Uhuru,Boban wajaza mashabiki mazoezini

July 15, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
WACHEZAJI waliosajili na timu ya Coastal Union ya Tanga,Uhuru Seleman na Haruna Moshi "Boban"jana walikuwa kivutio kikubwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.
 
Baada ya wachezaji hao kutua uwanjani hapo mashabiki wa soka mkoani hapa walianza kuingia kwa wingi huku wakiwa makini kuangalia aina ya uchezaji wao huku wengine wakiwashangilia mara kwa mara waliokuwa wakigusa mipira.
 
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi hayo,Uhuru alisema lengo la kuichezea klabu hiyo ni kuipa ushindi timu hiyo na  pamoja na kuisapoti timu hizo ifikie malengo yake iliyojiwekea kwa siku zijazo.
 
Uhuru alisema endapo wachezaji wanzie wataunganisha nguvu ya pamoja itasaidia timu hiyo kufikia malengo yake ya kuuutwaa ubingwa wa ligi kuu kwani hilo linawezekana iwapo mshikamano baina ya wachezaji utakuwepo.
 
"Ninaamini Coastal Union ni sehemu nzuri ya kuirudisha nafasi yangu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)kwa sababu niliwahi kuchaguliwa kuichezea timu ya Taifa nikitokea Coastal Union "Alisema Uhuru.

Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Hemed Morroco aliwataka wachezaji ambao hawajawasili kwenye mazoezi kuwasili ili kuweza kuunganisha nguvu za pamoja kufanya maandalizi kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
 
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »