RAISA SAIDI,BUMBULI.
Naibu Waziri
wa Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia January Makamba
amewataka baadhi ya watu
kuondokana na dhana ya
kusema mgogoro wa
kiwanda cha chai cha
Mponde ni siasa badala
yake amewataka kuiacha serikali
indelee na taratibu zake za kulitafutia
ufumbuzi swala hilo.
Makamba
ambaye pia ni Mbunge
wa jimbo la
Bumbuli alisema yeye kama
mbunge wa eneo hilo lazima
ashirikiane na wananchi
wake na si kikundi
cha watu wachache licha ya kutukanwa kwa
kuwaunga mkono wananchi wake.
Naibu waziri
huyo alieleza kusikitishwa
kwake na baadhi ya
watu kusema swala
hilo ni la
kisiasa na kwamba linamaslahi
binafsi ambapo alisema ni upambuvu nakwamba tangu
2010 wakati wa
uchaguzi ulishapita sasa ni wakati
wa kuleta maendeleo
kwa wananchi waliomuamini
na kumtuma kuwa
muwakilishi wao bungeni na si vinginevyo.
“Siamini kama
kuwaunga mkono wananchi
walionichagua yanatokana na tofauti za kisiasa kwani eneo hili
linamilikiwa na Chama kimoja ambacho ni Chama cha Mapinduzi na wala sina maslahi binafsi katika suala hilo”
Alisema Makamba nakuongeza
kuwa yeye anawasimia
wakulima wa zao la chai
kupata haki yao ya
msingi .
Kiwanda cha Mponde kimefungwa takribani
miezi mitano sasa kufuatia wakulima kususa kupeleka majani
mabichi ya chai kwa madai ya kutaka Uongozi wa Chama cha Wakulima wa Chai Usambara
(UTEGA) uitishe Mkutano Mkuu na kuwasomea mapato na matumizi ya chama hicho
ikiwa ni pamoja na mapato ya kiwanda ambacho kinamilikiwa na chama hicho.
Hivi karibuni Makamba, alimwaga machozi hadharani
katika kijiji cha Mponde Kweminyasa kutokana na taarifa za watu watano
kujeruhiwa kwa risasi za moto kufuatia vurugu zilizotokea kati ya wakulima wa zao la chai na Jeshi la polisi.
Vurugu hiyo ilitokea kutokana na Mkuu wa Mkoa
wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuamuru kiwanda cha chai cha Mponde
kilichokuwa kimefungwa kwa mwezi mmoja na nusu wakati huo kifunguliwe kwa nguvu chini ya usimamizi wa
Polisi jambo ambalo zilisababisha
vurugu kubwa mpaka
watu kujeruhiwa kwa
risasi za moto.
Makamba alisema kuwa
kuna haja kubwa ya kuwepo maridhiano katika kufungua kiwanda hicho badala ya
kutumia nguvu. “Unaweza kufungua kiwanda kwa bunduki lakini huwezi kukiendesha
kwa bunduki,” alisema na kuwataka wakulima wa Chai wa Mponde kuwa na subira na
uvumilivu kwa sababu haki yao haiwezi kupotea kwa sababu kiwanda hicho ni mali
yao.

EmoticonEmoticon