February 02, 2014

*YANGA YAICHAPA MBEYA CITY BAO 1-0 NA KUBAKI NAFASI YA PILI, AZAM FC YAIRARUA KAGERA SUGAR MABAO 4-0

 Mshambuliaji mwenye speed 120 wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa (kuashoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Mbeya City, Deogratias Julius, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. 
Katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Mrisho Ngassa , katika dakika ya 15 ya mchezo huo, bao lililodumu hadi kipyenga cha kuashiria kumalizika kwa dakika 90 za mchezo. 
Kwa bao hilo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 35 huku ikiendelea kuwa nyuma ya Azam Fc waliofikisha Pointi 36 baada ya kuwafunga Kagera Sugar katika mchezo wao uliopigwa katika dimba la Chamazi, leo jioni kwa jumla ya mabao 4-0.

Mbeya City wanabaki nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 31 sawa na Simba wenye Pointi 31 wakitofautiana kwa idadi ya magoli.

Aidha katika mchezo huo mchezaji Steven Mazanda, wa Mbeya City, alizawadiwa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu.

Mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa siku ya jumatano mjini Morogogoro, ndiyo unaoweza kutoa taswira kamili ya nani kati ya Simba na Mbeya City atabaki katika nafasi ya tatu.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia kwa pamoja bao lililofungwa na Mrisho Ngassa katika kipindi cha kwanza. 
 Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Ngassa.
 Mashabiki wa Mbeya City, wakiwa wamepoa baada ya kufungwa bao hilo.
 Kiungo mwenye chenga za maudhi wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akiwatoka mabeki wa Mbeya City.
 David Luhende wa Yanga (kulia) akimiliki mpira mbele ya beki wa Mbeya City.
 Simon Msuva wa Yanga, akimtoka beki wa Mbeya City.
 Kikosi cha kwanza cha Yanga.
Kikosi cha kwanza cha Mbeya City.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »