Kulia
ni Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo akisalimia na Mkuu wa
wilaya ya Tanga,Halima Dendego mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege
Tanga akiwa ameambana na timu hiyo wakitokea Pemba walipokuwa wamweka
kambi wa kwanza kulia anayemtabulisha ni Meneja wa Coastal Union Akida
Machai na kushoto ni Katibu Mkuu wa Coastal Union Kassim El Siagi,Picha
KWA HISANI YA COASTAL UNION
Msafara
wa Coastal Union ukiongozwa na pikipiki na Baiskeli zisizokuwa na idadi
wakipita katika mitaa mbalimbali jijini Tanga kabla ya kuelekea kwenye
Kambi yao iliyopo Raskazoni Jijini Tanga.
Mkuu
wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akizungumza na waandishi wa habari
katika uwanja wa Ndege jijini Tanga mara baada ya timu ya Coastal Union
kuwasili katika uwanja huo ikitokea visiwani Pemba ilipokuwa imeweka
kambi ya mwezi mmoja ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania
bara
Na Mwandishi Wetu, Tanga.
MKUU
wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego leo ameongeza mapokezi ya timu ya
Coastal Union yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga ambapo
timu hiyo ilikuwa ikitokea Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi kwa
muda wa mwezi mzima.
Akizungumza
wakati wa mapokezi hayo DC Dendego amesema kuwa serikali ya wilaya hiyo
haitasita kuchukulia hatua watu wote wanaoleta migogoro na chokochoko
ndani ya klabu ya Coastal Union kwa sababu wasiposhughulikiwa wanaweza
kupelekea kuwagawa wanachama,wapenzi na mashabiki hivyo kudhoofisha
maendeleo.
Wachezaji
hao walitua uwanja wa ndege Tanga wakitumia ndege mbili tofauti ambapo
baada ya hapo Mkuu huyo wa wilaya aliweza kuongoza msafara wa magari
zaidi ya 50,pikipiki na baiskeli zisizokuwa na idadi zilizunguka maeneo
mbalimbali jijini Tanga huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuilaki
kila ilipokuwa ikipita kwa kuimba nyimbo za kuisifu timu hiyo.
Baada
ya mzunguko huo ambao ulichukua takribani saa moja ndipo wachezaji wa
timu hiyo wakawasili kambini eneo la Raskazone Hotel Pembezoni mwa
bahari ya hindi ilipo kambi yao hivyo.
Dendego
amesema kuwa lazima wao kama serikali wahakikisha klabu zao mkoani hapa
zinakuwa na utulivu kila wakati kwa hiyo inapotokea inakwenda kunyume
chake basi wao watachukua hatua kali ili iweza kuwa fundisho kwa watu
wengine ambao wanaweza kufanya hivyo kipindi kingine.
Hata
hivyo amesema kuwa lazima wapenzi ,wanachama na mashabiki kuhakikisha
wanakuwa na mshikamano wa thati ili kuweza kuhakikisha timu hiyo
inafikia malengo yake waliojiwekea kwenye msimu mpya wa Ligi kuu soka
Tanzania bara.
Kwa
upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kuwa
timu hiyo ilifanya usajili mzuri msimu huu hivyo wana matumaini makubwa
ya kufanya vizuri kwa kuanzia na mechi yao na Simba ambao haiwapi
wasiwasi wa aina yoyote ile.
El
Siagi amesema kutokana na maandalizi timu hiyo walioifanya wakiwa
visiwani Pemba wana matumaini makubwa ya kuibuka na pointi tatu muhimu
mbele ya Simba mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu itakayochezwa uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali
akizungumza katika mapokezi hayo,aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal
Union,Hemed Aurora amewataka wapenzi ,wanachama kudumisha na kuendeleza
mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuweza kufikia malengo yao ya
kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Umoja
na mshikamano ndio siri ya mafanikio yoyote yale hivyo nawasihi wapenzi
,mashabiki na wanachama muenzi mshikamno kwa sababu ndio nuru ya
mafanikio kwenu “Alisema Aurora.
EmoticonEmoticon