MAFUNZO YAANZA VEMA LIGI KUU ZANZIBAR

September 18, 2014
Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
TIMU ya Mafunzo imepata ushindi mwembanba wa bao 1-0 dhidi ya Mtende Rangers katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar uwanja wa Amaan jioni hii.
Mchezaji Sadik Habib ndiye aliyepeleka kilio kwa wakulima hao wa viazi kutoka Mkoa wa Kusini Unguja, akipachika bao hilo mnamo dakika ya 60 ya mchezo akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na mwenzake Ali Juma.
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Amaan, timu hizo zilionesha soka la ushindani na kushambuliana kwa zamu, lakini hadi mapumziko milango ilibaki kuwa migumu kufunguka.
Wachezaji wa Mafunzo wakishangilia ushindi wao

Mafunzo iliyoongozwa na Hemed Suleiman ‘Moroko’ kocha wa zamani wa Zanzibar Heroes na Coastal Union, ilicheza kwa kujiamini na kupeleka mashambulizi mengi lakini washambuliaji wake Sadik Habibu na Rashid Abdalla walishindwa kutumia vyema nafasi nyingi walizozipata.
Moroko amepewa jukumu la kuinoa Mafunzo kwa muda kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo Mohammed Shaaban ‘Kachumbari’, kulazimika kutokukaa benchi kwa kukosa Leseni C kama agizo la Shirikisho la Soka Afrika linavyoelekeza.
Na katika uwanja wa Gombani Pemba,  wanagenzi wa ligi hiyo Shaba FC, wametoka sare ya 1-1 na maafande wa 1-1 dhidi ya JKU.
Mchezaji Is-hak Othman aliifungia JKU dakika ya 18 kabla Suleiman Ali kuisawazishia Shaba dakika ya 65.
Kesho na Jumamosi ni mapumziko na Jumapili ligi hiyo itaingia mzunguko wa pili kwa mchezo kati ya Shaba na Polisi uwanja wa Gombani, na Miembeni na Chuoni watakipiga uwanja wa Amaan.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »