MASHINDANO ya Vijana ya
Kombe la Gambo Cup yanatarajiwa kuingia hatua ya pili katika kituo cha Tarafa
ya Mombo wilayani humo ambapo timu nne zimefanikiwa kucheza hatua hiyo ambayo
itachezwa kwa mtindo wa mtoano.
Mashindano hayo ambayo
yalianzishwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Mrisho Gambo na kufadhiliwa na benki ya
NMB yakiwa na lengo la kuinua vipaji vya wachezaji wachanga pamoja na kukuza
kiwango cha soka wilayani humo.
Mratibu wa Mshindano
hayo, Zaina Hassani alilimbia gazeti hili kuwa hatua hiyo katika kituo hicho
inatarajiwa kuwa ni ngumu kuliko hatua iliyomalizika kutokana na ushindani
uliokuwepo kwani kila timu ilitaka kuingia hatua hiyo.
Hassani ambaye pia ni
katibu wa chama cha soka wilaya ya Korogwe,(KDF)alizitaja timu ambazo
zilifanikiwa kucheza hatua hiyo ya mtoano katika kituo cha Mombo ni Reli
Fc,Mwisho wa Shamba, Mkumbara.
Katika kituo cha Makuyuni zilizofanikiwa kuingia ni
Rangers Fc,Madago Fc na Gomba huku kituo cha Mswaha kikiingiza timu mbili
ambazo ni Kosovo na Mafleti.
Katibu huyo alisema timu
hiyo zilifanikiwa kucheza hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika hatua ya
makundi na kuweza kupatikana timu nane ambazo zilicheza kwa mfumo wa mtoano ili
kuweza kumpata bingwa wa tarafa ya Mombo ambaye atacheza hatua ya fainali
pamoja na mshindi wa pili.
Akizungumzia mashindano
hayo,Mwenyekiti wa Chama cha soka wilayani humo,Peter Juma alisema yamekuwa na ushindani
ikiwemo kuleta hamasa kwa wadau wa soka pamoja na kupelekea vijana kupenda
michezo na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa mkuu huyo wa wilaya kwa
kuanzisha ligi nyengine lengo likiwa ni kuinua vipaji vya soka.
Mwisho.
EmoticonEmoticon