Yanga na Mgambo Shooting ngoma droo.

April 17, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU za soka Mgambo Shooting na Yanga leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1,ikiwa ni mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha andanda nzuri na la kuvutia.

Si Yanga wala Mgambo ambayo itashindwa kujilaumu kutokana na nafasi za wazi ambazo waliweza kuzipata na ushindwa kuzitendea haki kutokana na wachezaji wao kushindwa kuzitumia vema.

Mgambo ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lao kupitia Issa Kanduru katika dakika ya 42 baada ya kumalizia krosi ya Salum Mlima na hatimaye kuweza kukwamisha wavuni bao hilo.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Yanga waliingia uwanjani hapo na hari na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwenye kikosi chao.

Wakionekana kujipanga na kucheza kwa umakini mkubwa Yanga waliweza kupata bao lao la kusawadhisha kwenye dakika ya 86 kupitia Saimon Msuva.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »