MKINGA wakubaliana na Agizo la RC Gallawa.

May 02, 2013
Na Oscar Assenga,Mkinga.

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wamesema kimsingi wamekubaliana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Chiku Gallawa lakuzuia ugawaji wa eneo katika msitu wa Segoma kwa manufaa ya uhifadhiwa mazingira.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga,Andrew Ngoda alitoa taarifa hiyo jana wakati akifafanua juu ya maazimio ya kikao cha baraza la madiwani lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita juu msitu huo wa Segoma.

Alisema licha ya kuwa kulikuwa na mvutano katika kikao cha baraza hilo huku baadhi ya madiwani wakitaka eneo la msitu huo limegwe ili wanavijiji vinavyouzunguka wagawiwe lakini kimsingi mwisho wa majadiliano baraza liliamua kwa kauli moja kukubaliana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga la kuzuia.

“Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga pamoja na kwamba lina mamlaka ya kufanya maamuzi yake lakini katika hili la msitu wa Segoma haliwezi kupingana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa sababu ina lengo la kuhakikisha msitu huo unadumu na uhifadhi wa mazingira unaendelea”alisema Ngoda.

Aidha maazimio katika kikao hicho walikubaliana kuwa kwa kuwa lengo la mkuu wa mkoa ni uhifadhi wa mazingira jambo ambalo ni la msingi hivyo baraza lilikubaliana kwamba msitu huo uendelee kuwa hifadhi lakini uwe chini ya wanakijiji cha Segoma.

MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »