicho kimekuwa kikizalisha ajira kwa wanafunzi wanaosoma
hapo mara baada ya kumaliza masomo yao lakini wanafunzi wengi
wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na ada.
“Kuna baadhi ya wanafunzi
wanajiunga na chuo hiki wakiwa na elimu ya darasa la saba, na hivi sasa
Serikali itaanza kutoa elimu bure kwa wanafunzi kwa darasa la kwanza
hadi kidato cha nne”.
“Ninaiomba Serikali iweze
kuwaangalia wanafunzi hawa wa darasa la saba ambao wanasoma chuoni kwetu
ili nao waweze kupata elimu bure sawa na wanafunzi wa Sekondari”,
alisisitiza Kadinde.
Kikao hicho kimeitishwa kufuatia
kikao cha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Makatibu wakuu, manaibu
makatibu wakuu na watendaji wakuu wa Serikali kilichofayika mwishoni
mwa wiki ambapo alieleza matarajio yake na matarajio ya wananchi katika
uongozi wake. Hivyo aliagiza kila sekta ikae na kujipanga kufanya kazi
ili kukidhi matarajio ya wananchi.
EmoticonEmoticon