Ripoti kutoka Bujumbura zinasema
kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre
Nkurunziza kama Rais wa Burundi
Meja Jenerali Godefroid
Niyombareh(Pichani juu) amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura,
kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa
hilo kwa kipindi cha mpito.
Kulingana na taarifa
iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon’golewa
madarakani. Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo
baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya
urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na
Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu
mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Kwa sasa rais Nkurunziza
yuko nchini alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya
Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza
atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ”Mapinduzi”
-BBC Swahili, Reuters
EmoticonEmoticon